CHADEMA yajutia kupokea waliokatwa CCM na kudai haitapokea tena katika uchaguzi mkuu

Naunga mkono Kwa nguvu zoote Hii hapa na ingefaa na viongozi Wengine kitaifa walisemee swala hili la kuwapokea walioshindikana huko CCM Haswa kuomba radhi Wananchi kwa yale ya 2015

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona dalili kwa sasa zinaonesha kuwa Membe atajiunga CDM...
NCCR, ACT na CUF officially watakuwa chini ya ccm...
 
Wapuuzi wote Hawa..imewachukua miaka minne kuliona hili. Kamati Kuu ijuzulu kwanza!

Acha ujinga wako... Kama hao watu kuja CDM ni tatizo je, unataka kutuambia kuwa wakirudi/wakibaki ccm wanabadilika kuwa malaika??
Acheni mauza uza yenu... Kwa akili kama hizi mnazidi kuwapotosha Watanzania wenye elimu duni!!
 
Hahaaaaa mnalo. Kinyesi kimeshakauka wala hakina harufu Kwa sasa yote imebaki kwenye Nguo zenu fuuuuuuuuuu
 
Maelezo yako kuwa CHADEMA kimuundo ni sawa na CCM, unaweza kuwa sahihi lakini kusema kwamba mapenzi yangu kwa CHADEMA yananifanya niwe kipofu, hupo sahihi.

Sijasema kuwa CHADEMA kimuundo au kifalsafa ni tofauti sana na CCM lakini nimesema kuna umuhimu mkubwa kuwa na upinzani imara.

Faida ya kuwa na upinzani imara ni kwamba wananchi wanakuwa na uwezo wa kukiadhibu chama na watawala wanapotenda kinyume na ahadi zao au wanapofanya makosa makubwa kama kukiuka sheria na katiba.

Lakini pia upinzani huwapa watu ujasiri wa maamuzi na maoni wakijua kuwa hata wakionewa na vyama vyao vya mwanzo, wana uwezo wa kujiunga na chama kingine na kuendelea kupigania wanachokiamini.

Mpaka sasa siamini kuwa CCM ina sera mbaya, na wala siamini kama CHADEMA au chama kingine chochote kitakuja na sera tofauti kabisa. Tofauti kubwa ipo kwenye utekelezaji.

Kwa sasa tatizo kubwa la CCM ni kutaka wananchi wote kuwa wafungwa wa fikra za Rais na CCM. Huku ni kuwadumaza watu. Wanataka tusione faida ya kuwa wengi.

Tatizo kubwa la pili la CCM ni kutenda mambo mengi kinyume na katiba na sheria za nchi. Kwenye hili ni CHADEMA ndiyo kila mara imesimama imara kukemea bila woga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…