Chadema waongea na waandishi habari juu ya shambulio la Mbowe na mtazamo wa chama

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, amesema kutokana na hali aliyonayo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, wamefikia uamuzi wa kufanya utaratibu wa kumsafirisha kuja jijini Dar es salaam kwa ajili uchunguzi zaidi na matibabu.

Katika tukio hili napo polisi wamejitokeza wakijaribu kueleza kama vile ni tukio la kawaida na wakitaka lisihusishwe na siasa" -John Mnyika. #HATUCHUJI #KwanzaHabari.

"Taarifa ya Kamanda wa Polisi imetoa viashiria kwamba, kama ilivyokua kwa tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, ambapo polisi walijitokeza harakaharaka na kutoa kauli ambazo hazionyeshi uhalisia wa tukio.>>>

Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, amelitaka jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa haraka tukio la kuvamiwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ili hatua za haraka

"Milango hii ya uchunguzi waifungue kwa upana wake, kwa sababu siku chache kabla ya mwenyekiti kushambuliwa, kulisambaa video ikimnukuu mtu aliyejiita mchungaji wa kitaifa, kwa jina la Mashimo, akisema kwamba kuna tukio mbele litatokea la kiongozi wa upinzani kushambuliwa>>>

>>na kati ya majina aliyoyataja ametaja jina la Mwenyekiti Freeman Mbowe"- John Mnyika.#HATUCHUJI #KwanzaHabari
"Mwenyekiti Freeman Mbowe hakuwa peke yake wakati tukio hili linatokea, nisingependa kuingia kiundani alikuwa na nani na aliyekuwa naye ameona nini. >>>

Tutakuja kueleza taarifa za ziada na sisi tunaendelea na ufuatiliaji kutokana na taarifa tulizozikusanya"John Mnyika.

"Waliomshambulia Mwenyekiti Mbowe kuna maneno walikuwa wanayatamka, walikuwa wanasema kwamba hatudhamili kukuua, lakni pamoja na kutamka maneno hayo walikuwa na silaha ambazo hawakuzitumia, walimshambulia maeneo mbalimbali ya mwili"-John Mnyika. #

"Katika hatua ya sasa, eneo lililoathirika zaidi ni mguu wake wa kulia lakini kwa sababu ameshambuliwa maeneo mbalimbali ya mwili bado uchunguzi unaendelea kujua kiwango cha madhara ambayo ameyapata"-John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema.

"Kwa kuwa tukio ndo limetokea, sisi kama chama tutaendelea kuangalia iwapo jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vitabadilika au laa, kwa namna ambavyo wanafanya uchunguzi.>>>

Tutawaita kuweza kutoa taarifa ya ziada kuhusiana na nini ambacho tunasema juu ya uhitaji wa uchunguzi, ili wahusika waweze kukamatwa"John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema. #

"Wanahabari ni vizuri mkaiuliza serikali, baada ya kushambuliwa Tundu Lissu, miezi michache baadaye serikali hii ya CCM, ikapeleka bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa na ule muswada ukapiga marukufuku vyama siasa kuwa na mifumo ya kuwalinda viongozi wake.

Magufuli atueleze je, waliamua kutunga sheria ya kuzuia vyama kuwalinda viongozi wake ili kutengeneza mazingira viongozi wa vyama kushambuliwa?"-John Mnyika.#

Wana-chadema na viongozi wa Chadema, hatuwezi kutishwa wala kupata hofu kwa sababu mmoja wetu ameshambuliwa,>>>>

>>>tutaendelea kusimama tukijilinda na kujipanga kuhakikisha kwamba tunaiondoa madarakani serikali hii ambayo inashindwa kuhakikisha hata usalama wa viongozi katika makao makuu ya nchi" John Mnyika.#HATUCHUJI #KwanzaHabari
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, amesema kutokana na hali aliyonayo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, wamefikia uamuzi wa kufanya utaratibu wa kumsafirisha kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya matibabu zaidi. https://t.co/M4Vg4e3iGp
Apelekwe Ubelgiji kama anaona wivu Lissu kuishi ubeberuni!
 
Madhara ya kutoka nje ya ndoa kuchepuka huku ukirubuni wabunge wa viti malum na wake za watu ni makubwa.

Pole sana kamanda.
Inasemekana alikuwa na mbunge wa viti maalumu chadema na huyo mbunge ndio alietoa taarifa polisi
 
Seala la kuzuia vyama kuwapa walinzi viongozi wao limenishangaza sana, nilikua sina hiyo taarifa, na inatia ukakasi, kwa nini wazuie ulinzi kutoka kwenye chama?
Njama ni nini?
 
Hii ndio ajenda kubwa ya hii serikali, hayo mengine sijui Stieglar Godge, SGR na Ndege ni usanii tu wa kuhalalisha ufujaji wa fedha za wananchi.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, amesema kutokana na hali aliyonayo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, wamefikia uamuzi wa kufanya utaratibu wa kumsafirisha kuja jijini Dar es salaam kwa ajili uchunguzi zaidi na matibabu.

