- Source #1
- View Source #1
Wanabodi leo nimekutana na hii taarifa kuwa imepostiwa na BBC kwamba CHADEMA wameomba maridhiano ya kisiasa ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu. Je, ni kweli?
- Tunachokijua
- John John Mnyika ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye mbali na nafasi hiyo, pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Ubungo, mwaka 2010-2015, na mwaka 2015 - 2020 alikuwa mbunge wa jimbo la Kibamba.
Mnamo mwezi Aprili 12, 2025 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Mnyika alichapisha taarifa ya kutokuhudhuria kikao cha kushauriana na kusaini maadili ya uchaguzi ya 2025, ambapo makamu mwenyekiti wa chama hicho John Heche pia aliongezea nguvu katika ujumbe huo kuwa "Chama chetu hakitashiriki kusaini maadili ya tume isiyo na maadili."
Madai
Kumekuwapo na taarifa inayodaiwa kuchapishwa na BBC Swahili ikirejelea chapisho lilnaloonekana kuwa la John Mnyika kupitia mtandao wa X kuwa CHADEMA wameandika barua kuomba kukutana na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi ili kujadili kuhusu uamuzi wao wa kushiriki uchaguzi mkuu.
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) umebaini taarifa hiyo haijachapishwa na BBC Swahili wala John Mnyika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X.
Aidha chapisho hilo ni la kutengenezwa kwani limebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo muundo wa chapisho unatofautiana na muundo rasmi wa machapisho ya BBC Swahili, mapungufu katika sehemu ya kichwa cha habari ambapo inaonesha kuna maneno awali yalifutwa kisha kuandika maneno mengine. Ubora mdogo wa chapisho hilo tofauti na machapisho rasmi ya chombo hicho.