CHADEMA wanatoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari, leo Julai 10, 2026

CHADEMA wanatoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari, leo Julai 10, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Screenshot 2026-07-10 104801.jpg


View: https://www.youtube.com/watch?v=m-kVFwmIRKE
​

"Ile ile kauli ya Rais ambaye sisi hatutambui uchaguzi wake ya kusema kwamba wanaharakati wanafanya ugaidi. Ni kauli hatari sana ikiachwa ilivyo na watetezi wa haki kote nchini. Na mimi nasema haya kwa sababu kutokana na taarifa za maandamano ya tarehe 7 mwezi wa 7 yaliyotangazwa huko mitandao. Inavyozungumzwa hivi sasa, kuna viongozi wa CHADEMA na wanachama wako vituo vya polisi bado. Na wengine wamepigwa na kuumizwa.

Geita kule kuna dada anayeitwa Nema. Huko kule Tanga kuna Nasra, kuna Rukia na wengine. Kule Mbeya kule kuna vijana wa CHASO, Dar es Salaam hapa kuna watu wamepigwa, wameumizwa. Katika kupigwa kwao walikuwa wanalazimishwa wengine wao kuandika maelezo kwamba walipanga vitendo vya kigaidi, alafu wanalazimishwa kwa vipigo kutaja majina ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

Sasa, kitendo cha matukio hayo kutokea siku chache kabla alafu Rais kutamka kuhusu wanaharakati na ugaidi, inatengeneza connection kwamba inawezekana kabisa kulikuwa na order ndani ya serikali na ndani ya mfumo wa vyombo vya ulinzi na usalama kubambika kesi za ugaidi kwa viongozi wa CHADEMA kwa malengo ambayo yana yanaleta maswali.

Soma: Mnyika: Kauli ya Rais kuhusisha wanaharakati na ugaidi wakati viongozi CHADEMA wanakamatwa ni hatari

Sasa hii behavior ya kuingiza neno ugaidi kubwa sana katika masuala ya kiraia ya watu, imekuwa trend ya hii serikali. Mwaka 2021 baada ya Mwenyezi Mungu kumtoa Magufuli, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema, alipoingia Samia, CHADEMA ilipoanza tu ziara ya Katiba Mpya kwa makongamano ya ndani, Rais akasema kuna chokochoko za katiba, Mwenyekiti Mbowe akiwa Mwanza akakamatwa akapewa kesi ya ugaidi kwa sababu ya Katiba Mpya.

Sasa leo wakati nchi inazungumza Katiba Mpya, free Tundu Lissu, Rais anarudia kile kile, kipateni ile ile. Ni ishara ya kwamba hakuna maridhiano, kuna tangazo la vita. Vita dhidi ya wanaharakati na by extension, vita dhidi ya CHADEMA na viongozi wa CHADEMA."
 
Kasoro dakika 7 sasa..nipo JF hapa nimeji koki....
 
Back
Top Bottom