Chadema wanafeli kwenye Suala la Matumizi ya fedha na namna ya kuhamasisha upatikanaji Wa fedha Kwa ajili ya watu Wa Chini yaani wale viongozi Wa matawi ya Chini au mitaa.
Bila fedha hakuna ushindi popote Kwa Karne hii. Hata Vita bila fedha hakuna ushindi. Mbele ya fedha Hata nchi imepigwa Bei.
Pesa ni Kila Kitu. Hata Uzalendo Kwa Sasa unahitaji fedha.
CCM walionufaika sana na kifo cha Ndesamburo mana alikua ndiye nguzo kubwa ya Chadema ukanda Wa Kaskazini. Alikua anauwezo Wa kugharamikia shughuli Zote za chama na kuzuia wasaliti kununuliwa na CCM.
Sasa cha KUFANYA ni Chadema kuwakubali Wazalendo wote popote walipo.
Pili kufanya uhakiki Wa Wanachama wao NDANI na nje ya nchi. Kuwajua Kwa majina na Kwa idadi Yao. Kuwapanga Wanachama Kwa makundi na Kwa Uwezo wao .
Baada ya kuwajua Wanachama Wa Chadema waliopo tayari Kupinga ukiukwaji Wa Sheria za uchaguzi Sasa waanze kuhamasisha michango KUANZIA wenye uwezo Wa kuchangia elfu moja mpaka million Kumi .
Kama Chadema itaweka watu waaminifu kukusanya michango bila tamaa kama zile za CCM basi Kwa Miezi Kumi na moja kufikia uchaguzi wa Serikali za mitaa watakua wamekusanya zaidí ya bil.20.
Pesa hizo zisikae makao makuu mana ni za Wananchi . Zitumike kuwagharamikia wagombea wote Wa Serikali za mitaa nchi Nzima. Hawa wagombea Wa Chini wakipatikana Kwa Wingi basi ni rahisi kuwapanga Wanachama kuelekea uchaguzi mkuu Wa wabunge na madiwani ambao kimsingi wanahitajika kupata hamasa ya kukabiliana na wagombea Katili na wenye fedha wa CCM.
Na KUANZIA Sasa Chadema inapaswa kuwasaidia wale wote wanaopingwa na CCM Kama akina Dr. Slaa, Mwabukusi, Shivj, Mbatia, pia wale waliopo kuwaunga mkono au kuwakaribisha wale wanCCM wachache sana ambao Kwa dhahiri Wanapinga nchi kukabidhiwa Kwa wakoloni Kwa mgongo Wa Nyuma.
Chadema ikiendelea kuangalia uchaguzi Wa wabunge na madiwani tuu watapoteza uchaguzi mkuu Hata kama watashinda. Hakuna watu Wa kuhamasisha maandamano nchi Nzima kuanzia vijijini.
Pia ni vyema wakaanzisha será ya kuwalipa pesa za vikao wenyeviti Wa mitaa Ili kuwapa Nguvu na moyo Wa kujitoa .
Mkuu '1000Digits', nimekusoma kwa uangalifu mkubwa sana hadi mwisho wa andiko lako, na ni nadra sana kwangu kutaka kurudia nilichosoma mara ya kwanza (huwa nasoma kwa spidi kubwa sana), ili niliyoyasoma kwa mara ya kwanza yaniingie vizuri akilini.
Sasa niseme, ninakubaliana nawe kwa ujumla. Kilichonifanya kusita kwa mara ya kwanza ni hayo maswala ya 'Hela'; siyo hela za kuwalipa wanachama huko matawini wanaofanya kazi kubwa sana; ni swala la "HELA" kuifanya kuwa rushwa katika uchaguzi.
Lakini hata hili, kwa wakati huu tuliomo, na hasa baada ya kuona CCM wanavyoitumia njia hiyo kuvuruga chaguzi ndani ya nchi hii, inanilazimu pia nilifumbie macho kama CHADEMA watahitaji kufanya hivyo ili kuwaondoa CCM madarakani.
Ninakubaliana nawe moja kwa moja, kuhusu CHADEMA kutafuta pesa za kuwasaidia katika chaguzi hizi, lakini isiwe ni kwa kuuza hisa za chama kwa wenye uwezo mkubwa wa pesa kwa mategemeo ya kuvuna baada ya CHADEMA kuingia madarakani.
Kwa hiyo, niseme hapa wazi, kwamba ninaungana nawe, na ninawasihi CHADEMA kuanzia sasa watafute vyanzo vya kuingiza pesa ndani ya chama kwa lengo la kufanikisha chaguzi zinazokuja karibuni. Ninakubaliana nawe pia, kwamba, pamoja na kuwahamasisha wanachama wao na viongozi wao huko mashinani, ni muhimu sana kuwapa motisha wafanye kazi zao kwa ufanisi zaidi huko kwenye ngazi za chini, kwa kuwawezesha kulipia mahitaji yao muhimu.
Mawazo haya yote ni sehemu ya mchango kwa chama hiki ili kiweze kufanikiwa zaidi katika shughuli yao kubwa ya kuiondoa madarakani CCM.