Wewe ama umeamua kujifanya hujui kinachoendelea ama unajitia wazimu, napenda kukwambia yafuatayo:
- Chadema toka 2019 walimuomba dictator kule Mwanza wakae chini wazungumze masuala yanayolikumba taifa, lakini hakujali kwa kiburi chake.
- Walikataa matokeo na matunda ya uchaguzi wa mwaka 2020 kwa sababu ulikuwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi.
- Kufuatia maridhiano yanayoendelea, Chadema imeonyesha nia ya kuliponya taifa hasa walioteswa kipindi cha dikteta uchwara. Ndicho maana leo hii imekuwa rahisi kwa viongozi wa CCM na Chadema kukaa pamoja. Na moja ya matunda ya maridhiano hayo ni kuachiwa wanachama mbalimbali wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti Mbowe, kurudi nchini viongozi wa Chadema, kufunguliwa mikutano ya hadhara iliyozuwiwa kihuni na pia kuchukua ruzuku ambayo Chadema iliikataa mpaka mazingira ya kisiasa yatakapowekwa vizuri, ambayo sasa tunaona.
NB, Kinachofuata ni kwamba wale waliopatikana na COVID-19 wanaondolewa bungeni kwa sababu walivunja taratibu za kichama. Hivyo, Chadema itateua wabunge wengine tofauti. Pia, katiba mpya inakuja, mashauriano yanaendelea, jiandae kutafuta kazi halali. Buku saba haitakuwepo tena, maana kila mtu atakula kwa jasho lake. Ni hayo tu.