Pre GE2025 CHADEMA ya Lissu ijikite kwenye kuangazia kero za wananchi ipate uungwaji mkono dhidi ya CCM

Pre GE2025 CHADEMA ya Lissu ijikite kwenye kuangazia kero za wananchi ipate uungwaji mkono dhidi ya CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu una maanisha nini??

Kwa manufaa ya wananchi tuweke ushabiki na mahaba pembeni. Tupaze sauti kwa pamoja kuhusu usimamizi na utekelezaji wa ilani kama ilivyo kwanza.

Mambo ni mengi sana ambayo bado sana. Mfano hali ajira ni mbaya sana, maslahi ya wafanyakazi hayajaboreshwa yapata miaka kumi sasa., kilimo bado ni cha kujikimu, Elimu na miundo mbinu yake bado ni kijima na kadhalika.

Mkuu tuwe wakweli, tuambiane ukweli na tuusimamie ukweli!!!
Kwao hao hakuna mkweli hata mmoja,au japo mwenye uthubutu wa kusema ukweki
 
Moja ya udhaifu wa Lisu ni huo. Huwa hazungumzii mambo yanayomgusa mwananchi moja kwa moja. Uchumi, shida za wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wachimbaji, wafanyakazi, mama, watoto, wagonjwa nk nk. Amejikita zaidi kuzungumzia michakato ya kisiasa. CDM na Lissu wanataliwa kubadili tone.
watafanya hivyo. kuna akili nyingi pale. Hata Heche amaekuwa akizitaja hizo hoja nimemsikia mara kadhaa
 
Katika vitu ambavyo vimeifanya CCM isurvive, au kupata ahueni ya kisiasa ni kwa sababu CHADEMA ya uongozi uliopita haikuchagua kuisagia kunguni CCM kisawasawa kwa wananchi juu ya kero zinazowasumbua wananchi. Wao walibaki kuongelea vitu secondary kama vile demokrasia na kuacha mambo ya maana yanayohusu uhai wao. Ninatambua kuwa Demokrasia ni muhimu lakini siyo kipaumbele kwa wananchi kama vile msosi mezani, maji etc.

Mimi naamini, kama CHADEMA itageuza KERO za WANANCHI kuwa ndiyo TALKING POINTS ZAO kila viongozi wao waongeapo na vyombo vya habari, na kila waongeapo na wananchi , basi uungwaji wao mkono utakuwa mkubwa sana. Kuna haya mambo lazima CHADEMA hususan Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA lazima ajikite kuyazungumzia.

1. MAJI
Amini usiamini shida ya Maji Dar es salaam ni kubwa mno. Tena miezi hii ya karibuni mpaka leo kuna mgao mkali mno na wa kutisha wa maji. Cha kushangaza hii hali hujitokeza kila mwaka lakini hakuna chama cha siasa kilichotokea na kuibeba hii kuwa ni Agenda ya kuitandikia CCM. Yaani kwa jinsi wananchi wanavyoteseka, wanavyoumia, iwapo CHADEMA itawaonyesha wananchi kuwa inajua hilo tatizo, na kwamba CCM imefeli, na kwamba wananchi waiunge Mkono CHADEMA katika kudemand reforms za msingi ili huko mbeleni tuweze kupata serikali zilizo accountable kwa wananchi, basi wananchi wataiunga mkono CHADEMA kwa kasi na kwa wingi mno.

2. AJIRA KWA VIJANA
Leo vijana ambao wanamaliza vyuo na ngazi mbalimbali za elimu wanasaga lami, hali ya ajira ni mbaya mno. Haijakuwepo sauti ya kutosha ya CHADEMA kuwagonganisha vijana na CCM ili waichukie CCM. CHADEMA inaweza kupata uungwaji mkono kutoka ktk kundi la vijana iwapo viongozi wakuu wa CHADEMA watakuwa wanakosoa mara kwa mara kushindwa kwa serikali ya CCM kupunguza hilo tatizo then wao kuonyesha mbadala wa mikakati. Wawaambie vijana kuwa mbadala huo wa mikakati hautawezekana chini ya katiba hii na mifumo hii ya uchaguzi, kwa hiyo vijana waiunge mkono CHADEMA ktk azma ya kufanya Reforms nchini ili hatimaye iwezekane kupatikana leadership ya kuweka mbele maslahi yao.

