CHADEMA ya sasa ndio chama kikuu cha upinzani kinachoogopwa zaidi na mamlaka

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Mwenye macho haambiwi tazama
Mwenye masikio haambiwi sikia
Watanganyika si mapoyoyo kiasi hicho kwamba hawaoni na hawaelewi kinachoendelea
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kupigwa na kuteswa
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kubambikiwa kesi mbalimbali zisizo na dhamana
Kutekwa na kupotezwa
Kuuliwa
Kuingilia mifumo ya kichama
Msajili kutengua maamuzi halali ya chama
Kugombanisha na kufitinisha wanachama na viongozi wao
Kufanya kila aina ya mbinu chafu kuhakikisha CHADEMA inapotea kwenye siasa za Tanganyika

Hawa wanaofanya hivi sidhani kama wana maono ya mbali.. Na sidhani kama wana tafakuri yakinifu
Kama wakiwaza vema kwa hekima na kwa tafakuri kuu.. Wataacha mara moja harakati zao hasi dhidi ya hiki chama

Unajua ni kwanini? Kwasasa wananchi waliochoka na siasa za ccm wana pa kuweka tumaini lao
Wana pa kusikiliza na kutii na kutulia
Jaribio lolote la kutaka kukiua hiki chama cha CHADEMA ni sawa na kutaka kumuua mchungaji mwenye kuongoza kundi kubwa la wanyama!

Mkimuua mchungaji hili kundi kubwa lenye imani na uaminifu mkubwa kwa mchungaji wao.. Litakosa kiongozi na litakosa udhibiti likitokea la kutokea..

Hakuna kitu kinachoogofya na kutisha sana kama kundi lisilo na cha kupoteza na lililokosa miongozo na waongozaji..

Iogopeni sana CHADEMA lakini msiifanyie hila chafu.. Ikifa tambueni hakuna atakayebaki salama
 
Iogopeni sana CHADEMA lakini msiifanyie hila chafu.. Ikifa tambueni hakuna atakayebaki salama
Ninakukosoa kwa Kichwa cha Mada Kisicho endana na hali halisi:

"CHADEMA ya Sasa ndio chama tarajiwa kuiongoza Tanzania; hata mamlaka maghumashi zinakigwaya"- Hiki ndicho kichwa cha mada stahiki, mkuu wangu 'Mshana Jr.
 
Sijajua inawezekanaje Chadema kujikuta kinapigwa vita na mamlaka zote. Lakini Mamlaka ya Wananchi wanakipenda 100%
 
Nchi hii kuna watu na viongozi 1635 wakimalizwa hao nchi ingefunguka ...tunaitaji dictator kwelikweli tena mzalendo haswa
 
Kila asset imekua activated kuhakikisha wanatekeleza mkakati mkuu. Je watafanikiwa kukiangusha? Muda utatupa majibu.
 
chadema ni imani kuiua ni kazi sana atakaye jaribu anakufa yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…