CHADEMA yafungua rasmi pazia la mbio za Urais. Wanaotaka kuomba ridhaa hiyo waruhusiwa

CHADEMA yafungua rasmi pazia la mbio za Urais. Wanaotaka kuomba ridhaa hiyo waruhusiwa

Pamoja na hilo Chadema inakaribisha mazungumzo na majadiliano kutoka vyama vingine hali ni mbaya.
Atimae chadema imeomba (poo)msaada kwa vyama vingine

Hata uchaguzi uliopita kulikuwa na huo umoja.
 
Mnyika ni kama mmechelewa katika hili. Kwa sasa muangalie Sana mtaji wenu. Hili laiti mngelifanya kwenye 2016 huko labda lingekuwa na tija ila mlishindwa kusoma alama za nyakati. Mlishindwa kuchukua hatua stahiki Kwa wakati stahiki, mshindani wenu alianza kuwatoa kwenye reli kidogo kidogo mkawa mnacheka Tu sasa mmetoka mazima Kwa hayo unayosema inaweza kuwa ngumu zaidi sasa hivi.

Mlijisahau Sana kama chama, mmepunguzwa nguvu Sana sasa hivi, na amini nakwambia asilimia kubwa ya mtaji wenu wa watu mmeupoteza. Either wamejiunga na mpinzani wenu au wameamua kuwa neutral Tu. Asilimia kubwa Sana ya watu wameamua kuachana na siasa kutokana na mtindo wa siasa ulivyo nchini sasa hivi.



Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu una angalizo la msingi, believe me watanzania wana uwezo wa kugeuka usiku mmoja. Kimsingi uhuru wa kufanya siasa kwa cdm umebanwa ndio maana unachookiona huamini kama watu wana msukumo tofauti. Kinachotakiwa ni mzungumzaji mzuri mwenye mvuto kwa cdm. Kama wananchi hawa hawa waliambiwa na cdm zaidi ya miaka 7 kuwa Lowasa ni fisadi, lakini ndani ya miezi 2 gia ikabadilishwa angani wakamkubali unategemea nini?
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA , John Mnyika atatoa tamko muhimu la Chama kwa umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari, leo Jumatano, Juni 3, 2020.

Je, Atamjibu Msajili wa vyama kuhusu vyama kupeleka ratiba za kampeni ilhali mikutano bado imezuiliwa na haijulikani lini itaruhusiwa.

Je, Ataijibu NEC Taifa kuja na kanuni zake mfukoni, mjawapo ikiwa mawakala kutopewa nakala ya matokeo.

STAY TUNED.

=====

"Bado kuna mwanya katika muda huu wa Bunge uliobakia, upelekwe muswada Bungeni ambao utafanya tupate Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kuhakikisha tunaitoa Ccm madarakani" Katibu Mkuu wa CHADEMA

"Tunatawaka watia nia wa CHADEMA kusoma miongozo vizuri, kuna muongozo mahsusi kabisa toka 2012, wazingatie muongozo katika hatua mbalimbali, wakikiuka Chama hakitasita kuwachukulia hatua,ili kuhakikisha tunapata viongozi walio bora katika Taifa" Katibu Mkuu Nyika

"CHADEMA kimefungua milango 2 muhimu, kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mlango wa 1; ambao tunaufungua leo ni wa kuruhusu watia nia wa Urais kupitia Chadema na mlango wa 2; ni mlango wa majadiliano na vyama vyenye dhamira ya kweli ya kushirikiana kuitoa Ccm madarakani" Mnyika

"Tulitaka Tume Huru ya Uchaguzi ili kuwe na uchaguzi huru na wa haki, bado tunasisitiza kwa watawala tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kwa njia nyingine kuhakikisha Ccm wanatoka madarakani, katika wakati muafaka tutawaongoza wananchi kudai haki" Mnyika
Safari hii mtampa bendera mwanaccm yupi?
 


Baada ya Tangazo la Katibu Mkuu John Mnyika, hii maana yake ni kwamba kipyenga sasa kimepulizwa, labda kwa taarifa tu na hasa kwa wenye ubongo usioelewa haraka kutokana na matatizo ya kuzaliwa (low score). Ni hivi, Chadema inaenda kushinda urais wa Tanzania octoba 2020, liwake jua ama inyeshe mvua, kwa hili naishukuru Kamati Kuu ya Chadema kwa mipango mizito ya ndani na nje.

Kwahiyo basi unapoweka jina la Mgombea wako unayependekeza ufahamu kwamba unayempendekeza huenda akawa Rais wa Tanzania iwapo chama kitampitisha, hivyo zingatia sana weledi, uungwana, afya ya akili pamoja na Uhusiano mzuri wa kimataifa (hapa pamejaa mambo yote ikiwemo haki za kikatiba na haki za binadamu)


Karibuni kwa mchakato .
 
Nenda kachukue fomu pale, yule waliemtegemea kaona maji marefu kupambana na daktari katafuta sababu nyingi ili aendele kubaki huko huko.
Chadema huwa hawana mambo mengi sana hasa kama utaweza kuongea vizuri na Mbowe au fanya mawasiliano kwanza na Lowassa kujua kiasi gani kinahitajika kupeperusha bendera.
Huu ndio wakati wa kazi na bata sio kila siku kumtuma mtoto mdogo Zitto kukuongelea. Njoo upambane kianaume uone maana ya mtu kuitwa chuma Magufuli.
 
Safari hi CDM hawaokoti dodo chini ya mnazi
 
Hongereni chadema fomu shilingi ngapi ya kugombea uraisi Hamjaweka Bei? CCM huwa tunaweka wazi
 
Hongereni japo mmebanwa sana mbavu na vyombo vya dola.Kule ccm marufuku mwanaccm kugusa fomu ya urais.ukigusa tu unafukuzwa.polepole anasema tayari ana mgombea wake tayari
 
Pamoja na hilo Chadema inakaribisha mazungumzo na majadiliano kutoka vyama vingine hali ni mbaya.
Atimae chadema imeomba (poo)msaada kwa vyama vingine
Wamejikuta wamesuswa na vyama vyote vya upinzani utapeli haulipi walipoingia Ukawa vyama vingine ilibifi chadema iwe lovely to other parties lakini wakivyojiona wamepata wabunge wengi na uongozi wa KUB bungeni wakaota jeuri wanafiki wakubwa hawapati chama . Chadema is a no party material kwa Sasa!! Duni Haji alipowaambia chadema kila mtu ana ndevu hawakuelewa Mimi nilimwelewa.Wangem handle vizuri Baada ya mgogoro CUF wapemba wote wangejiunga chadema wasingeenda ACT wazalendo na hiyo ingeijenga chadema zaidi bara na visiwani

Mbowe na genge lake hawana long term Vision.Sasa hivi wamechelewa wapambane na hali Yao wakidhani kupata wabunge na madiwani wengi na ruzuku kubwa kuliko vyama vingine vya upinzani wao ndio super kwa utapeli wao imekula kwao
 
Mpaka saizi bado mnapambana kuitoa ccm madarakani badala ya kupambana na kutoa ujinga na umasikini kwa watu unaofanya ccm waendelee kubaki madarakani.

Kuitoa ccm bila mipango madhubuti na mikakati ya muda mrefu, ni kujidanganya
 
Back
Top Bottom