3. UFISADI NA UPIGAJI
Hii ni agenda mama, kamwe CHADEMA wasiitupe agenda hii. Ni lazima kuirudiarudia agenda hii kwenye masikio ya wananchi. Kipindi cha uongozi wa CHADEMA uliopita, hii agenda waliitupa, wakaachana nayo. Hiyo ilikuwa ni mistake kubwa. Lazima CHADEMA hii ya sasa ya Lissu iendelee kuzodoa mifisadi, kusagia kunguni mbele ya umma. Yaani hakuna kuacha mafisadi wakapumua, na pia hakuna kuacha kuuzungumzia upigaji wa kutisha.

4. ISHU YA HUDUMA ZA AFYA NA GHARAMA ZAKE.
Kipindi cha CHADEMA ya Dr Slaa, huyu mkuu wa mkoa wa Dar aliyewaambia wanawake wasio na hela wakazalie nyumbani isingeweza kupita hivihivi. Kwanza CCM ilikuwa ikiogopa kutoa kauli za hovyo namna hii. Hata hivyo hoja yangu ni kwamba gharama za huduma za afya zinaongezeka sana huku umasikini wa watu ukiendelea kuongezeka. Hii Agenda, haswa huduma za akina mama wanaojifungua ktk mazingira magumu ktk hospitali za serikali, inapaswa kuzungumziwa pia mara kwa mara. Hii itawavutia wananchi na kujikuta wanasimama upande wa CHADEMA.

5. KUNA ISHU YA MAKATO KIBAO KUPITIA SIMU

Kuna hii kodi ya majengo kupitia malipo ya LUKU, yaani mpangaji analazimishwa kulipa kodi ya jengo linalomilikiwa na mwenye nyumba kila mwezi mpangaji anunuapo umeme. Kuna kodi serikali inakata kwa mtu pindi amtumiapo let say bibi yake kodi kijijini. Huu ni wizi, hupaswi kukata kodi au ushuru kwenye hela ya mtu anayomtumia bibi yake akanunue dawa au vyovyote vile. CHADEMA waitumie hii agenda kuwasagia kunguni kwa wananchi. Tena wapige za utosini haswa mpaka umma uone CCM haifai.

MWISHO
Ninatambua kuwa Sehemu kubwa ya Maongezi ya Viongozi wa CHADEMA yanahusu terms za kisiasa kama vile "Democracy", "Katiba mpya", "Uchaguzi huru na haki", Nataka niwaeleze tu kuwa japo hayo mambo ni muhimu, Yataeleweka zaidi kwa wananchi iwapo yatafungamanishwa na vitu vya uhai wao kama vile maji safi na salama ya kunywa, kana vile ajira za vijana, kama vile upatikanaji dawa na huduma nzuri hospitalini etc.

Kwa hiyo nategemea sasa kumsikia Lissu na Heche na makada wa CHADEMA wafanye adjustment kwenye maongezi yao pindi waongeapo kuhusu mambo ya nchi na siasa zake, yaani pamoja na mademokrasia yao wayapiganiayo lazima wajustify hayo kwa kugusa na kuisagia kunguni CCM kwa kuefeli kwenye social na economic fronts.


Lisu akitaka kupata kura nyingi sana ni rahisi mno .

Kama yupo humu ndani anitafute in box nimpe mikakati na mipango 10 ya kupata kura nyingi sana na hata akisema no reform no Election basi atapata uungwaji mkono mkubwa sana.
Samia hakubaliki Mbingu ni na duniani kwa watenda haki na wapinga uonevu.


Samia alitumiwa na wapelelezi wa kiuchumi kuwa kama mvumbuzi na mtangulizi wa Ukoloni wa kiuchumi kupitia Filamu ya Royal tours . Wazungu wamebaini kuwa Tanzania ni Tajiri kukaribiana na Kongo .

