Pre GE2025 CHADEMA yaitisha Mkutano na Waandishi wa Habari. Mbowe kuweka hadharani Azimio la Mtwara

Pre GE2025 CHADEMA yaitisha Mkutano na Waandishi wa Habari. Mbowe kuweka hadharani Azimio la Mtwara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 2925847

Hii ndio Taarifa Mpya iliyosambazwa kwa dharula na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka huko Mtwara .

Endelea kubakia hapahapa JF kwa taarifa kamili

06 March 2024
Mtwara, Tanzania

LIVE: CHADEMA WANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


View: https://m.youtube.com/watch?v=ebhU2B_SCm4

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Aikaeli Mbowe sasa yupo live anatoa Azimio la Mtwara
  • Wajumbe wa CC ya CDM
  • Tumechoka kusubiri katiba mpya
  • 1991 Tume ya Nyalali iliyoundwa na rais Ali Hassan Mwinyi ilitoa ripoti
  • Sheria za ukandamizaji zifutwe Tume ya Nyalali ilisema
  • Mapendekezo ya jaji Robert Kisanga 2008 CCM wamepuuza
  • Rais Benjamin Mkapa aliitupilia mbali maoni ya judge Mark Bomani 2005
  • Rais Jakaya Kikwete alishindwa kutekeleza mapendekezo ya Tume ya jaji Joseph Sinde Warioba Warioba 2014
  • JPM alikataa kila kitu 2015
  • Serikali ya rais Samia Hassan imekataa katiba mpya na mfumo wa haki ulio wa kidemokrasia 2024
  • Kutokana na hayo CHADEMA itachukua hatua ya pili baada ya Maandamano
  • Wiki ya Maandamano katika kila miji iliyo makao makuu ya mikoa yote yatakayoanza tarehe 22 April 2024
  • Kuonesha watanzania wamechoka kupuuzwa na pia hali ngumu ya maisha unaowakabili wananchi wote
  • Watanzania waliopo ktk mabara yote duniani kama diaspora nao waandamane ill dunia ifahamu ubakaji wa demokrasia unaoendelea nchini Tanzania
  • Maandamano yatasitishwa pale tu katiba mpya itakapopatikana., matatizo ya ugumu wa maisha kupatiwa suluhu n.k
  • Tume Huru ya Uchaguzi Taifa
  • Uchakachuaji wa daftari la wapiga kura
  • Kuenguliwa wagombea wa upinzani
  • Mgawanyo wa eneo bunge (jimbo) unaoangalia idadi ya watu
  • Refa na mchezaji ambao wote wanatoka CCM kupitia makada wa CCM walio maDED kusimamia uchaguzi
  • Matumuzi sahihi ya vyombo vya umma TBC, Habari Leo Daily News ambayo yanatumia kodi za watanzania wote
  • Mgombea binafsi aruhusiwe kugombea nafasi ya kisiasa bila kupitia chama cha siasa
  • Mazungumzo baina ya CHADEMA na CCM yameingia mkwamo, hivyo maandamano yasiyo na kikomo kuendelea
  • N.K
MASWALI KUTOKA KWA WAANDISHI WA HABARI :
  • Katiba mpya inaonekana bila katiba mpya haiwezi kukaa madarakani kutatua matatizo ya wananchi
  • Mgawanyo wa eneo bunge (jimbo) unaoangalia idadi ya watu upo sahihi
  • Bima ya afya, je CHADEMA inaweza kuokoa afya na maisha ya watu
  • Je maandamano yamefikia malengo
  • Utaratibu wa rais kusikkiliza kero za wananchi unafaa?
  • Tija ya diaspora iliyopo New York, Tokyo, London, Berlin
  • Maswali zaidi n.k
Freeman Mbowe na Tundu Lissu wanajibu maswali ya waandishi toka Azam Media, Radio Maria, Chama cha Waandishi mkoa wa Mtwara n.k
 
""WAMEPEWA LIFT WANATAKA KUPIGA NA HORN""
°Watanzania sio wajinga kiasi hicho,
°Tumechoka watu ambao kila uchao, wamejawa na uchu, hawapendi kuona taifa likistawi, they are based unto nation negativities!..
How shits are them!?.
CCM, Chapa kazi, tatua kero za watanzania, it's a main key, that frustrate them.
°Umeme wa uhakika
°Maji ya uhakika
°Huduma za afya za uhakika
°masoko ya mazao ya uhakika
°Pembejeo kwa wakati,
~Hawana hoja ya msingi.
---AZIMIO UCHWARA - - -
 
Tundu Lissu asisitiza Mabonde, milima hayapigi kura bali ni watu na kuwa kura moja ya Dar es Salaam iwe sawa na kura moja Bukoba, Mbeya n.k na kurejea takwimu za Tume ya Uchaguzi :

bali watu Mtwara wapiga kura 930,000 majimba bunge 10, huku Dar es Salaam watu 3,000,000 majimbo 10, Mbeya 1,000,000 majimbo 7.

Majimbo-bunge lazima yawe na idadi sawa ya wapiga kura ili kura zote ziwe na uzito unaolingana. Mfawanyo wa maeneo / jimbo bunge lazima yawe na idadi sawa

Kutoka maktaba :

SENSA NA DEMOKRASIA
Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi
Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.

Source : Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya 2022 na zilizopita
 
Tundu Lissu asisitiza Mabonde, milima hayapigi kura bali ni watu na kuwa kura moja ya Dar es Salaam iwe sawa na kura moja Bukoba, Mbeya n.k na kurejea takwimu za Tume ya Uchaguzi :

bali watu Mtwara wapiga kura 930,000 marimba 10, huku Dar es Salaam watu 3,000,000 majimbo 10, Mbeya 1,000,000 majimbo 7

Kutoka maktaba :

SENSA NA DEMOKRASIA

Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.

Source : Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya 2022 na zilizopita
Daaah
 
06 March 2024
Mtwara, Tanzania

Tundu Lissu - Kura moja ya mpiga kura jimbo lolote Dar es Salaam ilingane na kura moja ya mpiga kura iwe Nkasi, Mpanda. Kongwa, Ruangwa.

Hoja ni kwa sababu wapiga kura ni binadamu wala siyo mabonde, vilima, nyika, misitu, mlima au bahari na ndiyo maana kura moja popote Tanzania ilingane kwa uzito ule ule bila visingizio kuwa jimbo letu lina bahari na wanyama pori wengi vitu ambavyo havipigi kura



KUTOKA MAKTABA :

TUNDU LISSU - UGAWAJI MAJIMBO BUNGE, SENSA NA UKUBWA WA ENEO




Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania

N.B
Idadi ya majimbo bunge upande wa Bara ulingane na idadi ya watu kwa kuwa ukubwa wa eneo siyo kigezo msingi
 
Back
Top Bottom