CHADEMA ya sasa ndio chama kikuu cha upinzani kinachoogopwa zaidi na mamlaka

Mwenye macho haambiwi tazama
Mwenye masikio haambiwi sikia
Watanganyika si mapoyoyo kiasi hicho kwamba hawaoni na hawaelewi kinachoendelea
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kupigwa na kuteswa
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kubambikiwa kesi mbalimbali zisizo na dhamana
Kutekwa na kupotezwa
Kuuliwa
Kuingilia mifumo ya kichama
Msajili kutengua maamuzi halali ya chama
Kugombanisha na kufitinisha wanachama na viongozi wao
Kufanya kila aina ya mbinu chafu kuhakikisha CHADEMA inapotea kwenye siasa za Tanganyika

Hawa wanaofanya hivi sidhani kama wana maono ya mbali.. Na sidhani kama wana tafakuri yakinifu
Kama wakiwaza vema kwa hekima na kwa tafakuri kuu.. Wataacha mara moja harakati zao hasi dhidi ya hiki chama

Unajua ni kwanini? Kwasasa wananchi waliochoka na siasa za ccm wana pa kuweka tumaini lao
Wana pa kusikiliza na kutii na kutulia
Jaribio lolote la kutaka kukiua hiki chama cha CHADEMA ni sawa na kutaka kumuua mchungaji mwenye kuongoza kundi kubwa la wanyama!

Mkimuua mchungaji hili kundi kubwa lenye imani na uaminifu mkubwa kwa mchungaji wao.. Litakosa kiongozi na litakosa udhibiti likitokea la kutokea..

Hakuna kitu kinachoogofya na kutisha sana kama kundi lisilo na cha kupoteza na lililokosa miongozo na waongozaji..

Iogopeni sana CHADEMA lakini msiifanyie hila chafu.. Ikifa tambueni hakuna atakayebaki salama
We poyoyo umechanganyikiwa, nani anaiogopa? Wangeendesha siasa za kistaarabu kuna mtu angehangaika nayo. Kufanya uhalifu ndiyo siasa? Mtapigwa sana spana nyie nyumbu. Chadema inayojua siasa imeshakufa, hii ya sasa ni kundi la wahuni wanaolazimisha kupata dola kwa nguvu. Hiyo ni ngumu bwanamdogo, msipoangalia huu ndio mwisho wa hao wahuni.
 
Ninakukosoa kwa Kichwa cha Mada Kisicho endana na hali halisi:

"CHADEMA ya Sasa ndio chama tarajiwa kuiongoza Tanzania; hata mamlaka maghumashi zinakigwaya"- Hiki ndicho kichwa cha mada stahiki, mkuu wangu 'Mshana Jr.
Mazombie yaleyale majina yaleyale yakifikiri JF itawasaidia. Nendeni kwa wananchi, chama kila siku inakimbiwa halafu anakuja mwehu huku eti kinaogopwa
 
Mwenye macho haambiwi tazama
Mwenye masikio haambiwi sikia
Watanganyika si mapoyoyo kiasi hicho kwamba hawaoni na hawaelewi kinachoendelea
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kupigwa na kuteswa
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kubambikiwa kesi mbalimbali zisizo na dhamana
Kutekwa na kupotezwa
Kuuliwa
Kuingilia mifumo ya kichama
Msajili kutengua maamuzi halali ya chama
Kugombanisha na kufitinisha wanachama na viongozi wao
Kufanya kila aina ya mbinu chafu kuhakikisha CHADEMA inapotea kwenye siasa za Tanganyika

Hawa wanaofanya hivi sidhani kama wana maono ya mbali.. Na sidhani kama wana tafakuri yakinifu
Kama wakiwaza vema kwa hekima na kwa tafakuri kuu.. Wataacha mara moja harakati zao hasi dhidi ya hiki chama

Unajua ni kwanini? Kwasasa wananchi waliochoka na siasa za ccm wana pa kuweka tumaini lao
Wana pa kusikiliza na kutii na kutulia
Jaribio lolote la kutaka kukiua hiki chama cha CHADEMA ni sawa na kutaka kumuua mchungaji mwenye kuongoza kundi kubwa la wanyama!

Mkimuua mchungaji hili kundi kubwa lenye imani na uaminifu mkubwa kwa mchungaji wao.. Litakosa kiongozi na litakosa udhibiti likitokea la kutokea..

Hakuna kitu kinachoogofya na kutisha sana kama kundi lisilo na cha kupoteza na lililokosa miongozo na waongozaji..

Iogopeni sana CHADEMA lakini msiifanyie hila chafu.. Ikifa tambueni hakuna atakayebaki salama
yaani mamlaka ziogope chama kinachoongozwa na vibaka wa kisiasa wanaotumia uropokaji wa kilofa kufanya siasa? hiyo ni completely nonsense gentleman 🐒
 
Mwenye macho haambiwi tazama
Mwenye masikio haambiwi sikia
Watanganyika si mapoyoyo kiasi hicho kwamba hawaoni na hawaelewi kinachoendelea
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kupigwa na kuteswa
Viongozi na wanachama wa CHADEMA kubambikiwa kesi mbalimbali zisizo na dhamana
Kutekwa na kupotezwa
Kuuliwa
Kuingilia mifumo ya kichama
Msajili kutengua maamuzi halali ya chama
Kugombanisha na kufitinisha wanachama na viongozi wao
Kufanya kila aina ya mbinu chafu kuhakikisha CHADEMA inapotea kwenye siasa za Tanganyika

Hawa wanaofanya hivi sidhani kama wana maono ya mbali.. Na sidhani kama wana tafakuri yakinifu
Kama wakiwaza vema kwa hekima na kwa tafakuri kuu.. Wataacha mara moja harakati zao hasi dhidi ya hiki chama

Unajua ni kwanini? Kwasasa wananchi waliochoka na siasa za ccm wana pa kuweka tumaini lao
Wana pa kusikiliza na kutii na kutulia
Jaribio lolote la kutaka kukiua hiki chama cha CHADEMA ni sawa na kutaka kumuua mchungaji mwenye kuongoza kundi kubwa la wanyama!

Mkimuua mchungaji hili kundi kubwa lenye imani na uaminifu mkubwa kwa mchungaji wao.. Litakosa kiongozi na litakosa udhibiti likitokea la kutokea..

Hakuna kitu kinachoogofya na kutisha sana kama kundi lisilo na cha kupoteza na lililokosa miongozo na waongozaji..

Iogopeni sana CHADEMA lakini msiifanyie hila chafu.. Ikifa tambueni hakuna atakayebaki salama

Kwa jinsi mashambulizi makali zaidi kutoka kwa Watawala wakishirikiana pamoja na Vikosi vyake vyote kabisa vya wapiganaji wanavyoishambulia CHADEMA, ni uthibitisho tosha kabisa kwamba Viongozi wa CHADEMA waliopo hivi Sasa siyo Mamluki kama wale waliotangulia siku za nyuma. Huu ni uthibitisho kwamba kwa sasa hivi CHADEMA ina Viongozi ambao ni Wapinzani wa Ukweli, siyo Watu Mamluki, Viongozi hawa wa CHADEMA hawanunuliki wala hawahongeki. Viongozi hawa wa CHADEMA kwa hakika ni Miamba Migumu isiyoweza kupasuliwa hata kwa mabomu ya atomic!
 
Back
Top Bottom