Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika anazungumza na Waandishi wa habari muda huu, Makao Makuu ya Chama hicho, Mikocheni Dar es salaam.
Fuatilia live mazungumzo yake hapa
Fomu za kugombea ngazi ya Taifa zinapatikana katika ofisi za makao makuu ya Chama (Mikocheni), makao makuu ya Mabaraza, ofisi za Kanda, ofisi za Chama za mikoa na wilaya kuanzia tarehe 17 Desemba 2024. Mwisho wa kurejesha fomu ni Januari 5, 2025, saa 10 jioni katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho, Mikocheni Dar es salaam au katika ofisi za Kanda anayotoka mgombea husika.
Wanachama wanaogombea katika mabaraza ya vijana, wanawake na wazee wanatakiwa kurejesha fomu hizo kwenye ofisi za makao makuu ya mabaraza ya Chama zilizoko mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam, au katika ofisi ya kanda anayotoka mgombea husika.
Gharama ya fomu itategemea nafasi ambayo mwanachama anagombea, na mgombea atatakiwa kuambatanisha risiti ya malipo ya fomu katika fomu yake. Fedha hiyo ilipwe kupitia akaunti ya chama au kwa kila baraza ambako mwanachama anatokea mgombea, na namba za akaunti zimeandikwa kwenye kila fomu ya mgombea.
Pia, Soma:
• Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA
Tangazo lote limeambatishwa hapo chini👇👇
Fuatilia live mazungumzo yake hapa
- CHADEMA yatoa tamko la Uchaguzi wa Kitaifa kwa mwaka 2024