Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufafanua kwa umma kupitia vyombo vya habari kuhusu kauli ya upotoshaji iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera kupitia mojawapo ya magazeti ya Jumatatu, Novemba 9, 2020, kwamba majina ya Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema yameshatangazwa na kuwasilishwa bungeni, wakati Kamati Kuu ya Chama haijafanya uteuzi wala kuwasilisha majina hayo kwa NEC kama taratibu zinavyoelekeza.
Kupitia barua hiyo ya tarehe 09/11/2020, yenye Kumb. Na. C/HQADM/20/TU/05/140, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, kwenda kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, ikiwa na kichwa cha habari kisemacho, YAH; KAULI POTOFU YA NEC KUWA IMESHATANGAZA NA KUWASILISHA BUNGENI MAJINA 19 YA WABUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA CHADEMA, Chadema imeitaka NEC kuheshimu na kuzingatia mamlaka ya uteuzi wa Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum kwa mujibu wa Katiba ya Chadema Ibara ya 7.7.16(q) na (z) yako kwa Kamati Kuu ya Chama ambayo hadi sasa haijafanya uteuzi wowote wa nafasi hizo wala kuwasilisha majina kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
“Kauli hii ni potofu kwa kuwa Chadema (kupitia Katibu Mkuu ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuwasilisha orodha ya majina ya wanaopendekezwa kuteuliwa kuwa wabunge), haijawasilisha orodha yoyote,” imesema sehemu ya barua hiyo ambayo pia nakala yake imepelekwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
Kupitia Gazeti la Nipashe, Toleo la Jumatatu, Novemba 9, 2020, ISSN 0856. Na. 0580394, katika habari iliyopewa uzito ukurasa wa kwanza, ikiwa na kichwa cha habari “NEC yatangaza viti maalum, Chadema yaambulia 19,” imeiandikwa kuwa NEC imeweka wazi idadi ya Wabunge wa Viti Maalum huku, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Mahera akinukuliwa akitoa kauli ya upotoshaji kuwa waandishi wa habari wakiyataka majina hayo watayapata bungeni.
Imetolewa leo Jumatatu, Novemba 9, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema