Ni muhimu uelewe kilichoelezwa hapo kabla hujapindisha yaliyosemwa.
Ni muda kitambo sasa kwamba kila mtu alijua Katiba mpyaisingeweza kuwepo kabla ya 2024; na hata kama ingewezekana, Bunge lililopo sasa hivi siyo chombo sahihi cha kuanzisha mchakato huo. CHADEMA hili wameliona dhahri na kulitambua.
Pili, CHADEMA kususia uchaguzi katika hali hiii inayowapa matumaini makubwa ya ushindi mkubwa, watakuwa akili zao kichwani hazifanyi kazi sawasawa.
Wanachotakiwa CHADEMA kutamka na kutangaza waziwazi ni kwamba hawatavumilia uchafuzi wa uchaguzi huo kwa aina yoyote ile.
Hapa ndipo wanapotakiwa kujipanga vizuri tokea sasa, ili kukabiliana na matukio yoyote yatakayofanywa na CCM kuvuruga uchaguzi.
Lakini swala la Kushiriki au Kutoshiriki uchaguzi, hilo halipo tena. Ni lazima washiriki kwa nguvu zote walizonazo.
Chadema wanafeli kwenye Suala la Matumizi ya fedha na namna ya kuhamasisha upatikanaji Wa fedha Kwa ajili ya watu Wa Chini yaani wale viongozi Wa matawi ya Chini au mitaa.
Bila fedha hakuna ushindi popote Kwa Karne hii. Hata Vita bila fedha hakuna ushindi. Mbele ya fedha Hata nchi imepigwa Bei.
Pesa ni Kila Kitu. Hata Uzalendo Kwa Sasa unahitaji fedha.
CCM walionufaika sana na kifo cha Ndesamburo mana alikua ndiye nguzo kubwa ya Chadema ukanda Wa Kaskazini. Alikua anauwezo Wa kugharamikia shughuli Zote za chama na kuzuia wasaliti kununuliwa na CCM.
Sasa cha KUFANYA ni Chadema kuwakubali Wazalendo wote popote walipo.
Pili kufanya uhakiki Wa Wanachama wao NDANI na nje ya nchi. Kuwajua Kwa majina na Kwa idadi Yao. Kuwapanga Wanachama Kwa makundi na Kwa Uwezo wao .
Baada ya kuwajua Wanachama Wa Chadema waliopo tayari Kupinga ukiukwaji Wa Sheria za uchaguzi Sasa waanze kuhamasisha michango KUANZIA wenye uwezo Wa kuchangia elfu moja mpaka million Kumi .
Kama Chadema itaweka watu waaminifu kukusanya michango bila tamaa kama zile za CCM basi Kwa Miezi Kumi na moja kufikia uchaguzi wa Serikali za mitaa watakua wamekusanya zaidí ya bil.20.
Pesa hizo zisikae makao makuu mana ni za Wananchi . Zitumike kuwagharamikia wagombea wote Wa Serikali za mitaa nchi Nzima. Hawa wagombea Wa Chini wakipatikana Kwa Wingi basi ni rahisi kuwapanga Wanachama kuelekea uchaguzi mkuu Wa wabunge na madiwani ambao kimsingi wanahitajika kupata hamasa ya kukabiliana na wagombea Katili na wenye fedha wa CCM.
Na KUANZIA Sasa Chadema inapaswa kuwasaidia wale wote wanaopingwa na CCM Kama akina Dr. Slaa, Mwabukusi, Shivj, Mbatia, pia wale waliopo kuwaunga mkono au kuwakaribisha wale wanCCM wachache sana ambao Kwa dhahiri Wanapinga nchi kukabidhiwa Kwa wakoloni Kwa mgongo Wa Nyuma.
Chadema ikiendelea kuangalia uchaguzi Wa wabunge na madiwani tuu watapoteza uchaguzi mkuu Hata kama watashinda. Hakuna watu Wa kuhamasisha maandamano nchi Nzima kuanzia vijijini.
Pia ni vyema wakaanzisha será ya kuwalipa pesa za vikao wenyeviti Wa mitaa Ili kuwapa Nguvu na moyo Wa kujitoa .