CHADEMA walikosea kukubali kuichoma nchi wanayotaka kuiongoza

SAwa, Mwambie Heche atangaze maandamano uone watanzania wanafanya nini. Hakuna chama tena kuna magaidi, wananchi wanajificha majumbani mwao, hakuna duka linafunguliwa wakati kodi ya pango inabaki vilevile hata kama ukifunga duka kwa wiki 3
Ila anasikilizwa, anapendwa ,na anasema ukweli kabisa.

Wananchi tunaona ana haiba kubwa na utu wa kweli leo namtumia tena jioni elfu kumi
 
Hakuna chama kipya kinakuja madarakani pamoja na ofisi zake za serikali, majeshi, polisi, mahakama, barabara, hospitali, mahakama na majaji wake wapya. Watatumia miundombinu hiihii na rasilimali watu iliyopo, maana miundombinu hii sio mali ya chama kilichoko madarakani wala Rais, ni mali ya watanzania hata wale ambao hawajazaliwa. Kuichoma moto na kuiharibu sio sawa na kosa kubwa sana.

Hakuna mahali popote nimesikia chama cha chadema kimekerwa na kuharibiwa kwa mali/kodi za watanzania katika vurugu za Octoba 29, 2025 na siku zilizofuata siku hiyo. Hii ni kuonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wachomaji na chadema, la sivyo, walifurahishwa na uchomaji ule.

Hayati Reginald Mengi (RIP) alikuwa miongozi mwa watu wa kwanza nchini kumiliki vyombo vya habari. Kila wakati unapokaribia uchaguzi mkuu alikuwa akitumia vyombo vyake vya habari kutuonyesha watanzania ubaya wa kuvunjika kwa amani kunakoweza kuletwa na vurugu za uchaguzi na vyama vya upinzani. Nadhani alikuwa mwanaCCM lakini alifanyahivyo kwa kusukumwa na umuhimu wa amani na utulivu katika uwekezaji wake nchini. Kwenye vurugu mitaji inapotea.

Mzee Mengi alikuwa anatuonyesha vita na mauaji ya Rwanda, Burundi na Somalia kwenye kituo chake cha TV. Wapinzani walimlaumu sana kuwa anawatisha watanzania wasivichague vyama vya upinzani. Leo Mengi hayupo lakini nchi ilichomwa moto na watanzania wenzetu wamepoteza maisha wakati wa uchaguzi sawasawa na hofu na tahadhali yake.

Kuchoma au kuunga mkono kuchoma nchi/malalo yetu ni kosa la kiufundi ambalo chadema walilifanya katika harakati zao za kisiasa. Wamekirudisha chama kilometa nyingi sana nyuma. Leo hii chadema kinaogopwa na wananchi kama chama kisichowatakia mema wananchi na taifa. Mwananchi ambae amepoteza mtoto wake kwenye vurugu zile anawalaumu chadema, waliokosa matibabu wakati wa vurugu wanailaumu chadema, waliokosa usafiri wa mwendokasi kwakuwa umechomwa moto wanailaumu chadema, waliokosa ajira kwakuwa sheli na malori waliyokuwa wameajiliwa yamechomwa moto wanailaumu chadema; watoto waliokosa masomo kwa kule kufungwa kutokana na vurugu wanailamu chadema; walioshindwa kutoka nje kujitafutia riziki kwasababu ya vurugu wanailamu chadema, waliofilisika kwasababu maduka yao yaliporwa kwenye vurugu wanailaumu chadema na viongozi wao akina heche; wanaokosa huduma kwenye ofisi za serikali za mitaa na kata zilizochomwa wanailaumu chadema; chadema, chadema, chadema.

