CHADEMA watoa tamko zito, John Mnyika aanika gharama za fomu za kugombea na kutoa mwongozo

CHADEMA watoa tamko zito, John Mnyika aanika gharama za fomu za kugombea na kutoa mwongozo

CCM wanaumizwa sana na mambo yanavyoenda kimpangilio na kimkakati CHADEMA .. Hapa wale chawa kunguni na viroboto wao wamehazana kama wote
 
Siasa za Jino kwa Jino ndio zinafaa kwa sasa Nchini Tanzania, huyu Mama kaanza kuuwa na kupoteza Siasa za Kistaarabu za nini?!

Kumbukeni Wafanyabiashara wa Kariakoo walipofunga Maduka Serikali ya CCM yote ilihamia huko unajua ni kwanini?!

Lissu atafanya Siasa zihamie Mabarabarani ule Uwanja wa Mnazimmoja tunaenda kuweka kijiwe pale Occupy na kuipressure Serikali ya huyu Bibie tunataka REFORMS kwenye mfumo wetu wa Uchaguzi pamoja na KATIBA ILIYO BORA.
 
CCM ndiyo wanampenda Lissu awe mwenyekiti ndiyo cha kushangaza ,hata mkutano wa lissu umekuwa financed na Pastor Kinyambe Msigwa na waliohudhuria ni wanasisisemu waliovalia mavazi ya CDM.
Nyie lukeni wee, kwa macho yakawiada ukizungumza Mpinzani wakweli hapo CDM hata alieishia darasa la kwanza atakuambia ni Lisu.
 
Ukiona Mpinzani anakuunga mkono jua unaingia CHAKA ,kwanini haujiulizi CCM hawamtaki MBOWE wanamtaka TAL? Na kwanini Pastor Kinyambe Msigwa ndiyo a-finance mkutano wa Lissu? Na kwanini waliodhuria wengi pale kwqenye mkutano wa Lissu wengi walikuwa SISIEMU waliovalia mavazi ya CDM? Mimi nashangga jinsi sisisemu wanavyompigania Lissu awe mwenyekiti.
Kila mwana CCM anamtaka Mbowe.
 
CCM kwasasa wanafurahia hiyo Strategy ya Lissu kwamba NO REFORMS NO ELECTIONS hawajui kwamba tukianza Pressure kwa mwezi mmoja kila siku Mabarabarani mpaka Stock zao za Mabomu ya Machozi ziishe halafu waje Mezani tufanye REFORMS😁😄

Hakuna Lugha nyingine.
 
Lissu alikuwa na kiherehere cha nini kutangaza nia kabla chama hakijatangaza uchaguzi?
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika anazungumza na Waandishi wa habari muda huu, Makao Makuu ya Chama hicho, Mikocheni Dar es salaam.

Fuatilia live mazungumzo yake hapa

  • CHADEMA yatoa tamko la Uchaguzi wa Kitaifa kwa mwaka 2024
Katibu Mkuu anatangaza kuwa kutakuwa na uchaguzi wa Chama na Mabaraza kwa ngazi ya Taifa utakaofanyika Januari 2025.

Fomu za kugombea ngazi ya Taifa zinapatikana katika ofisi za makao makuu ya Chama (Mikocheni), makao makuu ya Mabaraza, ofisi za Kanda, ofisi za Chama za mikoa na wilaya kuanzia tarehe 17 Desemba 2024. Mwisho wa kurejesha fomu ni Januari 5, 2025, saa 10 jioni katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho, Mikocheni Dar es salaam au katika ofisi za Kanda anayotoka mgombea husika.

Wanachama wanaogombea katika mabaraza ya vijana, wanawake na wazee wanatakiwa kurejesha fomu hizo kwenye ofisi za makao makuu ya mabaraza ya Chama zilizoko mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam, au katika ofisi ya kanda anayotoka mgombea husika.

Gharama ya fomu itategemea nafasi ambayo mwanachama anagombea, na mgombea atatakiwa kuambatanisha risiti ya malipo ya fomu katika fomu yake. Fedha hiyo ilipwe kupitia akaunti ya chama au kwa kila baraza ambako mwanachama anatokea mgombea, na namba za akaunti zimeandikwa kwenye kila fomu ya mgombea.

Pia, Soma:

Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Tangazo lote limeambatishwa hapo chini👇👇

CHADEMA ni Chama Bora na mambo yake yako kisomi zaidi.
 
Kama fomu zinaanza kutolewa kesho, Lissu ya kwake aliipata wapi?
 
Back
Top Bottom