CHADEMA watangaza kutoshiriki majadiliano ya wadau wa vyama vya siasa na polisi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitashiriki vikao vya majadiliano ya wadau wa vyama vya siasa, vilivyoitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, hadi mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, atakapoachwa huru bila masharti yoyote.

Sharti hilo limetajwa leo Jumatatu, tarehe 11 Oktoba 2021 na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, akitoa maazimio ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho, kilichofanyika jana Jumapili, kwa njia za kidigitali.

“Sisi kama Chadema hatuwezi kwenda kwenye vikao vya msajili, mpaka mwenyekiti wetu aachiwe bila masharti yoyote. Sababu Watanzania, Serikali na dunia inajua kwamba Mbowe sio gaidi amebambikiziwa kesi kwa lengo la kumtesa,” amesema Kigaila.

Unknown-24.jpeg

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara
Kigaila amesema, Chadema hakiwezi kushiriki kikao hicho wakati mwenyekiti wake yuko ndani.

“Hatuwezi kwenda kwenye kikao kujadiliana chochote wakati kiongozi wetu yuko ndani, tunataka Serikali ifute mashtaka ya kubumba waliyomtengenezea mwenyekiti wetu atoke, aachwe huru ili kama kuna vikao vya kwenda twende naye,” amesema Kigaila.

Msimamo huo umetolewa katika kipindi ambacho Jaji Mutungi ameitisha kikao cha wadau wa vyama vya siasa, ikiwemo Inspekta wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, ili kutafuta suluhu ya changamoto zinazokabili tasnia hiyo.

Kikao cha wadau wa vyama vya siasa nchini, kinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma, tarehe 21 Oktoba 2021.

MWANAHALISI
 
Benson Kigaila na wenzake wamepoteza mwelekeo kabisaa!!!
Chama kinaelekea shimoni
 
Binafsi nampongeza sana IGP Sirro kwa kukubali ombi la Msajili wa vyama vya siasa la kutaka kumkutanisha na vyama ili awape semina namna jeshi hilo linavyotimiza wajibu wake.

Ila nawashangaa Chadema walivyokusudia kuipoteza fursa hiyo.

Kimsingi anayepaswa kubembelezwa kukutana na mwenzake ni IGP siyo Chadema.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nawashauri wakatanyie hicho kikao jela alipo Mbowe ili naye apate nafasi ya kuhudhuria maana bado ni mwenyekiti wa CDM.
 
“Hatuwezi kwenda kwenye kikao kujadiliana chochote wakati kiongozi wetu yuko ndani, tunataka Serikali ifute mashtaka ya kubumba waliyomtengenezea mwenyekiti wetu atoke, aachwe huru ili kama kuna vikao vya kwenda twende naye,” amesema Kigaila.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitashiriki vikao vya majadiliano ya wadau wa vyama vya siasa, vilivyoitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, hadi mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, atakapoachwa huru bila masharti yoyote.

MWANAHALISI
AMEN,AMEN.
 
Binafsi nampongeza sana IGP Sirro kwa kukubali ombi la Msajili wa vyama vya siasa la kutaka kumkutanisha na vyama ili awape semina namna jeshi hilo linavyotimiza wajibu wake.

Ila nawashangaa Chadema walivyokusudia kuipoteza fursa hiyo.

Kimsingi anayepaswa kubembelezwa kukutana na mwenzake ni IGP siyo Chadema.

Maendeleo hayana vyama!
IGP atakiwa kufuata katiba/sheria za nchi na SIO yeye kuamua kujitungia za kwake. Labda uende wewe ndio ukafundishwe kubumba na kubambika kesi.
 
Mwenyekiti aachiwe tu unless kuna ushahidi pasipo shaka wa madai. Naamini kesi itafika mwisho.
 
Eti Benson Kigaila ana sema hatuwezi kuhudhuria kikao cha Msajili hadi zuio la siasa kwanza liondolewe na pili eti Mbowe aachiwe mara moja.
kwa hoja hizo dhaifu ndipo nimeona kweli Viongozi wa Chadema wamepoteza mwelekeo kabisaa.
Hoja ya Pili ya kushinikiza Mbowe aachiwe huru ni kinyume kabisa na utawala wa sheria lkn pia kitendo au kauli hiyo ya viongozi wa Chadema inaingilia uhuru wa Mahakama kwa kuishinikiza Mahakama ifanye maamuzi kinyume na utaratibu wa kisheria.
Pili nendeni mkaonane na msajili kisha muwasilishe hoja ya kwa nn zuio la kisiasa? ni ujinga kulalamika nje ya kikao, nendeni mezani kwa Msajili kwani mnaogopa nini?! nendeni mkawasilishe hoja zenu.
Kesi ya Mbowe lazima iendelee, ndio maana yuko mahakamani, Mahakama ndiye muamuzi wa mwisho.
hoja ya Bensoni Kigaila ni ujinga eti Chama kisiendelee na shughuli zake za kawaida kwa sababu eti Mbowe hayupo!!!
 
Wewe hapo ndo akili hazimo!
 
Back
Top Bottom