Matokeo yake ni nini, leo hii ni rahisi sana kuyazuia maandamano ya chedema kuliko wakati mwingine wowote. Wakiitisha maandamano wananchi wooote wenye akili timamu wanabaki majumbani mwao na biashara zote zinafungwa kupisha maandamano ya chadema. Barabara na mitaa inabaki tupu, na hata wanaojitafutia riziki zao kwa kutoka kila siku kama bodaboda, daladala, mama lishe na wauza mboga wanakubali kukaa ndani na njaa ili kunusuru roho zao dhidi ya chadema na polisi. Chadema Wakiendelea kufanya hivi kwa muda mrefu watanzania hawa waliozoea amani wataifuta chadema vichwani mwao na kuwalinganisha na magaidi au watia hasara au wapenda vurugu au wapenda vita.

chadema kitabakia kuwa chama cha watu na vijana wapenda vurugu/wabwia unga, wavuta bangi na wasiokuwa na chakupoteza. Hata kwenye vurugu zile ni watoto wasiokuwa na chakupoteza tu ndio waliathirika; hakukuwepo na watoto wa wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi, maprofesa wala watumishi. Wengi wao walikuwa ni watoto wa masikini kabisa waliotolewa kafara na watu wanaowaamini na kuwaheshimu sana kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiroho. Watu ambao walikuwa wanajua kuwa vijana wale kwa kuchoma mali za umma na hata zile zinazolindwa kwa bunduki lazima wangeuliwa na kujeruhiwa kwa wingi. Hesabu zao zilikuwa wangeuliwa wachache tu na wengine watafanikisha lengo lao kwakuwa walijua kuwa polisi wengi walikuwa kwenye malindo ya kulinda uchaguzi. Bahati yao mbaya ni kwamba mikoa mingi na watanzania wengi hawakujitokeza kuunga mkono vurugu zao kama walivyokuwa wamekusudia. Hii ilisababisha Vijana waleta vurugu wakaminywa wote na kunyanyua mikono, bila hivyo serikali na watanzania wote tungekuwa tunashuhudia magofu kila kona. Yaani tungerudi nyuma miaka 50 kimaendeleo.

Chadema imetumika tu kama mtu wa mwisho/loud speaker nyuma ya wapanga mipango wakubwa wenye maslahi ya kibiashara nyuma ya pazia. Vurugu tunazoziona msingi wake mkuu sio demokrasia, bali biashara haramu ambazo zilivurugwa na utawala mpya wa Rais samia. Mpango ambao ulianza kwa kumnyang'anya Mbowe chadema ili kitumike kama jukwaa lao la kufanikisha kile wanachokidai/maslahi.

Samia amevuruga biashara zao haramu nyingi sana. Kulikuwa na mipango kabambe ambayo ilikuwa inafanyika wakati wa JPM, ambayo ghafla iliingia hitilafu baada Rais JPM kufa ghafla ambayo hawakuwa na uhakika kama Samia angeruhusu waendelee nayo kama ilivyo au Samia angehamia kwa watu wengine kama Rostam, nk.

Vita hii sio ya kidemokrasia hata kidogo, ni vita ya maslahi.
Lissu aliwadanganya kwamba wanaweza kuichukua nchi kwa kutengeneza mazingira ya kihuni ( political blackmailing ) kwamba wafanya fujo ikitokea wakadhibitiwa basi watazililia taasisi za kimataifa kwa kigezo cha kuonewa pia kwa kigezo cha kudai haki yao ya msingi.

Mbinu chafu zenye kufanana na namna kule Uturuki walivyotaka kumuondoa Rais wao na kule Iran ambapo Marekani aliamua kuwauzia fujo vijana wao ili aweze kupata uhalali wa kuianzisha vita.

Hawa wanasiasa wa upinzani wanapita njia zile zile chafu ambazo Marekani na wakubwa wengine wamezitumia mara kadhaa katika kupata uhalali wa uvamizi.

Kibaya kwa Lissu na wengi walio chini yake wamekuta kwamba mfumo wa ulinzi wa Tanzania umejichimbia sana kwenda chini kuliko walivyodhania.
 
Ukiitisha maandamano wananchi wote wanajifungia ndani na barabara zote zinabaki nyeupe, biashara zinasitishwa kuna chama tena hapo? Magaidi.
Muda unavyozidi kwenda wanakimbiwa na vijana waliodhania kwamba maandamano yanakuja na suluhisho lolote kwenye maisha yao.

