Ndugu zangu Watanzania,
CHADEMA ni watu wenye uroho na uchu mkubwa sana wa madaraka.ndio maana kwa kila jambo linalojitokeza mbele yao wao huangalia ni vipi watapata na kufaidika zaidi na kupata madaraka kiwepesi. kuliko kuangalia ni vipi wananchi watapata faida na kunufaika.ndio sababu huwezi ukaona CHADEMA wakipigania hoja zinazogusa maisha ya watu na ustawi wao wala kuwa na uchungu na maisha ya watanzania.
Hata katika masuala ya kisheria au mabadiliko ya sera au sheria ya aina yoyote ile wao hutafuta upenyo wa kupita utakao warahisishia kazi ya kupata madaraka.hii ndio sababu ya mara nyingi kutaka hoja ya kutugawa watanzania kwa kusema kuwa kuwe na sera ya majimbo,hii ndio sababu ya kutaka mfumo wa serikali tatu.
Na sasa wamekuja na kioja cha mwaka na karne kwa kusema kuwa eti kwa kila jimbo kuwe na wabunge wawili yaani mwanamke na mwanaume na kila mmoja apigiwe kura na jinsia yake au kundi lake.yaani wanawake wapige kura kwa mgombea mwanamke na wanaume kwa mgombea wa kiume.
Hii yote ni katika dhana ileile na mawazo yake yale na fikira zilezile za kusaka madaraka na uchu wa madaraka na kutafuta upenyo wa kuneemesha matumbo yao na familia zao.bila kujali maumivu watakayo yapata Watanzania katika kubeba gharama za kuwalipa hao wabunge.
Tuwakatae CHADEMA na mambo yake yote .tuwapinge kwa nguvu zetu zote.tusiwape upenyo wa kutimiza adhima zao za kutugawa watanzania na kutubebesha mzigo wa gharama zisizo na msingi.
Siku zote na wakati wote hawajawahi kuwa na dhamira njema kwa watanzania zaidi ya kupigania maslahi na matumbo yao tu.wao hawana habari na maisha ya watanzania wala shida za watu.wao huangalia ni vipi watamkamua pesa zote mtanzania na kumuacha maskini wa kutupwa.huku wao wakiogelea katika utajiri wa kila kitu na kucheua tu dharau kwa watanzania.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.