Katibu Mkuu wa CHADEMA , John Mnyika atatoa tamko muhimu la Chama kwa umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari, leo Jumatano, Juni 3, 2020.
Je, Atamjibu Msajili wa vyama kuhusu vyama kupeleka ratiba za kampeni ilhali mikutano bado imezuiliwa na haijulikani lini itaruhusiwa.
Je, Ataijibu NEC Taifa kuja na kanuni zake mfukoni, mjawapo ikiwa mawakala kutopewa nakala ya matokeo.
STAY TUNED.
=====
"Bado kuna mwanya katika muda huu wa Bunge uliobakia, upelekwe muswada Bungeni ambao utafanya tupate Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kuhakikisha tunaitoa Ccm madarakani" Katibu Mkuu wa CHADEMA
"Tunatawaka watia nia wa CHADEMA kusoma miongozo vizuri, kuna muongozo mahsusi kabisa toka 2012, wazingatie muongozo katika hatua mbalimbali, wakikiuka Chama hakitasita kuwachukulia hatua,ili kuhakikisha tunapata viongozi walio bora katika Taifa" Katibu Mkuu Nyika.
"CHADEMA kimefungua milango 2 muhimu, kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mlango wa 1; ambao tunaufungua leo ni wa kuruhusu watia nia wa Urais kupitia Chadema na mlango wa 2; ni mlango wa majadiliano na vyama vyenye dhamira ya kweli ya kushirikiana kuitoa Ccm madarakani" Mnyika.
"Tulitaka Tume Huru ya Uchaguzi ili kuwe na uchaguzi huru na wa haki, bado tunasisitiza kwa watawala tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kwa njia nyingine kuhakikisha Ccm wanatoka madarakani, katika wakati muafaka tutawaongoza wananchi kudai haki" Mnyika.