Wanadhani kuwa kupita kwa muda kuna faida kwenye siasa zao kumbe kinachokuja kutokea ni kinyume na matarajio yao ya kisiasa.

Wanadhani kuwepo kwa utulivu siku wanazoitisha maandamano ni ushindi kwao kumbe ukweli ni kinyume chake.
 
SSH wanamletea siasa za kihuni lakini wenye umri fulani tunaiona tofauti ya anachokifanya na kile walichokifanya watangulizi wake.

Pale Kawe ulipokuwa uwanja wa mpira yamejengwa majengo 10 ya ghorofa yanalipamba jiji la Dar.

Nyuma ya hayo maghorofa kulikuwa na yale majengo ambayo hayati JPM alikataa kuyamalizia kwa sababu akiamini kwamba bosi wa THB Jeremiah Msechu amepiga pesa kwenye michakato ya ujenzi na majengo yake yakaendelea kufanana na magofu.

Kaingia SSH anayamalizia kwa kasi ya ajabu yanaipendezesha mandhari ya jiji la Dar, hizi ni kazi ngumu ambazo Rais kazifanya kwa muda wa miaka mitano, huwezi kuwasikia jamaa zake Lissu wakiongelea michakato ya kuinua uchumi inayofanyika muda huu.

Kuuamini katika siasa za uchochezi kwa dhana potofu kwamba SSH ni mzenji mwenye haki ya kubaguliwa ni mlango mbaya sana wenye kuweza kabisa kuliangamiza Taifa la Tanzania lililojengwa kwa kipindi cha miaka 65.
 
Unahitaji kuwa na ujinga huu ili kuitetea CCM. Wewe hujui watoto shule za mjini wanakaa chini, hujui kuwa Mwanza mjini ilipo lake Victoria, kuna kaya nyingi hazina maji, hujui kuwa hospitali nyingi matibabu ni changamoto. ? Kinachoshangaza huu uongo mnamuambia nani, maana watanzania wanatambua hali halisi.
Mkuu tembea Tanzania nzima uone mengi mema yanayofanyika usichague maeneo machache yenye changamoto zinazoendelea kutatuliwa.

Jenga tabia ya kuitazama glasi ya maji ikiwa robo tatu imejaa sio kuishi na mtazamo kwamba glasi ipo robo tatu imepungua maji.

Live with a notion in your head that a glass of water is half full not half empty.
 
Hizi notion za kupambuzana na kulaghaiana.

Bro, nimetembea 95% ya nchi hii. Ninajua namna serikali inavyofanya kazi. So, najua why tuko Masikini katika nyanja zote za kimaisha.

HATUNA ACCOUNTABILITY SYSTEM NCHINI KWETU, NA SULUHU YAKE NI KUWA NA KATIBA ITAYOTENGENEZA MIFUMO YA UWAJIBIKAJI, KWA KUONDOA 1. MIFUMO YA CHAMA KIMOJA NA KUWA NA MIFUMO YA VYAMA VINGI. 2. KUPUNGUZA MADADARAKA YA RAISI NA KUMFANYA AWE MUWAJIBIKAJI ZAIDI KWA WANANCHI KAMA MKUU WA SERIKALI AMBAYE TUNAMKABIDHI KODI ZETU ILI ATULETEE MAENDELEO KULIKO HUU UJINGA WA SASA WA KUONA KAMA RAISI ANAFANYA HISANI KWETU WITH DIVINE RIGHT. 3. KUUFANYA MUHIMILI WA MAHAKAMA UWE HURU KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ILI KUWEZESHA UWAJIBIKAJI WA TAASISI ZA UMMA KUWA MKUBWA ZAIDI, MFANO IWE RAHISI KWA WANANCHI KUYASHITAKI MASHIRIKA NA VIONGOZI KWA KUTOWAJIBIKA.

Katiba Mpya itamaliza shida zote? Hapana, ila itajenga mwanzo na msingi wa Mazingira ya uwajibikaji nchini. Nchi zote duniani zilizoendelea zimeendelea sababu ya mazingira ya kisheria yaliyotengeneza uwajibikaji.

