Chadema yaipongeza Taifa Stars kwa kufuzu AFCON 2019

Mkuu umeongea mengi ya msingi Ila nikukosoe sehemu moja tu, hili taifa halijajigawa. Kama ilivyo mitazamo ya mambo mengine mitandaoni na hili lipo hivyo. Mfano mwaka 2016,2017 nilikuwa nje ya nchi kwa muda wa miezi mingi nilikuwa nikipitia humu naogopa, nilihisi Tanzania watu hawana hata 200 ya kunywa chai asubuhi kwa namna uchumi ulivyokuwa unaongelewa humu. Kila thread ni uchumi unayumba, uchumi unayumba.Wengine njaa,njaa mpaka Lissu naye kuingiza siasa kwenye njaa.Niliporudi nikashangaa mambo tofauti kabisa, mtaani ni picha tofauti na ya humu JF. Hivyo hivyo swala unalolisema la kuligawa Taifa, kwa mtu asiyekuwa nchini angepitia Jamii Forums akaona thread zenu za kuiombea mabaya Taifa Stars na LIKES kibao angesikitika Sana akihisi watanzania wamefikia hapa?, kumbe ni wanafiki wachache tu wa mitandaoni.Nimeenda Taifa huo umati wa watu na foleni za magari, uswahilini ndo usiseme na wachache waliotaka timu ifungwe ni sababu za kubet(Mikeka), wenyewe wanasema nimeiua Taifa Stars point zilikuwa nyingi, wala hawana time na siasa zenu. Nimegundua ndo maana mmejazana humu kudanganyana eti watu wanamchukia JPM na serikali hii, mwakani mtashangazwa Sana msipobadilika. Watu sio wajinga kuzungusha tena mikono.

Kwa taarifa yako hao watu wameenda uwanjani sio kwa hiyo hamasa ambayo unadhani imeletwa na hao wanasiasa. Hata simba na Yanga watu huwa wanajaa nao wamepewa hamasa na mwanasiasa gani? Huwa tunajazana kuangalia mechi za Ulaya na huwa gumzo kila mahali, nayo ni mwanasiasa gani aliwahamasisha?

Huko Sudan leo wanaandamana, unadhani hawana hata hela ya kunywa hiyo chai? Libya walimtoa Gaddafi, unadhani walikosa hela ya chakula? Kwa taarifa yako waliotoa likes sio kwamba hawapendi mpira bali walitoa baada ya kuona nuksi inaingizwa kwenye timu ya taifa na wanasiasa uchwara na ujumbe umefika.

Sio tunejazana humu kusema watu wanamchukia JPM, huku ndio sehemu pekee unayoweza kusema hivyo, jaribu kusemea hayo huko hadharani uone nini kitakukuta. Udhibitisho wa hilo ni juzi wakati wa mjadala wa amani alichosema Mzee Butiku kwamba kwa sasa taifa letu limekuwa la watu minong'ono, je ni kipi kimesababisha watu kuwa wanong'onaji?

Unasema mwakani watu tutashangazwa na ushindi, hakuna atakayeshangazwa kwani tunajua haheshimu box la kura. Zaidi ya nusu ya matokeo yatakuwa ni ya kupika ili kufikia haya unayoyasema. Kikubwa na kutaka kujua watu hawaridhishwi utaona idadi ndogo ya wapiga kura itakayojitokeza kama ushahidi wa kwamba watu hawaridhiki. Nikurahisushie hapendwi bali anaogopwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya wasiomkubali.
 
Mkiwa na kiongozi mkuu ambaye hataki siasa anataka kazi tu ,mambo yote hubadilika kutoka juu mpaka chini ,tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa na baadhi ya wasomi hasa Chadema kwamba rais hata akiwa mwizi ,mvivu mzururaji mambo yataenda tu kisa eti urais ni taasisi?

Asante Taifa stars, Simba na bondia Mwakinyo

Asante kasi ya Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
insanity!
 
Sijaona mahali chadema wameombea tanzania ifungwe. Mbowe alikuwepo uwanjani.. james mbatia alikuwepo uwanjani.. na viongoz wengine wote walikuwa waki support stars maana walikuja wamevaa jezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbatia ni kiongozi wa NCCR-MAGEUZI na wala chama chake hakijatajwa hivyo usimchanganye na huo upuuzi. Pili, viongozi hawana shida sana maana wao wanajua wanachokifanya, tatizo lipo kwa vinyamkera wao humu mitandaoni wasiojua lolote.

Mwisho, ushindi huu ni wa watanzania wote bila kujali rangi, itikadi, umri, imani, n.k Waliokuwa wanabeza muwasamehe wako katika political foolish age.
 
Sijasema kuwa mbatia ni kiongoz wa chadema. Nimesema wa vyama vya upinzan walikuwepo coz hata NCCR mageuzi ni chama cha upinzani.
Taifa star imeshinda.. tanzania imeshinda.
Mbatia ni kiongozi wa NCCR-MAGEUZI na wala chama chake hakijatajwa hivyo usimchanganye na huo upuuzi. Pili, viongozi hawana shida sana maana wao wanajua wanachokifanya, tatizo lipo kwa vinyamkera wao humu mitandaoni wasiojua lolote.

Mwisho, ushindi huu ni wa watanzania wote bila kujali rangi, itikadi, umri, imani, n.k Waliokuwa wanabeza muwasamehe wako katika political foolish age.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CDM kama chama nafurahi kikipongeza, na mimi nakipongeza kwa uzalendo huo, tatizo lipo kwa nyie wafuasi wa mitandaoni. Zile nyuzi za kuitakia mabaya Taifa Stars mmetoa likes za kutosha na ku comment mabaya na wewe ukiwemo, na huu Uzi wako wa kupongeza umepata LIKES za wafuasi, wengi wao wakiwa walewale mliotoa likes kwenye kuiombea mabaya kisa mratibu mkuu Makonda, huu kama sio UNAFIKI ni Nini??!?..
Ulikagua na kumuhoji mmojammoja ukatambua ni CDM? Makalio ya ngedere.
 
