13 November 2024 Arusha, Tanzania
CHADEMA WANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MUDA HUU, tathimini kuelekea uchaguzi 2024
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Mhe. Amani Golugwa Leo tarehe 13 November 2024, akiwa na Godbless Lema ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini pamoja na kamanda Benson Kigaila Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA bara watoa takwimu za ndani juu ya CHADEMA ilivyo jizatiti kwa kusimamisha wagombea nafasi zote kwa asilimia 100 za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji ..
Ingawa wasimamizi wasaidizi wamewaeunga wagombea wengi wa CHADEMA ila taratibu za kukata rufaa dhidi ya mapingamizi zinaendelea na kuwa CHADEMA haitajitoa ktk uchaguzi wa 2024 ...
Takwimu nzito alizozisoma Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Mhe. Amani Golugwa, ni kujibu propaganda za CCM na vyama rafiki vya chama dola tawala wanazosambaza kuwa CHADEMA haikuwa imejipanga. Propaganda hizo zimekuwa zikirudiwa na katibu uenezi, itikadi na mafunzo wa Halmashauri kuu ya CCM ndugu CPA Amos Makala hivi karibuni ..
kamanda Benson Kigaila Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA bara amepiga kama kwa muda mrefu kanda ya kaskazini kwa kazi za kichama kuangalia tangu mwanzo zoezi la kuandikisha wakazi katika daftari la mkaazi (mtaani), uchukuaji fomu za kugombea uongozi serikali za mitaa, uteuzi wa wagombea uliofanywa na TAMISEMI, kubandika majina ya wagombea hadi kuenguliwa wagombea.
Na sasa kumulika usikilizaji wa rufani za wagombea wa CHADEMA walioenguliwa pia kuona kauli ya rais Samia Suluhu Hassan kupitia Katibu mkuu wa CCM Dr. Emmanuel Nchimbi kuhusu 'makosa madogo katika fomu' zinatekelezwaje kimatendo kuwarudisha wagombea katika kinyanganyiro cha uchaguzi wa TAMISEMI, kutayarisha ripoti itakayopelekwa Kamati Kuu ya CHADEMA kuhusu hali halisi ilivyo...
CHADEMA warejea kauli ya katibu mkuu wa CCM balozi Dr. Emmanuel Nchimbi hapa chini :
12 November 2024
CCM: TAMISEMI IPUUZE MAKOSA MADOGO MADOGO, KUKUZA DEMOKRASIA
Imewekwa tar.: November 12th, 2024
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kuwaelekeza Wasimamizi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kupuuza makosa madogo madogo yaliyotokea, ili kuruhusu wagombea wengi kushiriki uchaguzi huo.
Akizungumza na wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo vya habari nchini, Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa mfano wa makosa hayo yanayostahili kupuuzwa ni pamoja na wagombea kukosea herufi.
Kupitia mkutano huo uliofanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 12, 2024, Balozi Nchimbi amesema ni vyema TAMISEMI ikaangalia uwezekano wa kuwarudisha wagombea wote walioenguliwa kutokana na makosa hayo madogo madogo ili kuhamasisha ukuaji wa demokrasia kwenye uchaguzi huo.
Aidha, kuhusu sehemu kubwa ya malalamiko mengi ya kuenguliwa kuonekana ni ya wagombea wa vyama vya upinzani, Balozi Nchimbi amewatoa shaka Watanzania kuwa, si kweli kwamba wagombea walioenguliwa ni wale wa vyama vya upinzani pekee, bali pia hata wagombea wa CCM wapo waliowekewa mapingamizi ya kugombea.
“Waziri wa TAMISEMI tunajua anafuata sheria, lakini ni muhimu kutambua demokrasia yetu hii bado ni changa hivyo tunahitaji muda wa kuendelea kujiífunza tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI katika nyakati za mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogo madogo ili watu wengi wapate nafasi ya kugombea", alisema Dkt. Nchimbi.
PIA SOMA
- LGE2024 - Lema: CCM wanakaa vikao na ACT Wazalendo ili kukifanya kuwa Chama Kikuu cha Upinzani nchini na kuondoa hadhi yetu
Source : OR TAMISEMI
