Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 761
- 6,985
Kelele zimekuwa nyingi Sana na upinzani hasa Chadema wanaonekana kumiliki agenda nyingi kila Kona , wanaonekana Wana wafuasi wengi sana mitandaoni Jambo linalokwamisha ujumbe wa serikali na CCM kusambaa ipasavyo.
Wakosoaji wamekuwa wengi mitandaoni na nje ya mitandao hii inaweza kuwa imechangiwa na sababu zifuatazo
1. Awamu ya Tano ilikamata,ikafunga,na kunyanyasa watu wengi sana wakiwemo Wana CCM kindakindaki Jambo lililowavunja Moyo na kuwafanya wabaki wanaccm majukwaani na mbele za WATU ila wageuke wakosoaji sirini
2. Hakuna anayejua Nani mwana CCM ,yapo mashaka kwamba wapinzani ni wengi kwenye mfumo wa chama kuliko nje ya mfumo
3. Chama kimegawanyika kwenye sukuma Gan na Wanaojihita wamiliki wa CCM.
4. Waliotesa watu wakiwemo akina Makonda bado nimashujaa ndani ya CCM. Ikumbukwe walioteswa ni pamoja na viongozi waliopo ofisini Leo akiwemo Chongolo
5. Watu wengi wenye chama na wasio na chama wanataka maridhiano. Hakuna anayekubaliana na Mama kwenye mfumo wakuweka wapinzani wake mahabusu na kitendo cha kuendelea kuwa na wafungwa wa kisiasa kinawafanya Wana ccm waamini ipo siku na wao watakamatwa kwani hata JPM alianza na wapinzani mwisho akaelekea Kwa Wana CCM na wafanyabiashara alioona wanatishia uwepo wake madarakani.
6. Wapo watu wanajiuliza, Kwanini Zanzibar pametulia na hakuna wafungwa Wala mahabusu wa kisiasa? Kwanini Kati ya mahabusu hakuna Mzanzibari? Kwanini Makamu wa Rais hata alipotoka adharani akatishia kujiuzulu hakukaripiwa badala yake uchaguzi ulirudiwa na ACT wakapewa ushindi?
7. Baadhi wanauliza, JPM aliwekeza Chato, je Sasa hivi Hali ilivyotulia Zanzibar haina maana kwamba Sasa ni zamu ya Zanzibar?
8. Lakini viongozi wengine waliokuwa vocal na watetezi kindakindaki wa JPM akina Hapi, Mnyeti, KABUDI nk Kwanini awamu hii wamesusa wakati Bado Wana madaraka yaleyale?
Haya na mengine yanafikirisha na kufanya kutafakari nakuona upo umuhimu wakuanza maridhiano kabla Tundu Lisu ajaingia nchini na kutumia agenda ya wafungwa wa kisiasa kuimarisha Chadema. Lakini Mama amerealize kwamba washauri wake wanatamani afeli na walitamani afeli ila Sasa wanaona anaenda vyema wanajitokeza kumpinga adharani kuashiria kwamba hata Yale waliuomshauri ikiwemo kuendelea na wafungwa wa kisiasa bara walitaka afeli.
Jambo lakujiuliza, endapo atakubali kukaa na Chadema pekee wajadiliane na akawaachia bila madharti wafungwa wa kisiasa. Chadema itwaambia Nini Watanzania kuhusu msigano walioanzisha na Act wakiwatuhumu ni masnitch?Je agenda ya katiba Bado itakuwa na nguvu?