imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Sitishiwi Nyau.Sawa, kuwa makini usije kujikuta kwenye pipa la taka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sitishiwi Nyau.Sawa, kuwa makini usije kujikuta kwenye pipa la taka
Ni KweliUkisoma kilicho andikwa ni wazi chadema hawako tayari kwa mdaharo maana wameweka masharti ambayo wanajua hayatawezekana
Safi sana, Huu mdahalo moderator wawe wakili Peter kibatala na wakili Pascal Mayalla, ufanyike nkrumah hall
Baada ya tamko la Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kuhusu maazimio ya Kamati Kuu ya
Imetolewa leo Jumatatu tarehe 15 Januari, 2024.
Pia soma: Video: Makonda ataka mdahalo na Tundu Lissu
Ana wataalamu kama chama tawala watampatia taarifa zote na uzuri kwa kuwa anamudu kujieleza atawararua tu hao jamaaDogo Makonda anafikiri kila kitu kinataka porojo tu na bla bla! Anafikiri kufanya mdahalo ni sawa na kupiga vijembe!!
Mkuu aliyeita mdahalo alipaswa kuweka wazi rules of engagement, kosa la kwanza hakuweka! Wenzie wamekubali mdahalo naye kama alivyomba but with their stipulated rules of engagement! Nafikiri hicho ndicho ulichokosa kuona!Umeona nilichoona mimi.
Mkuu Makonda (the party's mouth piece) missed that opportunity, hawezi kuweka masharti yoyote kwa kwa sasa sababu yupo engaged tayari na aliowaalika mdahaloni, Chadema!..Ccm nao watoe masharti tuone nani muoga.
..kwenye mdahalo wowote washiriki hutoa mapendekezo / masharti namna gani mdahalo ufanyike.
..Chadema hawezi kukimbia nafasi ya kuonekana ktk vyombo vya habari.
Mkuu hapana, Makonda alipaswa kuweka masharti yake, he missed that! Chadema has engaged him with such! Down don't turn the tables with crocodile tears!CCM wamesema mdaharo ufanyike siku ya tarehe 24-25😂😂😂😂😂
Shida ni kwamba Chadema wamekataa mdaharo kwa kuweka masharti….
Chadema kwa nini huwa hamsikii hamjifunzi.
Huyu wa kuwafanya muandike barua ndeeefu
Mkiwaaikiliza wananchi
Msiende
Maji mmeyavulia nguo kwa nini mnakuwa waoga kuyaoga
Kesho UWT wakiwaita kwa mdahalo mtaenda?
Huyu huyu mwenye kesi lukuki mnamtuhumu mnaenda kuketi naye meza moja!
Hii ni mistake kubwa mnafanya
Angewaita Mkuu wa nchi labda huyu huyu bashite mkae muongee nini mbona hamjifunzi ninyi watu
FOCUS
Mkuu Faiza acha unafiki, Makonda aweke masharti ya kufanya mdahalo unaona sawa ila wenzie wamejibu kwa kuweka masharti ya kufanya mdhhalo naye unaona nongwa!Wanaweza mdahalo wameambiwa wajichaguwe mpaka wa tano au hata wakipenda zaidi. Makonda kawaambia atakuwa peke yake, wachaguwe venue na waandishi wao wanaowapenda.
Sasa kuna nini zaidi hapo? Masharti ya nini? Open dia;og, wajikusanye wote.
Makonda kishaelewa hao hawana hoja ni fujo tu, na nnaaaini atawagaragaza hoja zao wote kwa pamoja.
Mimi na challenge chadema wote mje hapa tulumbane. Muwe hata 1000 na mimi peke yangu hapa JF, naanza:
Chadema hamna hoja na wabakaji wa hoja, sera zenu kama chama ni zipi?
Midogo midogo ya jf aliikimbia itakua hii ya kiumeni ataiweza shost yenu?Wanaweza mdahalo wameambiwa wajichaguwe mpaka wa tano au hata wakipenda zaidi. Makonda kawaambia atakuwa peke yake, wachaguwe venue na waandishi wao wanaowapenda.
Sasa kuna nini zaidi hapo? Masharti ya nini? Open dia;og, wajikusanye wote.
