Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Mara tu baada ya kuvuliwa uanachama, Halima Mdee na wenzake walitinga mahakamani na kufungua kesi na mmoja wa walalamikiwa ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Chadema wanapinga NEC kushitakiwa kwa sababu ni kinyume na katiba. Ila NEC ndio wangetanzua mzozo wa mamlaka iliyowateua akina Halima Mdee na wenzake kwa kutoa ushahidi wa barua iliyotumika.
CHADEMA wanasema hawakuandika barua wakati NEC inasema ilipokea barua kutoka CHADEMA.
Kama mashitaka yamekosewa kuijumuisha NEC, na NEC wangefika mahakamani na kutoa ushahidi uliojitosheleza, Chadema wangepoteza nini? Au Chadema haitaki NEC ifike mahakamani na kutoa ushahidi ambao waweza kuwa mwiba mkali kwa Chadema?
Hivi ruzuku ya chama ya wabunge wote wa Chadema inalipwa?
Kwa kifupi inaonekana kuwa hii ni sanaa!