Hebu kwanza mkuu 'Makupa'. Naelewa unacho llamikia, lakini kwani kufikia kwenye ngazi hii pamekuwepo na mchujo wa hao wagombea, au ni hiari ya mtu kujitokeza mbele kugombea?
Hili unalo lilalamikia wewe ni sawa na hili jingine ambalo ni kubwa zaidi,.... Tazama vizuri hayo majina. Unaweza kusema CHADEMA imewabagua watu kwa sababu ya imani zao ndiyo sababu hawaonekani kwenye orodha hizo?
Sijui kama CHADEMA wanyayo sera ya kuwakataa watu kwa misingi ya wanako tokea au imani zao. Ila kama ni lawama, labda tuseme hawajafanya bidii ya kutosha kukifanya chama kiwe na mwonekano wa kitaifa zaidi. Inabidi waongeze bidii katika eneo hilo.