Sasa nchi nivamiwa na mafisadi na matapeli kwa jina la uwekezaji huku maisha ya watanzania wengi ikiwa ni mbaya sana ikiwemo vyombo vya dola kama polisi na Magereza na hata migambo wanaotumika kusaidia ushindi wa wahalifu wa kisiasa ndani ya CCM hawalipwi na serikali ya CCM.

Lakini pia ni Lazima Lisu awe mkomavu sasa na ajue kuwa Anaelekea Ikulu kuwatumikia watanzania wote na kuwa mfano mzuri wa utawala bora unaofuata misingi ya kisheria .

Jambo muhimu ni kutangaza hadharani kuwa anajua kuwa waliompiga Risasi walikua wametumwa lakini Mungu amemponya na kumpa nguvu na ujasiri zaidi wa kupigania haki .
Lisu atangaze Msamaha kwa Waliomtendea uovu huo . Amwachie Mungu .

Siku Lisu alitakapotangaza msamaha kwa watesi wake ndio Siku Mungu au Karma itakapo lipa kisasi na kumpeleka juu ya watesi wake na hakika Lisu ataiangusha CCM .

Msamaha kwa watesi wake ni Msamaha kwa JPM na wale waliokubali kutengeneza njama za kumpiga Risasi . Mpaka sasa kwa yanayotokea ya kasi ya mudafupi wa waliokua wasaidizi wa JPM kujimilikisha mali nyingi na kuuza rasilimali za nchi na njama za kuagiza sukari nje kifisadi tena kwa kampuni isiyozalisha sukari . Kuna walakini sana kuwa mauaji na utekaji uliokuwepo wakati wa JPM wafadhili wake ndio waliopo leo au ilikua ni agenda ya ndani na nje ya vyama vya kisiasa visivyopenda mtu mwenye kusimamia rasilimali za nchi .

Lisu kwa sasa aachane na siasa za kumkejeli Magufuli bali sasa aonyeshe mafanikio yake ambayo yanagusa maisha ya watu kama kusimamia dawa hospitalini ,nidhamu ya kasi ,watumishi hewa , miundo mbinu . Haya yanawahusu wananchi na siyo wanasiasa wa upinzani .

Hapo ni lazima uyataje utakayo unachukua kwa JPM ,na kwa Samia pia lakini yale mabaya utakabiliana nayo vipi kisheria bila kutoa mwanya kwa vyombo vya dola kutumia nguvu au kuteka na mara nyingine kuua .
Lakini ni lazima Lisu aonyeshe Udhaifu wa serikali ya Samia ukilinganisha na ya JPM katika kulinda maslahi ya nchi na amani ya nchi kupitia ushindani wa kibiashara unaotoa mianya ya kuua mashirika ya ndani na kuleta bidhaa feki na sukari ya kiwango cha chini.

Lakini pia umuhimu wa kuwatumia wawekezaji wa ndani ya nchi zaidi na kuwawajibisha bila kujali urafiki na ukanda jambo lililopelekea Samia kuamua kuwapa wageni kila shirika lenye kuzalisha na kuajiri watu kwa ndugu zake wa Oman ambao kimsingi ni matajiri wakubwa na watanzania hasa Watanganyika wengi ni maskini sana . Wamebaki kuwa machawa na wasindikizaji tu na kujenga mifumo ya ubinafsi usiojali wale wasio na ajira wala ardhi ya kumiliki . Kila mahali thamani ya ardhi imepanda na wenye uwezo wa kuinunua ni waarabu na wachina na mafisadi walioko kwenye utawala .

Lisu kwa miaka mitano amemsema sana JPM kwa ubaya tu jambo linalowatumiza sana wananchi wengi sana sana kwa sababu nchi huo sio ya wana CCM na Chadema tu na tu chama tudogo tudogo bali ni ya watu mil. 65 kati yao wenye umri zaidi ya miaka 18 ni zaidi ya mili 35 kati yao zaidi ya mil. 28 wanaokumbuka sana JPM . Hao wanasiasa wachache tena wengi wakiwa ni mlafisdi na wachache wasiozidi mil .4 ndio wanaielewa ubaya wa JPM .

