Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Muundo wa uongozi wa CHADEMA unapata nguvu kutokana na aina ya watu waliokaa juu, mfumo wao una watu wenye nguvu ya kisiasa na kiuchumi mmoja Wapo Mwenyekiti na una watu wenye akili nyingi na maarifa mmoja Wapo Tundu Lisu.
Serikali ilipoaanza kupambana na Mwenye akili walidhani Mwenye fedha atasarenda nakumwacha Mwenye akili apambane peke yake. Lakini pia waliamini Mwenye fedha ataachana na siasa nakuziegemea Mali zake. Kumbe walikosea.
Mfumo mzima wakununua watu kwa ahadi ya fedha na madaraka umekwenda kuondoa solidarity ndani ya chama Cha mapinduzi na kuweka makundi ambayo waliokuwa ndani ya chama miaka yote wametupwa nje na walionunuliwa wamekabidhiwa madaraka. Hawa waliokabidhiwa madaraka leo wanajua wazi kwamba kiongozi wao aidha Mwenye fedha (Mbowe) au Mwenye akili nyingi (Lisu) wameshiriki kwa namna moja au nyingine kuwajenga, watawasaliti Hawa watu wawili kwa vipande vya fedha lakini si kwa kubadili miyoyo yao juu ya harakati za maisha.
Kwa wanaoona kesho ya CHADEMA wanaona wazi kwamba chama kinaimarika kwa sababu ya msimamo unaoendana na wanachotaka wananchi, CCM imeashindwa kurejesha imani kwa wananchi na hata baada ya Mbowe kukamatwa hakuna mabadiliko ya siasa za upinzani unayoona kwenye jamii, watu wamebaki na nafsi zilezile.
Hotuba moja ya Tundu Lisu inafuatiliwa na mamilioni ya wananchi ,lakini hotuba za viongozi wa chama Tawala zinasuswa hata na wafuasi wao wenyewe. Means hakuna ajuaye mfuasi wa CCM Ni yupi hasa linapokuja suala la nafsi moja moja.
Kwa mantiki hii napenda kuwaambia imefika wakati ambao mageuzi hayamtegemei Tena Mbowe Wala Tundu Lisuu, yanamtegemea yeyeyote anayewapeleka wananchi kule wanapotaka. Si sahihi kwa CCM kupambana na vyama vya upinzani kupitia dola maana namna wanavyopambana ndivyo wanavyopoteza watu hata wale wanaowazunguka na wenye madaraka.
NJAA IMEKUWA KALI TUMBONI LAKINI HAIMAANISHI NJAA YA UBONGO IMEPOA.