Ndugu
Lucas mwashambwa;
1. Mimi nadhani badala ya kupiga propaganda za kijinga na kipumbavu kama hizi za kujadili petty issues, ungeonesha kuwa una akili na ufahamu kwa kuichambua na kuitetea kwa kuonesha uzuri wa miswaada hii mitatu kuhusu mambo ya uchaguzi iliyowasilishwa na serikali ya chama chako ili tukuelewe na kukuunga mkono wewe na chama chako CCM na kisha tuwapuuze CHADEMA..
Kwa mfano;
👉Unaweza kutueleza chaguzi zetu za kisiasa (serikali za mitaa, udiwani, ubunge na Rais) huwa zinakabiliwa na matatizo gani kiasi cha kulalamikiwa na wadau na wananchi kwa ujumla hata serikali kuja na miswaada hii ya sheria hizi tatu ikifikiri kuwa itatatua matatizo hayo?
👉Na hakuna ubaya na wewe kutoa maoni yako iwapo sheria hizi zinajibu matatizo hayo au la..
👉 Na kumbuka kuwa CHADEMA, wao wametoa maoni yao. Maoni ni maoni tu.
👉Hata hivyo, miongoni mwa taasisi zilizotoa maoni bora na iwapo yatachukuliwa na kufanyia kazi, uwezekano wa kupata sheria bora na nzuri za uchaguzi na Tume ya uchaguzi zitakazojibu matatizo ya chaguzi zetu ni CHADEMA, Baraza la Maaskofu Katoliki - TEC, KKKT na TLS...
👉Hebu tuambie sasa, Kwa akili na mtazamo wako, unadhani miswaada hii ya sheria hizi tatu ikiachwa ipite hivhivi kama CCM wanavyopendekeza, itatua changamoto za kiuchaguzi ambazo zimekuwa zikilalamikiwa miaka mingi?
##Kama una akili na ufahamu, hebu shiriki mjadala huu Kwa kujibu swali hilo☝️☝️