Kwa hali hiyo ili kuigawa CCM ni lazima Lisu amsamehe JPM . Ameshalipa kisasi kwa kuwashinda majangili yaliyokuwa yanatumika kuhujumu wapinzani mpaka wanatekwa . Sasa ni wakati wa kumtangazia msamaha . Jambo hili litampa heshima kubwa sana ndani ya nchi hii lakini pia viongozi na waumini wa dini zote watamuunga mkono maana wanajua nguvu ya msamaha .


Nimefuatilia sana kauli za Musiba nikagundua kuwa ndani ya CCM kampeni zitakua ngumu sana . Hivi mtu kama Bashiru Ali atasimama aseme nini kuhusu Ufisadi na udalali wa ardhi na rasilimali za umma unaofanywa na Samia !?
Pole pole atasema nini kumpigia kampeni Samia aliyeuza nusu ya ardhi ya Tanganyika kwa miaka mitatu tu. Ardhi imekwenda yote na misitu yote na bandari zote .

CCM hawatapata kura zaidi ya mili. 6 kati ya watanzania zaidi ya mil.28 wenye uwezo wa kupiga kura .

Pia kumkashifu JPM ni kuwaumiza watu wa ukanda ya Ziwa wanaoamini mpaka kesho kuwa JPM kilikua ni chuma kweli kweli.
Hata mikoa ya Kusini pamoja na kunyang'anywa korosho lakini wamachinga wengi wanakumbuka JPM kwa kuwaondolea unyanyaswaji kwenye biashara zao.

Vyombo vya dola hasa Jeshi la wananchi na Polisi hata Magereza na JKT wanajua kuwa JPM alikua ni mzalendo aliyekomesha ugaidi na uingiaji na uingizwaji holela wa bidhaa na hata fedha haramu kutoka nje na kutoa mianya ya ufadhili wa magaidi na wauza madawa ya kulevya .

Sera nzuri zitampa ushindi mkubwa sana Lisu dhidi ya yule Rais Mgeni toka nchi jirani ambaye ni dalali wa mabeberu akishirikiana na bilionea Dakawa Kiwewe .
 
kwa kweli Mungu atusaidie tupate wa kutuamsha. Tumelala mno! kama mazombie


Ni kweli kabisa mfano leo kuna Marais wamekuja kukaa Tanganyika wakati Tanganyika haina Rais aliyewakilisha .

Yaani marais wageni wamekuja kujadili mambo yao hapa Tanganyika bila kuwa na mwenyeji .

Kikao cha marais wageni peke yao ndani ya Tanganyika , Wanajadili nini kwenye nchi yetu kama sio kuihujumu .

Huu ujinga tusiukubali kulazimishwa na akina Wasira na machawa wao.

Hivi kweli CCM inashindwa kutumetea Majaliwa Kasimu Majaliwa Mtanganyika Mwenzetu na mzalendo wa kuipgania nchi yetu inatumetea Rais mgani aliyekua anakaimu tu kwa Muda kutolana na Rais wetu kufia madarakani ?
Hapana ni Lazima CCM tuiadhibu vibaya sana mwaka huu . Ndio wataheshimu watu na kujua uchungu wanaoupata wakulima na wafugaji wanaoporwa ardhi zao na kupewa waarabu na wachina na wazungu na pesa kuishia kwenye rushwa za uchaguzi ili nchi iwe kama Kongo . Mabeberu kazi yao ni kutoa pesa kwa majeshi ya Kimataifa kwenda kulinda uporaji wao huku wakiwaletea Wananchi maskini wasio na elimu wala ajira silaha za kuuana na kumalizana .

Yote ni kwasababu ya kukosa uzalendo kwenye nchi zao na kuthamini wageni kama anavyofanya Samia kwa waarabu ,wazungu na wachina kwa sababu ya pesa za kampeni .
Aishiye zake 2025 hatutaki tena mafisadi kuuza nchi kwa sababu ya kuiweka CCM madarakani bila kujali vijana mamilio wasio na ajira .
 
Back
Top Bottom