Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katika vitu ambavyo vimeifanya CCM isurvive, au kupata ahueni ya kisiasa ni kwa sababu CHADEMA ya uongozi uliopita haikuchagua kuisagia kunguni CCM kisawasawa kwa wananchi juu ya kero zinazowasumbua wananchi. Wao walibaki kuongelea vitu secondary kama vile demokrasia na kuacha mambo ya maana yanayohusu uhai wao. Ninatambua kuwa Demokrasia ni muhimu lakini siyo kipaumbele kwa wananchi kama vile msosi mezani, maji etc.
Mimi naamini, kama CHADEMA itageuza KERO za WANANCHI kuwa ndiyo TALKING POINTS ZAO kila viongozi wao waongeapo na vyombo vya habari, na kila waongeapo na wananchi , basi uungwaji wao mkono utakuwa mkubwa sana. Kuna haya mambo lazima CHADEMA hususan Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA lazima ajikite kuyazungumzia.
1. MAJI
Amini usiamini shida ya Maji Dar es salaam ni kubwa mno. Tena miezi hii ya karibuni mpaka leo kuna mgao mkali mno na wa kutisha wa maji. Cha kushangaza hii hali hujitokeza kila mwaka lakini hakuna chama cha siasa kilichotokea na kuibeba hii kuwa ni Agenda ya kuitandikia CCM. Yaani kwa jinsi wananchi wanavyoteseka, wanavyoumia, iwapo CHADEMA itawaonyesha wananchi kuwa inajua hilo tatizo, na kwamba CCM imefeli, na kwamba wananchi waiunge Mkono CHADEMA katika kudemand reforms za msingi ili huko mbeleni tuweze kupata serikali zilizo accountable kwa wananchi, basi wananchi wataiunga mkono CHADEMA kwa kasi na kwa wingi mno.
2. AJIRA KWA VIJANA
Leo vijana ambao wanamaliza vyuo na ngazi mbalimbali za elimu wanasaga lami, hali ya ajira ni mbaya mno. Haijakuwepo sauti ya kutosha ya CHADEMA kuwagonganisha vijana na CCM ili waichukie CCM. CHADEMA inaweza kupata uungwaji mkono kutoka ktk kundi la vijana iwapo viongozi wakuu wa CHADEMA watakuwa wanakosoa mara kwa mara kushindwa kwa serikali ya CCM kupunguza hilo tatizo then wao kuonyesha mbadala wa mikakati. Wawaambie vijana kuwa mbadala huo wa mikakati hautawezekana chini ya katiba hii na mifumo hii ya uchaguzi, kwa hiyo vijana waiunge mkono CHADEMA ktk azma ya kufanya Reforms nchini ili hatimaye iwezekane kupatikana leadership ya kuweka mbele maslahi yao.
3. UFISADI NA UPIGAJI
Hii ni agenda mama, kamwe CHADEMA wasiitupe agenda hii. Ni lazima kuirudiarudia agenda hii kwenye masikio ya wananchi. Kipindi cha uongozi wa CHADEMA uliopita, hii agenda waliitupa, wakaachana nayo. Hiyo ilikuwa ni mistake kubwa. Lazima CHADEMA hii ya sasa ya Lissu iendelee kuzodoa mifisadi, kusagia kunguni mbele ya umma. Yaani hakuna kuacha mafisadi wakapumua, na pia hakuna kuacha kuuzungumzia upigaji wa kutisha.
4. ISHU YA HUDUMA ZA AFYA NA GHARAMA ZAKE.
Kipindi cha CHADEMA ya Dr Slaa, huyu mkuu wa mkoa wa Dar aliyewaambia wanawake wasio na hela wakazalie nyumbani isingeweza kupita hivihivi. Kwanza CCM ilikuwa ikiogopa kutoa kauli za hovyo namna hii. Hata hivyo hoja yangu ni kwamba gharama za huduma za afya zinaongezeka sana huku umasikini wa watu ukiendelea kuongezeka. Hii Agenda, haswa huduma za akina mama wanaojifungua ktk mazingira magumu ktk hospitali za serikali, inapaswa kuzungumziwa pia mara kwa mara. Hii itawavutia wananchi na kujikuta wanasimama upande wa CHADEMA.
5. KUNA ISHU YA MAKATO KIBAO KUPITIA SIMU
Kuna hii kodi ya majengo kupitia malipo ya LUKU, yaani mpangaji analazimishwa kulipa kodi ya jengo linalomilikiwa na mwenye nyumba kila mwezi mpangaji anunuapo umeme. Kuna kodi serikali inakata kwa mtu pindi amtumiapo let say bibi yake kodi kijijini. Huu ni wizi, hupaswi kukata kodi au ushuru kwenye hela ya mtu anayomtumia bibi yake akanunue dawa au vyovyote vile. CHADEMA waitumie hii agenda kuwasagia kunguni kwa wananchi. Tena wapige za utosini haswa mpaka umma uone CCM haifai.
MWISHO
Ninatambua kuwa Sehemu kubwa ya Maongezi ya Viongozi wa CHADEMA yanahusu terms za kisiasa kama vile "Democracy", "Katiba mpya", "Uchaguzi huru na haki", Nataka niwaeleze tu kuwa japo hayo mambo ni muhimu, Yataeleweka zaidi kwa wananchi iwapo yatafungamanishwa na vitu vya uhai wao kama vile maji safi na salama ya kunywa, kana vile ajira za vijana, kama vile upatikanaji dawa na huduma nzuri hospitalini etc.
Kwa hiyo nategemea sasa kumsikia Lissu na Heche na makada wa CHADEMA wafanye adjustment kwenye maongezi yao pindi waongeapo kuhusu mambo ya nchi na siasa zake, yaani pamoja na mademokrasia yao wayapiganiayo lazima wajustify hayo kwa kugusa na kuisagia kunguni CCM kwa kuefeli kwenye social na economic fronts.