Pre GE2025 CHADEMA yakubali kufanya mdahalo na CCM kwa masharti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Dogo Makonda anafikiri kila kitu kinataka porojo tu na bla bla! Anafikiri kufanya mdahalo ni sawa na kupiga vijembe!!
Ana wataalamu kama chama tawala watampatia taarifa zote na uzuri kwa kuwa anamudu kujieleza atawararua tu hao jamaa
 
Umeona nilichoona mimi.
Mkuu aliyeita mdahalo alipaswa kuweka wazi rules of engagement, kosa la kwanza hakuweka! Wenzie wamekubali mdahalo naye kama alivyomba but with their stipulated rules of engagement! Nafikiri hicho ndicho ulichokosa kuona!
 
..Ccm nao watoe masharti tuone nani muoga.

..kwenye mdahalo wowote washiriki hutoa mapendekezo / masharti namna gani mdahalo ufanyike.

..Chadema hawezi kukimbia nafasi ya kuonekana ktk vyombo vya habari.
Mkuu Makonda (the party's mouth piece) missed that opportunity, hawezi kuweka masharti yoyote kwa kwa sasa sababu yupo engaged tayari na aliowaalika mdahaloni, Chadema!

Mdahalo umeshaisha kabla haujaanza, na Chadema wameshaondoka na point 3 kibindoni mapema!

Ukisikia makonda ana cheti feki usifikiri kasingiziwa, ni kweli anacho!
 
CCM wamesema mdaharo ufanyike siku ya tarehe 24-25😂😂😂😂😂
Shida ni kwamba Chadema wamekataa mdaharo kwa kuweka masharti….
Mkuu hapana, Makonda alipaswa kuweka masharti yake, he missed that! Chadema has engaged him with such! Down don't turn the tables with crocodile tears!
 
Chadema wabakaji wa hoja, hawana hoja zao wala sera zao.

Wameshaambiwa tarehe hiyo ni ya majeshi yetu kufanya usagfi. Sasa wao waende kama hawajakuwa ndiyo uchafu wenyewe.

Chadema huwa wanapenda sana waonekane wanaonewa, nadhani ndiyo pesa za kutokea ujerumani zinapokuja kwa wingi.
 
Wanaweza mdahalo wameambiwa wajichaguwe mpaka wa tano au hata wakipenda zaidi. Makonda kawaambia atakuwa peke yake, wachaguwe venue na waandishi wao wanaowapenda.

Sasa kuna nini zaidi hapo? Masharti ya nini? Open dia;og, wajikusanye wote.

Makonda kishaelewa hao hawana hoja ni fujo tu, na nnaaaini atawagaragaza hoja zao wote kwa pamoja.

Mimi na challenge chadema wote mje hapa tulumbane. Muwe hata 1000 na mimi peke yangu hapa JF, naanza:

Chadema hamna hoja na wabakaji wa hoja, sera zenu kama chama ni zipi?
 
Chadema ondoeni hayo mashart ya kuindoa miswada nendeni kwenye mdahalo mtueleze yana manufaa gani kwa mtanzania hayo mnayoyasema ili tiwavute wengi ikiwezekana hata malonda aje chafema pamoja chimbi katibu ccm
 

Mkuu Faiza acha unafiki, Makonda aweke masharti ya kufanya mdahalo unaona sawa ila wenzie wamejibu kwa kuweka masharti ya kufanya mdhhalo naye unaona nongwa!

Ama kweli kunya anye Kuku akinya Bata matata!

Mkuu toa mfano mmoja tu ambapo Chadema waliwahi kuanzisha fujo.

Mkuu kuna kumbukumbu na ushahidi wa Makonda kumfanyia Mzee Warioba fujo, na hata kumlamba vibao!

Hili nalo umelisahau! Acha unafiki!
 
Midahalo
Midogo midogo ya jf aliikimbia itakua hii ya kiumeni ataiweza shost yenu?
 
Hayo yote mbona na kazi ya Bunge? Ugumu wa maisha anaulizwa Waziri wa Kilimo na Gavana wa Benki kuu, siyo blogu ya fatmakarume. Kama unataka kuruhusu mgombea binafsi ili tutawaliwe na petrodollars hilo si wazo la Watanzania wote ni lako wewe mmoja. Ila ni rukhsa kutushawishi weka mada hiyo kwenye Ilani ya 2025 tutaona. Kama hutaki Rais achague tume ni nani ataichagua? Kwa ruhusa ya nani? Rais ana kura za Watanzania ndizo zinazompa madaraka, wewe ni nani unachukia? Si ndiyo tundulissu aliyeshindwa 87%/13% sasa unataka watu waandamane kusapoti 13%?
 
Masharti mengi sana. Wangekubali mdahalo tu, wampeleke Lissu.
 
Ni kweli msingi wa uimara wa CHADEMA umejengwa katika nguvu za hoja kupitia midahalo na ushawishi katika mambo ya msingi, lakini je kauli ya kebeli za Mwenezi wa CCM zinaonesha u seriousness wa kuwa na platform za kujadili maswala hayo tena kwa kusema anawataka Mh. Mbowe, Mh. Lissu na Mh. Mnyika na yeye peke yake atakiwakilisha chama chake?

Lakini kama ni kweli CHADEMA hubinywa kutoa maoni katika makongamano yaliyoandaliwa na serikali je ni kweli hawatabinywa katika kongamano hili lililo kuwa innitiated na mwenezi wa Chama Tawala?

Kwa muda mrefu sasa tumeona ni jinsi gani chama kinakimbia midahalo si tu ya wakati wa kampeni za chaguzi mbalimbali kwa kuwazuia makada na wagombea wake, bali pia hata mijadala ya kikatiba ya ndani ya bunge inahaririwa kwanza kabla ya kurushwa hewani, leo cham hiki hiki kikubali kuwa na mijadala na midahalo mizito juu ya uhitaji wa Katiba mpya na marekebisho ya sheria ya Tume ya Uchaguzi?
Mh. Makonda hapa kawaini wapinzani wake. Amewatoa katika kujadili hoja na maandamano kwenda kwenye midahalo ambayo haitafanyika!
 

..Makonda hajamtoa mtu yeyote ktk kujadili au kutamani Tume Huru au Katiba Mpya.
 
..Makonda hajamtoa mtu yeyote ktk kujadili au kutamani Tume Huru au Katiba Mpya.
Tukubali hata kama haitupendezi wapenda demokrasia kwamba amefanikiwa kuua mjadala kutoka Maandamano hadi kwenye kuomba venue ya mjadala na CHADEMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…