So, acha hizi pumbaza za kutazama Glass Nusu imejaa, wakati tunahaki na uwezo wote wa hiyo glass kuwa imejaa. Wanaopaswa kuijaza glass wanapaswa waijaze na nilazima tuwalazimishe waijaze. Raia tukiwa na mindset hizi, hao wanaopaswa ijaza glass watawajibaka vipi?

We Need MASS DEMOCRATIC ACTION.
 
Endelea kukumbatia imani potofu, Kenya wanayo katiba mpya mpaka kesho wanasiasa wanaiba mabilioni ya pesa za wananchi.

Hakuna mahali dunia ambapo glass inajaa, ni mitazamo chanya itakayotutoa hapa tulipo na kutusogeza mahali pazuri zaidi, kwa kutafuta maarifa na elimu za darasani tutaweza kufanya ya maana kimaendeleo.

Katiba ni karatasi tu, Rwanda wanayo katiba mbovu lakini kila kukicha wanapiga hatua za kimaendeleo. Dubai yule mfalme alifungia siasa tangu miaka aliyoanza kuongoza wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Wazo la maana ni kuifanya katiba ikawa chombo cha maendeleo, kiwe chombo chenye kurahisisha shughuli za kimaendeleo, ndio kilichoandikwa kwenye kitabu kilichozinduliwa jana pale Arusha, kwamba tunahitaji sheria ambazo zitayarahisisha maisha yetu sio hizi kelele za katiba katiba!.
 
Kama hujui hata maana ya Katiba hatuwezi elewana.
 
Sipendi mitazamo ya kitumwa, ya kukaririshwa kutoka kwa wanaharakati wenye kuwafanyia kazi wazungu kwa siri.

Kimezinduliwa kitabu kuhusiana na mwelekeo wa Tanzania katika kuufikia mwaka 2050 humu kuna madini ya maprofesa wa chuo kikuu wakishirikiana na AG Hamza Johari tafuta nondo humo zitakusaidia.
 
Wewe ndio una mtazamo wa kitumwa. Kwanini unaamini mtazamo wangu huu unatokana na wanaharakati? Yaani mimi siwezi kuwa na mawazo yangu binafsi? What a rubbish way of thinking is this!!!
 
Tulikuwa na maandiko hayo ya kufikia 2025? Niambie umasikini umepungua kiasi gani nchi hii?
1.jpeg
 
Wewe ndio una mtazamo wa kitumwa. Kwanini unaamini mtazamo wangu huu unatokana na wanaharakati? Yaani mimi siwezi kuwa na mawazo yangu binafsi? What a rubbish way of thinking is this!!!
Rubbish way of thinking inaonekana tu huhitaji kuandika gazeti zima.

Msikaririshwe kwamba katiba itatatua kila kitu, ukiwa huna ubunifu kichwani hakuna katiba mpya itakayobadili chochote miongoni mwa watanzania.

Dubai hawana katiba mpya lakini hatuwafikii kwa maendeleo.

Rwanda hawana katiba rafiki kwa wanaharakati lakini kasi ya maendeleo yao ipo juu sana.
 
Tulikuwa na maandiko hayo ya kufikia 2025? Niambie umasikini umepungua kiasi gani nchi hii? View attachment 3628968
Unasoma kilichoandikwa humo ndani, tatizo letu wabongo ni kuwa negative mno yaani tunapitiliza.

Hayo maandiko hatuyasomi tunakuja kulaumu baadae vitu vilivyoelezewa kwa kina na vyenye kuhusiana na maisha yetu wakati tulichotakiwa kufanya ni kupata maarifa kutoka kwenye maandiko ya watu mbalimbali.
 
We Unaliwa wewe tena kavu kavu bila futa kwahyo walioandamana woote walikua ni wanachama wa chadema!!?
 
Uzi wote ni logical fallacy.
Huwezi kutuma watu waichome nchi yao wenyewe halafu ukashughulikiwa kisha ukaanza kujiliza kwa wahisani wetu.

Kuna mawili, aidha wewe na hao wanaokutuma mna nia mbaya na nchi hii, au wewe huna huo uzalendo unaojaribu kuutumia ukiwa silaha ya kisiasa.