Kwa taarifa yako Makonda au Wema Sepetu hawana mchango wowote kwenye ushindi huu
Kama mlijua hawana mchango wowote zile dua mbaya dhidi ya Tanzania zilikua za nini?Sema saiz mnatapatapa tu

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Kwa jinsi nilivyoona uzalendo ulotukuka wa Watanzania pale U/taifa asee nimeamini hawa wapiga mbiu wa Ufipa siyo chochote. Yaani walivyokua wanaanzisha nyuzi za kutaka stars ishindwe na walivyokua wanajipa ma likes ungeweza sema taifa asingefika mtu kwa jinsi walivyokua wanahamasishana dhidi ya stars. Nimeamini ndo maana CCM inawapiga bao sana hawa jamaa, ukiwaona Jf wapo wengiiii kweli lakini kumbe Taifa watu wakaenda wengi zaidi yao. Na kwenye uchaguzi hivyo hivyo kwenye Jf wapo wengiii lakini kura wanapata chache.
Yani ukiwa unashinda Jf na hujiongezi unaweza sema Taifa limesimama na mda wowote kutaibuka vita. Before mechi walitukana na sana na kuhamasishana wasiende uwanjani. Walikua wanashabikia Uganda na Lesotho, baada ya kuumbuka wanakuja na vi nyuzi uchwara kujifanya nao wamefurahi ushindi.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Hivi yule jamaa aliyesema TZ wakishinda AFCON atakunya kuanzia Mwenge hadi Airport ni wa CCM au wa CDM?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu ndiye aliyedeki barabara 2015,jibu unalo ni chama gani.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Na wewe mkuu ifike hatua uache unafiki ilifikia hatua ukahoji kuhusu mkuu wa mkoa kuwa kwenye kamati ya ushindi
Nitaendelea kuhoji kwa sababu ni dhahiri hana sifa hiyo , kwanza alichaguliwa na nani ?
 
Wa kupongezwa ni Makonda na kamati yake siyo TFF!

TFF ni wavurundaji na bila Makonda kuingilia kati hadithi ya kichwa cha mwendawazimu ingeendelea!
uongo utakusaidia nini , huyo makonda aliletwa na nani kwenye ile kamati batili ?
 
Kwa taarifa yako hao watu wameenda uwanjani sio kwa hiyo hamasa ambayo unadhani imeletwa na hao wanasiasa. Hata simba na Yanga watu huwa wanajaa nao wamepewa hamasa na mwanasiasa gani? Huwa tunajazana kuangalia mechi za Ulaya na huwa gumzo kila mahali, nayo ni mwanasiasa gani aliwahamasisha?

Huko Sudan leo wanaandamana, unadhani hawana hata hela ya kunywa hiyo chai? Libya walimtoa Gaddafi, unadhani walikosa hela ya chakula? Kwa taarifa yako waliotoa likes sio kwamba hawapendi mpira bali walitoa baada ya kuona nuksi inaingizwa kwenye timu ya taifa na wanasiasa uchwara na ujumbe umefika.

Sio tunejazana humu kusema watu wanamchukia JPM, huku ndio sehemu pekee unayoweza kusema hivyo, jaribu kusemea hayo huko hadharani uone nini kitakukuta. Udhibitisho wa hilo ni juzi wakati wa mjadala wa amani alichosema Mzee Butiku kwamba kwa sasa taifa letu limekuwa la watu minong'ono, je ni kipi kimesababisha watu kuwa wanong'onaji?

Unasema mwakani watu tutashangazwa na ushindi, hakuna atakayeshangazwa kwani tunajua haheshimu box la kura. Zaidi ya nusu ya matokeo yatakuwa ni ya kupika ili kufikia haya unayoyasema. Kikubwa na kutaka kujua watu hawaridhishwi utaona idadi ndogo ya wapiga kura itakayojitokeza kama ushahidi wa kwamba watu hawaridhiki. Nikurahisushie hapendwi bali anaogopwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya wasiomkubali.

Kwanza kabisa,unaonekana kutokueleww kile ambacho jamaa amejaribu kukwambia hapo juu....
Pili ni kwamba unarudi kule kule kwenye hulka yenu ya kila siku,kuwa kwa kadri mnavyofikiria/kuona nyinyi mambo yanayoendelea katika nchi hii,basi na wengine wote wanaona hivyo hivyo au wanapaswa kuona hivyo.
 
Sasa kama wengine hawaoni hivyo unashangaa nini sisi wengine tukiona tofauti na hao watu?
 
Kwa jinsi nilivyoona uzalendo ulotukuka wa Watanzania pale U/taifa asee nimeamini hawa wapiga mbiu wa Ufipa siyo chochote. Yaani walivyokua wanaanzisha nyuzi za kutaka stars ishindwe na walivyokua wanajipa ma likes ungeweza sema taifa asingefika mtu kwa jinsi walivyokua wanahamasishana dhidi ya stars. Nimeamini ndo maana CCM inawapiga bao sana hawa jamaa, ukiwaona Jf wapo wengiiii kweli lakini kumbe Taifa watu wakaenda wengi zaidi yao. Na kwenye uchaguzi hivyo hivyo kwenye Jf wapo wengiii lakini kura wanapata chache.
Hukutuona Chadema pale uwanjani ? ujinga ni kudhani timu ya Taifa ni mali ya ccm
 
Back
Top Bottom