MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Remember, it's a good teacher if you really want to learn!
Asiye funzwa na mamaye...!Remember, it's a good teacher if you really want to learn!
Lazima tuukubali ukweli, kumchukua Lowasa na kumfanya mgombea wa Urais lilikuwa kosa kubwa.
Lile lilikuwa funzo kubwa. Badala ya kuendelea kulalamika na kujilaumu, ni vema kuutumia uzoefu huo kwaajili ya kusonga mbele.
Binafsi siyo mfia CHADEMA lakini ni vema kama Taifa kuwa na chama imara cha upinzani, na kwa sasa hakuna kingine zaidi ya CHADEMA. Chama hiki ndiyo pekee chenye watu waliojitoa kikamilifu katika kujenga nchi yenye demokrasia na kuoinga mfumo wa usultani ambao umeota mizizi.
...hufunzwa na ulimwengu!
Sasa hivi amerudi nyumbani je na huko kwenu mnamuonaje? ni asset au liability?Leo Lowassa na genge lake amekuwa hafai na hakuleta mafanikio yoyote ndani ya CHADEMA!
Ikumbukwe Dkt. Slaa aliuza kama Lowassa ni Asset or Liability lakini alichoambulia ni matusi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA na wanachama.
Kwa sasa majibu wameanza kuyatoa wao wenyewe kwa sababu ukweli huwa haupuuzwi!
Mtoto uliyemzaa huwezi kumkataa hata kama ni asset or liability!sasa hivi amerudi nyumbani je na huko kwenu mnamuonaje? ni asset au liability?
Sent using Jamii Forums mobile app
Wapuuzi wote Hawa..imewachukua miaka minne kuliona hili. Kamati Kuu ijuzulu kwanza!Chadema yajutia kupokea waliokatwa majina CCM
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinajutia uamuzi kiliochukua wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kuchukua wale waliokatwa kutoka CCM ambao sasa wamerejea katika chama chao cha zamani.
Akizungumza ofisi za Makao Makuu ya Chadema jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashim Juma alisema pamoja na heshima aliyonayo kwa aliyekuwa mgombea wa Ukawa mwaka 2015, Edward Lowassa, lakini tathmini ya baraza hilo imeonyesha hakuwa na msaada mkubwa kwenye chama.
“Kwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 tuliweka mgombea dhaifu ambaye kwanza alishindwa kulinda kura zetu kwa sababu ya u-CCM wake ambao hakuuvua wakati huo.
“Lakini pia ndani ya Ukawa tulisimamisha mgombea mwenza ambaye pia hakuwa mwana Chadema, hivyo hakuwa na uchungu na chama chetu.
“Kwa hiyo, hatutaki kuona makosa tuliyoyafanya mwaka 2015 yakijirudia mwaka huu, hasa baada ya kukijenga chama nchi nzima kuanzia ngazi ya chini kabisa, kazi tuliyoifanya kwa miaka miwili.
“Ni wazi kwamba tayari kuna mmoja wa viongozi wakuu wa chama, ambaye ana uchungu na chama, aliyeko nje ya nchi kwa sasa, ambaye ameshaeleza utayari wake wa kuwania urais iwapo atateuliwa na chama kwa hiyo huyo ndiye tunayemuunga mkono,” alisema Juma.
Mwenyekiti huyo wa Bazecha alisisitiza kuwa kwa sasa hawako tayari kutumika kama njia ya baadhi ya wanasiasa kutaka kutimiza mahitaji yao binafsi kwa kuingia katika chama hicho na wakikosa wanachokihitaji wanarejea kule walikotoka, kama walivyofanya baadhi ya wanasiasa walioingia Chadema kisha kurejea CCM baada ya kushindwa kutimiza malengo yao binafsi.
Alisema japokuwa halina mamlaka ya Kamati Kuu ya chama, wala ya mkutano mkuu, baraza hilo linatamka wazi kwamba haliko tayari kuona uongozi wa chama hicho ukizungumza suala la kumpokea Bernard Membe, aliyekuwa mwanachama wa CCM ambaye Kamati Kuu ya chama chake imeridhia kwa kauli moja kumvua uanachama.
Alieleza kuwa anajua kwamba kwa hali halisi Membe hataweza kujiunga na Chadema kwa sasa iwapo atataka kutumia fursa hiyo kutimiza mahitaji au matakwa yake binafsi.
Akizungumzia uwezekano wa Membe kwenda katika chama kingine cha siasa, alisema itakuwa jambo jema iwapo chama kingine kitampokea kwa kuwa itasaidia upande wa upinzani kupunguza zaidi kura za CCM ambayo alidai kuwa kwa sasa imeshindwa kujijenga kama ilivyojengwa na Abdulrahman Kinana aliyekuwa Katibu Mkuu kabla ya Dk. Bashiru Ally.
“Kama ataenda chama kingine tutashukuru sana, kwa sababu atasaidia kupungusa kura za CCM, na tunamuombea aende huko ili tuzidi kupunguza na kuzigawanya zaidi kura za CCM,” alisema Juma.
CHanzo: Mtanzania
Dr Slaa huyohuyo unaye Fanya rejea ndiye alisema wakati kapokewa Lowassa kuwa Chadema imetoa kinyesi (Eddo) chooni (CCM) na kukileta Chumbani (Chadema).Leo Lowassa na genge lake amekuwa hafai na hakuleta mafanikio yoyote ndani ya CHADEMA!
Ikumbukwe Dkt. Slaa aliuza kama Lowassa ni Asset or Liability lakini alichoambulia ni matusi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA na wanachama.