Hao CHADEMA wanapita mle mle walimopita wanasiasa walioyaharibu mataifa mengi duniani. Wanapofanikiwa kutengeneza chuki leo hii maana yake huo ni mtaji haramu ambao wanapambana uendelee kuwa hai ili siku moja uje kuichoma moto Tanzania yote.

Unapojaaliwa utajiri wa asili kwa bahati mbaya kunakuja vita ngumu ya wenyeji wa nchi husika kuenda sambamba na uelewa kuhusiana na utajiri husika.
 
Unasoma kilichoandikwa humo ndani, tatizo letu wabongo ni kuwa negative mno yaani tunapitiliza.

Hayo maandiko hatuyasomi tunakuja kulaumu baadae vitu vilivyoelezewa kwa kina na vyenye kuhusiana na maisha yetu wakati tulichotakiwa kufanya ni kupata maarifa kutoka kwenye maandiko ya watu mbalimbali.
Nimewayasoma na nifahamu Sera na Program nyingi za serikali. Im a concerned and informed citizen.

Lakini, hatuhitaji kuwa wasomi kujua kinachoendelea nchi hii. Elimu, Maji, Miundombinu, Afya, Niambie ni wapi unaweza sema tumefanikiwa kwa hata 75% for 60 of self rule?
 
Hakuna chama kipya kinakuja madarakani pamoja na ofisi zake za serikali, majeshi, polisi, mahakama, barabara, hospitali, mahakama na majaji wake wapya. Watatumia miundombinu hiihii na rasilimali watu iliyopo, maana miundombinu hii sio mali ya chama kilichoko madarakani wala Rais, ni mali ya watanzania hata wale ambao hawajazaliwa. Kuichoma moto na kuiharibu sio sawa na kosa kubwa sana.

Hakuna mahali popote nimesikia chama cha chadema kimekerwa na kuharibiwa kwa mali/kodi za watanzania katika vurugu za Octoba 29, 2025 na siku zilizofuata siku hiyo. Hii ni kuonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wachomaji na chadema, la sivyo, walifurahishwa na uchomaji ule.

Hayati Reginald Mengi (RIP) alikuwa miongozi mwa watu wa kwanza nchini kumiliki vyombo vya habari. Kila wakati unapokaribia uchaguzi mkuu alikuwa akitumia vyombo vyake vya habari kutuonyesha watanzania ubaya wa kuvunjika kwa amani kunakoweza kuletwa na vurugu za uchaguzi na vyama vya upinzani. Nadhani alikuwa mwanaCCM lakini alifanyahivyo kwa kusukumwa na umuhimu wa amani na utulivu katika uwekezaji wake nchini. Kwenye vurugu mitaji inapotea.

Mzee Mengi alikuwa anatuonyesha vita na mauaji ya Rwanda, Burundi na Somalia kwenye kituo chake cha TV. Wapinzani walimlaumu sana kuwa anawatisha watanzania wasivichague vyama vya upinzani. Leo Mengi hayupo lakini nchi ilichomwa moto na watanzania wenzetu wamepoteza maisha wakati wa uchaguzi sawasawa na hofu na tahadhali yake.

Kuchoma au kuunga mkono kuchoma nchi/malalo yetu ni kosa la kiufundi ambalo chadema walilifanya katika harakati zao za kisiasa. Wamekirudisha chama kilometa nyingi sana nyuma. Leo hii chadema kinaogopwa na wananchi kama chama kisichowatakia mema wananchi na taifa. Mwananchi ambae amepoteza mtoto wake kwenye vurugu zile anawalaumu chadema, waliokosa matibabu wakati wa vurugu wanailaumu chadema, waliokosa usafiri wa mwendokasi kwakuwa umechomwa moto wanailaumu chadema, waliokosa ajira kwakuwa sheli na malori waliyokuwa wameajiliwa yamechomwa moto wanailaumu chadema; watoto waliokosa masomo kwa kule kufungwa kutokana na vurugu wanailamu chadema; walioshindwa kutoka nje kujitafutia riziki kwasababu ya vurugu wanailamu chadema, waliofilisika kwasababu maduka yao yaliporwa kwenye vurugu wanailaumu chadema na viongozi wao akina heche; wanaokosa huduma kwenye ofisi za serikali za mitaa na kata zilizochomwa wanailaumu chadema; chadema, chadema, chadema.