Makonda kishaelewa hao hawana hoja ni fujo tu, na nnaaaini atawagaragaza hoja zao wote kwa pamoja.
Mimi na challenge chadema wote mje hapa tulumbane. Muwe hata 1000 na mimi peke yangu hapa JF, naanza:
Chadema hamna hoja na wabakaji wa hoja, sera zenu kama chama ni zipi?
Hayo yote mbona na kazi ya Bunge? Ugumu wa maisha anaulizwa Waziri wa Kilimo na Gavana wa Benki kuu, siyo blogu ya fatmakarume. Kama unataka kuruhusu mgombea binafsi ili tutawaliwe na petrodollars hilo si wazo la Watanzania wote ni lako wewe mmoja. Ila ni rukhsa kutushawishi weka mada hiyo kwenye Ilani ya 2025 tutaona. Kama hutaki Rais achague tume ni nani ataichagua? Kwa ruhusa ya nani? Rais ana kura za Watanzania ndizo zinazompa madaraka, wewe ni nani unachukia? Si ndiyo tundulissu aliyeshindwa 87%/13% sasa unataka watu waandamane kusapoti 13%?
Baada ya tamko la Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kuhusu maazimio ya Kamati Kuu ya Chama kuitisha maandamano ya amani tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Dar Es salaam, ameibuka Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi na kutoa kauli potofu dhidi ya Maazimio ya Kamati Kuu.
Ikumbukwe kwamba Maandamano hayo ni sehemu ya vuguvugu la kudai haki nchini, ikiwa na madai ya kuitaka Serikali kuondoa miswada mibovu mitatu Bungeni, kuanzisha mchakato wa mabadiliko madogo ya Katiba ya Mwaka 1977 (minimum reforms), kupunguza ugumu wa maisha na kusikiliza na kuheshimu maoni ya wananchi.
Tumesikia kauli ya ya Katibu wa Uenezi wa CCM akitoa rai kuwa anaomba ufanyike mdahalo baina ya viongozi wa Chadema na 'yeye binafsi.
Msimamo wa Chama ni kuwa kama anataka mdahalo sisi kama Chama tupo tayari na hatujawahi kukimbia midahalo kama wao na Chama chao, Hivyo basi mdahalo unaweza kufanyika katika masuala yafuatayo ambayo tumeweka msimamo wetu wazi ili yatekelezwe na Serikali;
1. Serikali iondoe kwanza miswada mitatu mibovu Bungeni; ili kuwezesha wadau mbalimbali tukae kwenye mdahalo wa kujadili maudhui ya Miswada ya Sheria za Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi na Sheria zinazohusu masuala ya Vyama vya Siasa.
2. Serikali ianzishe mara moja mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Mwaka 1977 (Minimum reforms) ili kuwezesha kuondoa mapungufu yaliyopo kwenye Katiba hiyo ili kuruhusu maandalizi ya kuandikwa Kwa miswada mipya ya kuboresha mifumo ya chaguzi nchini.
3. Serikali iwasilishe Bungeni muswada wa Sheria ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi huo usimamiwe na Tume ya Uchaguzi badala ya TAMISEMI.
4. Serikali iwasilishe Bungeni muswada wa Sheria wa kukwamua mchakato wa Katiba Mpya ukiwa na mwelekeo (Road Map)wa lini nchi itapata Katiba Mpya.
5. Wadau tutaweza kukaa kwenye mdahalo ili kuishauri Serikali jinsi ya kuweza kupunguza ukali wa gharama za maisha na kuonyesha Kodi na tozo zipi zipunguzwe, anasa gani ziondolewe Serikalini, na mkakati mima wa kupunguza ukali wa gharama za maisha kwa wananchi.
Aidha, tunamkumbusha Mwenezi wa CCM kuwa Miswada hii imepelekwa Bungeni na Serikali na imepuuza maoni ya wananchi, Viongozi wa dini, Wadau na vyama vya siasa, ripoti za waangalizi wa Uchaguzi wa kimataifa na ndani, Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 pamoja na amri za Mahakama ya Afrika na Afrika Mashariki kuhusu maeneo mahususi ya kuboresha mifumo ya chaguzi na Sheria ya Vyama.