Kwa sasa majibu wameanza kuyatoa wao wenyewe kwa sababu ukweli huwa haupuuzwi!
Tatizo si kuwapokea, tatizo ni kuwapa nafasi kubwa za uongozi mara tu walipokuja CHADEMA. Kwa mawazo yangu, hata Membe akitaka kuja CHADEMA aje ila awe mwanachama wa kawaida kama mwanachama mwingine.Chadema yajutia kupokea waliokatwa majina CCM
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinajutia uamuzi kiliochukua wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kuchukua wale waliokatwa kutoka CCM ambao sasa wamerejea katika chama chao cha zamani.
Akizungumza ofisi za Makao Makuu ya Chadema jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashim Juma alisema pamoja na heshima aliyonayo kwa aliyekuwa mgombea wa Ukawa mwaka 2015, Edward Lowassa, lakini tathmini ya baraza hilo imeonyesha hakuwa na msaada mkubwa kwenye chama.
“Kwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 tuliweka mgombea dhaifu ambaye kwanza alishindwa kulinda kura zetu kwa sababu ya u-CCM wake ambao hakuuvua wakati huo.
“Lakini pia ndani ya Ukawa tulisimamisha mgombea mwenza ambaye pia hakuwa mwana Chadema, hivyo hakuwa na uchungu na chama chetu.
“Kwa hiyo, hatutaki kuona makosa tuliyoyafanya mwaka 2015 yakijirudia mwaka huu, hasa baada ya kukijenga chama nchi nzima kuanzia ngazi ya chini kabisa, kazi tuliyoifanya kwa miaka miwili.
“Ni wazi kwamba tayari kuna mmoja wa viongozi wakuu wa chama, ambaye ana uchungu na chama, aliyeko nje ya nchi kwa sasa, ambaye ameshaeleza utayari wake wa kuwania urais iwapo atateuliwa na chama kwa hiyo huyo ndiye tunayemuunga mkono,” alisema Juma.
Mwenyekiti huyo wa Bazecha alisisitiza kuwa kwa sasa hawako tayari kutumika kama njia ya baadhi ya wanasiasa kutaka kutimiza mahitaji yao binafsi kwa kuingia katika chama hicho na wakikosa wanachokihitaji wanarejea kule walikotoka, kama walivyofanya baadhi ya wanasiasa walioingia Chadema kisha kurejea CCM baada ya kushindwa kutimiza malengo yao binafsi.
Alisema japokuwa halina mamlaka ya Kamati Kuu ya chama, wala ya mkutano mkuu, baraza hilo linatamka wazi kwamba haliko tayari kuona uongozi wa chama hicho ukizungumza suala la kumpokea Bernard Membe, aliyekuwa mwanachama wa CCM ambaye Kamati Kuu ya chama chake imeridhia kwa kauli moja kumvua uanachama.
Alieleza kuwa anajua kwamba kwa hali halisi Membe hataweza kujiunga na Chadema kwa sasa iwapo atataka kutumia fursa hiyo kutimiza mahitaji au matakwa yake binafsi.
Akizungumzia uwezekano wa Membe kwenda katika chama kingine cha siasa, alisema itakuwa jambo jema iwapo chama kingine kitampokea kwa kuwa itasaidia upande wa upinzani kupunguza zaidi kura za CCM ambayo alidai kuwa kwa sasa imeshindwa kujijenga kama ilivyojengwa na Abdulrahman Kinana aliyekuwa Katibu Mkuu kabla ya Dk. Bashiru Ally.
“Kama ataenda chama kingine tutashukuru sana, kwa sababu atasaidia kupungusa kura za CCM, na tunamuombea aende huko ili tuzidi kupunguza na kuzigawanya zaidi kura za CCM,” alisema Juma.
CHanzo: Mtanzania
punguza jazba za kike.Wapuuzi wote Hawa..imewachukua miaka minne kuliona hili. Kamati Kuu ijuzulu kwanza!
Baada ya kuyasoma maandiko yako haya''Chama hiki ndiyo pekee chenye watu waliojitoa kikamilifu katika kujenga nchi yenye demokrasia na kuoinga mfumo wa usultani ambao umeota mizizi'', nimehitimisha kuwa inawezekana wewe sio mfia CHADEMA lakini mapenzi yako kwa CHADEMA yanakupa upofu wa kutotambua kuwa muundo wa CHADEMA kikatiba ni copy & Paste ya muundo wa CCM.
Chama ambacho kikatiba kinafanana na chama ambacho kiko madarakani hakiwezi kuwa chama kikuu cha upinzani chenye matokeo tofauti na yale yanayofanywa na chama tawala. Tofauti ya chama tawala na CHADEMA ni majina tu ya viongozi na kutokuwa madarakani lakini utendaji kazi wake ni sawa.
CCM walijua kukitunza ''kinyesi'' chao ili ''kisitoe harufu'' lakini CHADEMA kwa ulafi wao wa madaraka wakadhani wanaweza kukitumia kuwapeleka ikulu bila kunuka na matokeo yake ndio haya kwa sasa wanajitokeza na kuanza kusema ukweli!Dr Slaa huyohuyo unaye Fanya rejea ndiye alisema wakati kapokewa Lowassa kuwa Chadema imetoa kinyesi (Eddo) chooni (CCM) na kukileta Chumbani (Chadema).
Tunasubiri kauli yake mahsusi kuwa Kinyesi (Eddo)kimetolewa chumbani (Chadema) na kurudishwa chooni (CCM).
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha mkuu ndiyo maana wakaitwa nyumbuLeo Lowassa na genge lake amekuwa hafai na hakuleta mafanikio yoyote ndani ya CHADEMA!