CHADEMA watoa tamko zito, John Mnyika aanika gharama za fomu za kugombea na kutoa mwongozo

CHADEMA watoa tamko zito, John Mnyika aanika gharama za fomu za kugombea na kutoa mwongozo

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika anazungumza na Waandishi wa habari muda huu, Makao Makuu ya Chama hicho, Mikocheni Dar es salaam.

Fuatilia live mazungumzo yake hapa

  • CHADEMA yatoa tamko la Uchaguzi wa Kitaifa kwa mwaka 2024
Katibu Mkuu anatangaza kuwa kutakuwa na uchaguzi wa Chama na Mabaraza kwa ngazi ya Taifa utakaofanyika Januari 2025.

Fomu za kugombea ngazi ya Taifa zinapatikana katika ofisi za makao makuu ya Chama (Mikocheni), makao makuu ya Mabaraza, ofisi za Kanda, ofisi za Chama za mikoa na wilaya kuanzia tarehe 17 Desemba 2024. Mwisho wa kurejesha fomu ni Januari 5, 2025, saa 10 jioni katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho, Mikocheni Dar es salaam au katika ofisi za Kanda anayotoka mgombea husika.

Wanachama wanaogombea katika mabaraza ya vijana, wanawake na wazee wanatakiwa kurejesha fomu hizo kwenye ofisi za makao makuu ya mabaraza ya Chama zilizoko mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam, au katika ofisi ya kanda anayotoka mgombea husika.

Gharama ya fomu itategemea nafasi ambayo mwanachama anagombea, na mgombea atatakiwa kuambatanisha risiti ya malipo ya fomu katika fomu yake. Fedha hiyo ilipwe kupitia akaunti ya chama au kwa kila baraza ambako mwanachama anatokea mgombea, na namba za akaunti zimeandikwa kwenye kila fomu ya mgombea.

Pia, Soma:

Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Tangazo lote limeambatishwa hapo chini👇👇

Naona ccm walikuwa wametega sikio la hatari wakidhani Mnyika atatoa tamko kuhusu Lisu. Wamejikuta hawana cha kubeba wamebaki wanashangaashangaa.
 
Wachaga wanaona ulaji unaenda kupotea, TL ataifufua chagadema iliyotaka kupotelea mikononi mwa makonyagi
Ccm imejaa mazombi na mauza UNGA pamoja na mafisadi ndio maana hakuna chama Tena Bali ni genge la matapeli yaliyopo madarakani Kwa mgongo wa vyombo vya Dola.
 
Naona ccm walikuwa wametega sikio la hatari wakidhani Mnyika atatoa tamko kuhusu Lisu. Wamejikuta hawana cha kubeba wamebaki wanashangaashangaa.
Toka lini ccm yakawa na akili mengi ya mafuasi yake ni mapumbavu ndio maana yameshinda asilimia 99 lakini yanahuzuni.
 
CDM acheni ubabaishaji na kupoteza muda bure, Lisu apewe Uenyekiti mambo yasiwe mengi
Kuna chama kinagawa nafasi ya uenyekiti bila kugombea ? Lisu atapewa au atagombea kwa vigezo alivyokidhi na kushindwa au kushinda.
 
Siasa ni Biashara.

CHADEMA wataenda kuuza hii nchi. Hata Fomu? Eti ina gharama zake kulingana na nafasi🙌🏾
 
Utashangaa safari hii na utathibitika kuwa mtabiri fake wa Chadema

Mbowe anashinda mapema tu tena kwa kura nyingi mno

Jiandae kuhama Chadema kwa hasira za Lisu kushindwa uchaguzi
Mbowe anategemea pesa za abduli na mama yake, kununua wapiga kura,
 
Hapa katikati kuna Uchaguzi ndani ya Chama sisi humu Jf hatupigi kura. mwenye kushinda na ashinde iwe ni Mbowe abakie kwenye Uenyekiti au tumpate Lissu kama Mwanyekiti mpya wa CHADEMA yote sawa.

Tuiache Demokrasia ifanye kazi yake na atakayeshinda tumuunge mkono kwa dhati.

Lakini mimi Imhotep ningekuwa ni Mjumbe na ninapiga kura mimi ningempigia Tundu Lissu.

Mungu Ibariki CHADEMA ✌️
 
Kwa jinsi CCM wanavyompa promo TAL awe mwenyekiti naona kuna shida pahala ,Ukizangiatia Abdul alionana na TAL na Pastor Kinyambe ni mshikaji wake sana TAL na ndiye aliyefinance mkutano.
Abdul alipelekwa kwa Lissu na Mbowe. Lissu akawafukuza. CCTV videos zipo ombeni Lissu aendelee kujaa hekma.
 
Back
Top Bottom