CHADEMA wanachukia maendeleo ya Tanzania?

CHADEMA wanachukia maendeleo ya Tanzania?

Mara kadhaa imesemwa na CCM kwamba CHADEMA hupinga kila kitu/jambo linalofanywa na serikali inayoongozwa na CCM.

Ina maana CHADEMA hawataki nchi yetu ipate maendeleo? Na ni kweli pia kwamba huwa wanapinga kila kitu kinachofanywa na serikali inayoongozwa na CCM?

..kama nchi imekwama kwa miaka 60 tangu uhuru basi Ccm ndio wanaochukia maendeleo.
 
Mara kadhaa imesemwa na CCM kwamba CHADEMA hupinga kila kitu/jambo linalofanywa na serikali inayoongozwa na CCM.

Ina maana CHADEMA hawataki nchi yetu ipate maendeleo? Na ni kweli pia kwamba huwa wanapinga kila kitu kinachofanywa na serikali inayoongozwa na CCM?

Tatizo halijaanzia kwa chadema. Tatizo liko kutoka kwa wale waliotuletea vyama vingi. Wao walifundisha kwamba. Kuna aina mbili ya vyama vya siasa; mosi ni chama tawala; pili cha/vyama vya upinzani. Basi wakahubiriwa hivyo miaka yoote, kuwa byie ambao hamko madarakani ni wapinzani. Kazi yenu ni kuja na HOJA za KUPINGA TU, badala ya kuja na HOJA MBADALA. Sasa matokeo yake ni kupingaa, pingaaa, pingaaa weeee. Pingaaa mpaka basi. Kama kawaida ya Afrika, kwamba inameza kama dodoki chochote kinachotoka magharibi. Hata vyama vingi ikawa hivyo hivyo. Tangu Washington consensus waseme nyie msio madarakani ni wapinzani, basi kazi ni moja tu ni kupinga, pingaaa mpaka mwisho. Na kwa nini inakuwa hivyo, kwa sababu kupinga ni rahisi kuliko kuja na hoja mbadala. Kuleta hoja mbadala inahitaji akili, maana unapaswa kulielewa jambo, halafu ndiyo unakuja na mbadala wake.
Ndiyo maana wepesi sana wa kupinga.

Kwa hiyo ndugu yangu, hili litaendelea hadi pale tutakapo amua kuja mabadiriko ya kutoka vyama visivyo ongoza dora, kutoka VYAMA VYA UPINZANI kweda VYAMA MBADALA.

Mwisho, KUPINGA KITU KUNATUMIA HISIA, LAKINI KULETA KITU MBADALA KUNATUMIA AKILI.
 
Mwisho, KUPINGA KITU KUNATUMIA HISIA, LAKINI KULETA KITU MBADALA KUNATUMIA AKILI.
Hivi tofauti kati ya kupinga na kutofautiana ni nini? Na nani anayeamua kama huku ni kuleta kitu mbadala ama ni kupinga?
 
Chadema wanapinga kila kitu kinachofanywa na ccm kasoro kulambishwa asali tuu.
Vipi unayepinga kuondosha kwenye jungu la hiyo asali,hata kuona Bora tukose wote🤔.Sasa sibora anayelamba na kuwaachia wengine kuliko anayevunja jungu ilmradi tukose wote🤔
 
Hivi tofauti kati ya kupinga na kutofautiana ni nini? Na nani anayeamua kama huku ni kuleta kitu mbadala ama ni kupinga?

Kutofautiana ni kupinga katika lugha ya staha.

Kupinga hakuhusishi kutumia vyema uwezo wa kufikiri, lkn kuleta kitu mbadala lazima uchambue kasoro na pia kuleta sulihisho au mbadala wake.

Kupinga tunasema ni hisia kwa sababu pengine unapinga kitu kwa kuwa hukipendi kibinafsi au hata hukielewi. Pinga pinga si afya na mara nyingi kufanywa na wasio na hekima.
 
Nani anayeweka kigezo cha jinsi ya kutoa hayo mawazo mbadala!!?? Maana kama anayeweka kigezo ni yule anayekusudiwa kukosolewa basi sio sawa. Maana kama CCM ndiyo wanaotakiwa kuweka kigezo ni vipi wakosolewe na CHADEMA haitakuwa sawa.

Inavoonekana watu wengi hata hayo mawazo mbadala toka CHADEMA hawayajui hata yakoje.
 
Hayo ni mambo madogo madogo sana, ambayo yanahusisha kuweka MIONGOZO iliyojajiliwa na kuandaliwa na wadau.
 
Back
Top Bottom