CHADEMA yafungua rasmi pazia la mbio za Urais. Wanaotaka kuomba ridhaa hiyo waruhusiwa

CHADEMA yafungua rasmi pazia la mbio za Urais. Wanaotaka kuomba ridhaa hiyo waruhusiwa

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628

Katibu Mkuu wa CHADEMA , John Mnyika atatoa tamko muhimu la Chama kwa umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari, leo Jumatano, Juni 3, 2020.

Je, Atamjibu Msajili wa vyama kuhusu vyama kupeleka ratiba za kampeni ilhali mikutano bado imezuiliwa na haijulikani lini itaruhusiwa.

Je, Ataijibu NEC Taifa kuja na kanuni zake mfukoni, mjawapo ikiwa mawakala kutopewa nakala ya matokeo.

STAY TUNED.

=====

"Bado kuna mwanya katika muda huu wa Bunge uliobakia, upelekwe muswada Bungeni ambao utafanya tupate Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kuhakikisha tunaitoa Ccm madarakani" Katibu Mkuu wa CHADEMA

"Tunatawaka watia nia wa CHADEMA kusoma miongozo vizuri, kuna muongozo mahsusi kabisa toka 2012, wazingatie muongozo katika hatua mbalimbali, wakikiuka Chama hakitasita kuwachukulia hatua,ili kuhakikisha tunapata viongozi walio bora katika Taifa" Katibu Mkuu Nyika.

"CHADEMA kimefungua milango 2 muhimu, kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mlango wa 1; ambao tunaufungua leo ni wa kuruhusu watia nia wa Urais kupitia Chadema na mlango wa 2; ni mlango wa majadiliano na vyama vyenye dhamira ya kweli ya kushirikiana kuitoa Ccm madarakani" Mnyika.

"Tulitaka Tume Huru ya Uchaguzi ili kuwe na uchaguzi huru na wa haki, bado tunasisitiza kwa watawala tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kwa njia nyingine kuhakikisha Ccm wanatoka madarakani, katika wakati muafaka tutawaongoza wananchi kudai haki" Mnyika.
 
Tuna kusubiri kwa hamu mhe. J J mnyika katibu makini unayetokana na chama makini..kwa jinsi ccm wanavyo muota mnyika kuhamia ccm...cku akihamia watampa urais wa nchi kbs...[emoji1787][emoji1787]
 
Katibu Mkuu wa @ChademaTz Mhe. @jjmnyika atatoa tamko muhimu la Chama kwa umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari, leo Jumatano, Juni 3, 2020.

Je, Atamjibu Msajili wa vyama kuhusu vyama kupeleka ratiba za kampeni ilhali mikutano bado imezuiliwa na haijulikani lini itaruhusiwa.

Je, Ataijibu NEC Taifa kuja na kanuni zake mfukoni, mjawapo ikiwa mawakala kutopewa nakala ya matokeo.

STAY TUNED.
Saa ngapi ataanza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi tunashuhudia LB7 Vs UB10 tu humu jukwaani.
 
Chadema fateni katiba yenu jamani, hivi Tumaini Makene ana kazi gani sasa? Toka akwae kisiki cha corona naona mwenyekiti anaogopa media house
 
Kwakweli mwaka huu Chadema inaelekea kwenye uchaguzi mkuu huku ikiwa imepoteza mvuto 100%.
Sioni kama kuna mbunge wa chadema anaye weza kurudi bungeni, walio soma alama ndio hao wamekihama chama huenda wakashinda. Heri yao wamejiongeza mapema, walio baki wamekubali kufa na tai shingoni. Kila la heri!
 
Anaunga mkono juhudi na hutoamini macho yako,,Stay tuned

Kama Kaunga mkono juhudi Slaa watu hatuyumbi, ndio itakuwa Mnyika? Kizazi cha kuisujudia CCM kiliisha na Nyerere, hiki sio kizazi cha CCM.
 
Kwakweli mwaka huu chadmema inaelekea kwenye uchaguzi mkuu huku ikiwa imepoteza mvuto 100%.
Sioni kama kuna mbunge wa chadema anaye weza kurudi bungeni, walio soma alama ndio hao wamekihama chama huenda wakashinda.....heri yao wamejiongeza mapema, walio baki wamekubali kufa na tai shingoni. Kila la heri

Hayo ndio matamanio ya kila mwanaccm cdm ipoteze mvuto. Lakini kwenye chaguzi tunaona uhayawani wa wazi dhidi ya cdm.
 
Kwakweli mwaka huu chadmema inaelekea kwenye uchaguzi mkuu huku ikiwa imepoteza mvuto 100%.
Sioni kama kuna mbunge wa chadema anaye weza kurudi bungeni, walio soma alama ndio hao wamekihama chama huenda wakashinda.....heri yao wamejiongeza mapema, walio baki wamekubali kufa na tai shingoni. Kila la heri
Hayo ni mawazo yako na mtazamo wako
 
Siku hizi nani yule naniii yulee naniii Bashiru akiongea wala havutii masikion mwa watu. Sijui tatizo nini
 
Back
Top Bottom