JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kikidai kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuendelea kushikiliwa kusikojulikana watu watatu wakiwamo viongozi wa wawili wa chama hicho wilayani Temeke kinyume cha sheria, Jeshi hilo limesema halina taarifa kuhusu madai hayo.
Kwa mujibu wa Chadema viongozi hao wana siku ya tatu sasa tangu wakamatwe maeneo ya Buza Agosti 18, 2024.
Chama hicho kimewataja watu hao kuwa ni Katibu wa Jimbo la Temeke Jacob Mlay, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Wilaya ya Temeke Deusdedith Soka na dereva wa bodaboda, Frank Mbisa.
Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Foka Dinya amesema jeshi hilo halina taarifa kuhusu madai hayo. Dinya amesema kama Chadema wanalitaja jeshi hilo, itakuwa wanajua waliko.
“Jeshi la Polisi hatuna taarifa za kupotea kwa watu au kushikiliwa kwa watu hao wa Chadema,” amesema Dinya alipozungumza na Mwananchi leo Agosti 20, 2024.
Taarifa za madai ya kukamatwa viongozi hao zilianza kusambaa jana Agosti 19, 2024 kupitia mitandao ya kijamii ikionyesha picha za viongozi hao zikiambatana na maandishi yaliyoshapishwa kuwa wamekamatwa na polisi na hawajulikani walipo.
CHANZO: MWANANCHI