Katika tukio hili napo polisi wamejitokeza wakijaribu kueleza kama vile ni tukio la kawaida na wakitaka lisihusishwe na siasa" -John Mnyika. #HATUCHUJI #KwanzaHabari.

"Taarifa ya Kamanda wa Polisi imetoa viashiria kwamba, kama ilivyokua kwa tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, ambapo polisi walijitokeza harakaharaka na kutoa kauli ambazo hazionyeshi uhalisia wa tukio.>>>

Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, amelitaka jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa haraka tukio la kuvamiwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ili hatua za haraka

"Milango hii ya uchunguzi waifungue kwa upana wake, kwa sababu siku chache kabla ya mwenyekiti kushambuliwa, kulisambaa video ikimnukuu mtu aliyejiita mchungaji wa kitaifa, kwa jina la Mashimo, akisema kwamba kuna tukio mbele litatokea la kiongozi wa upinzani kushambuliwa>>>

>>na kati ya majina aliyoyataja ametaja jina la Mwenyekiti Freeman Mbowe"- John Mnyika.#HATUCHUJI #KwanzaHabari
"Mwenyekiti Freeman Mbowe hakuwa peke yake wakati tukio hili linatokea, nisingependa kuingia kiundani alikuwa na nani na aliyekuwa naye ameona nini. >>>

Tutakuja kueleza taarifa za ziada na sisi tunaendelea na ufuatiliaji kutokana na taarifa tulizozikusanya"John Mnyika.

"Waliomshambulia Mwenyekiti Mbowe kuna maneno walikuwa wanayatamka, walikuwa wanasema kwamba hatudhamili kukuua, lakni pamoja na kutamka maneno hayo walikuwa na silaha ambazo hawakuzitumia, walimshambulia maeneo mbalimbali ya mwili"-John Mnyika. #

"Katika hatua ya sasa, eneo lililoathirika zaidi ni mguu wake wa kulia lakini kwa sababu ameshambuliwa maeneo mbalimbali ya mwili bado uchunguzi unaendelea kujua kiwango cha madhara ambayo ameyapata"-John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema.

"Kwa kuwa tukio ndo limetokea, sisi kama chama tutaendelea kuangalia iwapo jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vitabadilika au laa, kwa namna ambavyo wanafanya uchunguzi.>>>

Tutawaita kuweza kutoa taarifa ya ziada kuhusiana na nini ambacho tunasema juu ya uhitaji wa uchunguzi, ili wahusika waweze kukamatwa"John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema. #

"Wanahabari ni vizuri mkaiuliza serikali, baada ya kushambuliwa Tundu Lissu, miezi michache baadaye serikali hii ya CCM, ikapeleka bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa na ule muswada ukapiga marukufuku vyama siasa kuwa na mifumo ya kuwalinda viongozi wake.

Magufuli atueleze je, waliamua kutunga sheria ya kuzuia vyama kuwalinda viongozi wake ili kutengeneza mazingira viongozi wa vyama kushambuliwa?"-John Mnyika.#

Wana-chadema na viongozi wa Chadema, hatuwezi kutishwa wala kupata hofu kwa sababu mmoja wetu ameshambuliwa,>>>>

>>>tutaendelea kusimama tukijilinda na kujipanga kuhakikisha kwamba tunaiondoa madarakani serikali hii ambayo inashindwa kuhakikisha hata usalama wa viongozi katika makao makuu ya nchi" John Mnyika.#HATUCHUJI #KwanzaHabari
Wakati anashambuliwa ilikuwa saa ngapi? Alikuwa anatoka wapi? Dereva wake alikuwa wapi wakati huo? Mlinzi wake alikuwa wapi wakati huo? Joyce Mukya alikuwa wapi wakati huo? Nimeanza uchunguzi
 
Mkuu umejaribu kulibeba hili jambo mabegani mwako ukajua uzito wake.
Madhara ya kutoka nje ya ndoa kuchepuka huku ukirubuni wabunge wa viti malum na wake za watu ni makubwa.

Pole sana kamanda.
Elitwege,huyu jamaa huwa anachukua mademu tu hachukui mashoga,hivyo tafuta basha mwingine,hana mpango na wewe.
 
Mbowe bae ana maisha yake binafsi mbali na kuwa mwanasiasa, maana ni binadamu. Kuwa mwanasiasa haikuzuii kufanya ratiba zako za maisha za kila siku ilimradi muda wa kazi umeisha, hata kama alikua natoka baa bado hakuna alie juu ya sheria kusema amshambulie Mbowe

Na akimaliza wapinzani, hata sisi wanaccm tutakua tunashambuliwa, hili sio jambo la kushangilia hata kidogo. Usalama wa raia ni ajenda kuu na ya muhimu kwenye taifa bila kujali mahala ulipo, itikadi ya chama au hali yako ya kiuchumi

Back
Top Bottom