Hivyo basi katika kipindi hiki aweke mdahalo na Serikali ili waone ulazima wa kusikiliza na kuheshmu maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa chaguzi katika kuandaa mazingira
Bora ya kuwa na chaguzi huru na haki nchini.
Katika kipindi hiki Chama kinaendelea na maandalizi ya maandamano ya amani yatakayofanyika Jijini Dar Es salaam tarehe 24 Januari, 2024.
Imetolewa leo Jumatatu tarehe 15 Januari, 2024.
Pia soma: Video: Makonda ataka mdahalo na Tundu Lissu
Masharti mengi sana. Wangekubali mdahalo tu, wampeleke Lissu...kawa-beep na wao wamempigia.
..mdahalo ni nafasi ya wao kueleza sera zao kwa umma.
..usifikiri mwenyekiti wa kamati ya bunge na Spika walikuwa wajinga kuwauzia Chadema wasiwasilishe hoja zao kule bungeni.
..Mfano mdogo, Makonda atakuja na hoja gani kushawishi kuwa Wakurugenzi ambao ni makada wa Ccm watasimamia uchaguzi kwa haki?
..haya mambo yakifanyika kwa uwazi Ccm haiwezi kushinda.
Humu ni kwasisi tusiokuwa na kazi maalum. Mwenye kazi zake za majukumu afate nini humu kila siku?Midahalo
Midogo midogo ya jf aliikimbia itakua hii ya kiumeni ataiweza shost yenu?
Wewe ndio huna kazi wenzako tanazo kazi za kutuingizia kipatoHumu ni kwasisi tusiokuwa na kazi maalum. Mwenye kazi zake za majukumu afate nini humu kila siku?
Ni kweli msingi wa uimara wa CHADEMA umejengwa katika nguvu za hoja kupitia midahalo na ushawishi katika mambo ya msingi, lakini je kauli ya kebeli za Mwenezi wa CCM zinaonesha u seriousness wa kuwa na platform za kujadili maswala hayo tena kwa kusema anawataka Mh. Mbowe, Mh. Lissu na Mh. Mnyika na yeye peke yake atakiwakilisha chama chake?..midahalo ni PLATFORM ambayo Chadema wanaihitaji kuwasilisha hoja zao kwa wananchi.
..kama utakuwa ume-observe Chadema huwa wanabinywa kutoa maoni yao ktk makongamano mbalimbali yanayoandaliwa na serikali.
..sasa kama Makonda anataka kuwapa jukwaa la one-on-one na Chadema ambapo watakuwa na nafasi ya kuongea nadhani ni jambo jema kwa Chadema.
Ni kweli msingi wa uimara wa CHADEMA umejengwa katika nguvu za hoja kupitia midahalo na ushawishi katika mambo ya msingi, lakini je kauli ya kebeli za Mwenezi wa CCM zinaonesha u seriousness wa kuwa na platform za kujadili maswala hayo tena kwa kusema anawataka Mh. Mbowe, Mh. Lissu na Mh. Mnyika na yeye peke yake atakiwakilisha chama chake?
Lakini kama ni kweli CHADEMA hubinywa kutoa maoni katika makongamano yaliyoandaliwa na serikali je ni kweli hawatabinywa katika kongamano hili lililo kuwa innitiated na mwenezi wa Chama Tawala?
Kwa muda mrefu sasa tumeona ni jinsi gani chama kinakimbia midahalo si tu ya wakati wa kampeni za chaguzi mbalimbali kwa kuwazuia makada na wagombea wake, bali pia hata mijadala ya kikatiba ya ndani ya bunge inahaririwa kwanza kabla ya kurushwa hewani, leo cham hiki hiki kikubali kuwa na mijadala na midahalo mizito juu ya uhitaji wa Katiba mpya na marekebisho ya sheria ya Tume ya Uchaguzi?
Mh. Makonda hapa kawaini wapinzani wake. Amewatoa katika kujadili hoja na maandamano kwenda kwenye midahalo ambayo haitafanyika!
Tukubali hata kama haitupendezi wapenda demokrasia kwamba amefanikiwa kuua mjadala kutoka Maandamano hadi kwenye kuomba venue ya mjadala na CHADEMA..Makonda hajamtoa mtu yeyote ktk kujadili au kutamani Tume Huru au Katiba Mpya.