Pre GE2025 CHADEMA ya Lissu ijikite kwenye kuangazia kero za wananchi ipate uungwaji mkono dhidi ya CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
aliyoeleza muungwana hapo juu hakuna hata moja halijatekelezwa na CCM gentleman..

Lipi jipya kati ya hayo au nalofikiri wewe?

au ni yapi waTz wanayahitaji hayatimizwa na CCM?au una mbwelambwela tu 🐒
Mkuu una maanisha nini??

Kwa manufaa ya wananchi tuweke ushabiki na mahaba pembeni. Tupaze sauti kwa pamoja kuhusu usimamizi na utekelezaji wa ilani kama ilivyo kwanza.

Mambo ni mengi sana ambayo bado sana. Mfano hali ajira ni mbaya sana, maslahi ya wafanyakazi hayajaboreshwa yapata miaka kumi sasa., kilimo bado ni cha kujikimu, Elimu na miundo mbinu yake bado ni kijima na kadhalika.

Mkuu tuwe wakweli, tuambiane ukweli na tuusimamie ukweli!!!
 
Huyo Lisu unayemsema wa kuzungumzia kero za wananchi ni yupi, ni huyu huyu Tundu, au yule kaka yake? Kama ni tundu basi nakuhakikishia utasubiri sana. Mtu mwenye umimi wa kiwango cha juu kiasi hicho hawezi kukumbuka kero za wananchi.
🤔 🤔 🤔
 
Jitu kutwa nzima linaasama mdomo Kama mamba na lile tumbo lake kutukana na kubagaza wenzie unafikiri Ana sera gani zaidi ya kuimba katiba mpya?? CDM imepotea kuruhusu wahuni kukiongoza
😲😲😲
 
ukiangalia hali ya miundo mbinu naona kama ni tofauti kabisa na miaka ya kuanzia 2013 kwenda nyuma, miundo mbinu imeboreshwa mno lakini pia upatikanaji wa maji safi kwa maeneo ya mjini inatia moyo. Kuna tatizo kubwa sana kwenye utoaji wa haki ambao unasababishwa na wafanyakazi wa serikali amba sio waaminifu na hawafuati miongozo. kama tunavyojua wahalifu wanapendana kuliko watenda haki na hata kama hawafahamiani wanalindana, kwa mfano ukijaribu kulalamika kwa trafiki kuhusu trafiki mwingine ambae hata hawafahamiani hapo hapo ataanza kumtetea na utaonekana wewe ni mtu hatari na anaweza kukuadthibu. kwahiyo shida kubwa iko kwa wafanyakazi wa serikali.
 
Mkuu hakuna kiongozi anaye jua kila kitu, ndio maana kuna washauri.

Kukumbusha tu, Jukumu la kuwasemea wananchi na kuisimamia serikali sio la upinzani pekee yake. Ni jukumu la kila mtu mzalendo.

Na kuhusu wananchi, mwananchi ni mimi, wewe, ndugu zetu na majirani waliotuzunguka mkuu!!

usijione upo ulimwengu tofauti!!
 
Ngoja tuone atajitune vipi. But I wish siasa zake pamoja na kudai mambo kama vile "tume huru", "katiba mpya" etc, ziwe pia ni kuibananisha CCM kwenye masuala yanayogusa maisha ya kila siku ya watu kama haya niliyoyaandika.
🌤️🙋‍♂️🎯✍️🤝🙏
 
Ngoja tuone atajitune vipi. But I wish siasa zake pamoja na kudai mambo kama vile "tume huru", "katiba mpya" etc, ziwe pia ni kuibananisha CCM kwenye masuala yanayogusa maisha ya kila siku ya watu kama haya niliyoyaandika.
🌤️🙋‍♂️🎯✍️🤝
🌤️🙋‍♂️🎯✍️🤝🙏
 

mkuu, umenena vema
 
Naunga mkono hoja
 

Shida ya maji hasa inapofika miezi ya November hadi January huwa ni kubwa sana.
 
Moja ya udhaifu wa Lisu ni huo. Huwa hazungumzii mambo yanayomgusa mwananchi moja kwa moja. Uchumi, shida za wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wachimbaji, wafanyakazi, mama, watoto, wagonjwa nk nk. Amejikita zaidi kuzungumzia michakato ya kisiasa. CDM na Lissu wanataliwa kubadili tone.
 

Observation yako ni sahihi. Lissu yuko sana kwenye mambo ya Justice, Democracy, Human rights lakini hana interest sana na issues za "Ugali" wa watu. Kama anataka CHADEMA ipate uungwaji mkono zaidi, Lazima aongeze arsenal yake ya agenda. Aongeze issues zinazogusa maisha yao ya kila siku.
 
Unapoleta mada unatakiwa kujua mfumo wa utendaji katika huduma za jamii.

Hayo mambo uliyoyaleta ni majukumu ya Serekali ambayo huwa inaandaa bajeti kila mwaka. Unaposema upinzani ujikite kujibu kero za wananchi watapata wapi rasilimali fedha na watu za kutekeleza na kuondoa hizo kero? Au kwa mfano suala ajira watalitekeleza vipi wakati siyo waliounda serikali?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Wakati Dr Slaa anagombea Urais kupitia Chadema, walikuwa na sera nzuri na hata kwenye kuziwasilisha waligusa angalua matatizo yaliyowagusa sana Wananchi, ninadhani kipindi kile Chadema waliwekeza haswa, kipindi cha Lowasa hiyo ishu ikapungua kidogo, ila wakati wa Lissu ndio kabisaa walipotea, sio Chadema wala Lissu aliyeonyesha kujipanga.
Sasa kipindi hiki, japokuwa wamechelewa kidogo, wanaweza bado kuwekeza kwenye kufanya research ya kero mbali mbali zinazowakabili Wananchi katika maeneo mbali mbali wakawaandaa Wahusika wao watakaowania nafasi za kiuongozi, kisha wakazutumia hizo kero dhidi ya wapinzani wao na namna ya kuzitatua.
 
Sasa kama Demokrasia hakuna katika uchaguzi,huo uungwaji mkono wako utaupataji ikiwa uchaguzi si wa haki,uwazi na uhuru.? Kama TUME si HURU hata watanzania wakupigie kura wote, atatangazwa yule ambaye TUME itamtaka.
 
Huyo Lisu unayemsema wa kuzungumzia kero za wananchi ni yupi, ni huyu huyu Tundu, au yule kaka yake? Kama ni tundu basi nakuhakikishia utasubiri sana. Mtu mwenye umimi wa kiwango cha juu kiasi hicho hawezi kukumbuka kero za wananchi.
Uko sahihi,
Dr Slaa aliweza sana kwenye hili, lakini sasa sioni wa kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…