Matokeo yake ni nini, leo hii ni rahisi sana kuyazuia maandamano ya chedema kuliko wakati mwingine wowote. Wakiitisha maandamano wananchi wooote wenye akili timamu wanabaki majumbani mwao na biashara zote zinafungwa kupisha maandamano ya chadema. Barabara na mitaa inabaki tupu, na hata wanaojitafutia riziki zao kwa kutoka kila siku kama bodaboda, daladala, mama lishe na wauza mboga wanakubali kukaa ndani na njaa ili kunusuru roho zao dhidi ya chadema na polisi. Chadema Wakiendelea kufanya hivi kwa muda mrefu watanzania hawa waliozoea amani wataifuta chadema vichwani mwao na kuwalinganisha na magaidi au watia hasara au wapenda vurugu au wapenda vita.

chadema kitabakia kuwa chama cha watu na vijana wapenda vurugu/wabwia unga, wavuta bangi na wasiokuwa na chakupoteza. Hata kwenye vurugu zile ni watoto wasiokuwa na chakupoteza tu ndio waliathirika; hakukuwepo na watoto wa wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi, maprofesa wala watumishi. Wengi wao walikuwa ni watoto wa masikini kabisa waliotolewa kafara na watu wanaowaamini na kuwaheshimu sana kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiroho. Watu ambao walikuwa wanajua kuwa vijana wale kwa kuchoma mali za umma na hata zile zinazolindwa kwa bunduki lazima wangeuliwa na kujeruhiwa kwa wingi. Hesabu zao zilikuwa wangeuliwa wachache tu na wengine watafanikisha lengo lao kwakuwa walijua kuwa polisi wengi walikuwa kwenye malindo ya kulinda uchaguzi. Bahati yao mbaya ni kwamba mikoa mingi na watanzania wengi hawakujitokeza kuunga mkono vurugu zao kama walivyokuwa wamekusudia. Hii ilisababisha Vijana waleta vurugu wakaminywa wote na kunyanyua mikono, bila hivyo serikali na watanzania wote tungekuwa tunashuhudia magofu kila kona. Yaani tungerudi nyuma miaka 50 kimaendeleo.

Chadema imetumika tu kama mtu wa mwisho/loud speaker nyuma ya wapanga mipango wakubwa wenye maslahi ya kibiashara nyuma ya pazia. Vurugu tunazoziona msingi wake mkuu sio demokrasia, bali biashara haramu ambazo zilivurugwa na utawala mpya wa Rais samia. Mpango ambao ulianza kwa kumnyang'anya Mbowe chadema ili kitumike kama jukwaa lao la kufanikisha kile wanachokidai/maslahi.

Samia amevuruga biashara zao haramu nyingi sana. Kulikuwa na mipango kabambe ambayo ilikuwa inafanyika wakati wa JPM, ambayo ghafla iliingia hitilafu baada Rais JPM kufa ghafla ambayo hawakuwa na uhakika kama Samia angeruhusu waendelee nayo kama ilivyo au Samia angehamia kwa watu wengine kama Rostam, nk.

Vita hii sio ya kidemokrasia hata kidogo, ni vita ya maslahi.
Kwa huu ugumba wa vichwa vyenu , Chadema mnaweza kuifuta lakini nawahakikishieni msipoacha kuiba chaguzi, kuteka na kupoteza raia, uzi ni uleule.
 
Hayo ni maneno yako , hakuna kiongozi yoyote wa Chadema aliyesema maneno hayo. Mnatafuta kisingizio cha mauaji ya halaiki mliyofanya 29.10.2025, hii haiwezi kuwasaidia sana sana mnazidi kuwatia wananchi hasira na chuki kwa serikali yenu haramu.

Pole sana,nilijua utaweza kuachana na ukweli
 
Back
Top Bottom