Ze Bulldozer
JF-Expert Member
- Jun 12, 2020
- 1,070
- 568
===
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wake Salum Mwalim Juma wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kwa Vitendo Uhuru wa kutoa maoni na kukusanyika,
Ndugu zangu wa Chadema huu Sasa ndio Uzalendo wa kweli kwa Rais wenu na nchi yenu, Sasa kwa pamoja tujenge nchi yetu kwa amani na Upendo huku tukiweka pembeni tofauti zetu za kisiasa
Tundu Lissu na wenzako rudini kwenu Tanzania, Mungu anajua na Dunia inajua awamu hii ya Rais Samia Suluhu Hassan ni salama kuliko Tanzania ya wakati wowote katika historia ya nchi hii,