Elections 2010 CHADEMA Yapeta Mpanda mjini; Yarudisha majimbo yake yote except 1!!


Ninaomba mtu anikumbushe majina ya majimbo yote ambako uchaguzi ulifanyika leo.
 
Hivi kumbe uchaguzi bado unaendelea? Dah asante mkuu:nono:
 
Jamani,

Mnakumbuka nimepiga kelele sana kwamba uzembe wetu ilikuwa ni kuacha Tume ijumlishe kura za kituo kwa kituo wakati na sisi tunajua hesabu hiyo ndogo.

Wa Ndima katuletea matokeo ya vituo na mimi nimeyapanga ndani ya worksheet hii ambayo tuliileta tuitume kwenye uchaguzi mkuu uliochakachuliwa.

Mwanajamvi Wa Ndima, vituo ulivyotutajia kura zake hapo juu vituo juu nimeviweka na viko 19 na inaonyesha kwamba CHADEMA wanaongoza kwa 1,574 wakati CCM wanazo 1,110.

Ambayo ni kwamba CHADEMA wanaongoza kwa asilimia 58.64 na CCM wana asilimia 41.36.

Kama jumla ya vituo ni 28 basi tuleteeni matokeo ya vilivyobaki tisa tuwaonyeshe kuwa tuko mbele kiteknology na hatuwasubiri watujumlishie.

Kama kuna majimbo mengine leteni pia tuyajumlishe.

Fungueni sheet hii niliyo-attch humu muone uhondo wa kujijulishia wenyewe.

Hi ni rasharasha. Mwaka 2015 hii sheet inabidi iatwanywe kwa watanzania wote ifikapo February 2015 na ijadiliwe ili kil ammoja mwaka ule ajue kila mtanzania anahitaji kujijumlishia mwenyewe na kazi yake itakuwa ni kut-type tu kwenye komputer na kuingiza jina la kituo na idadi ya kura.
 

Attachments

Matokeo wameshahesabu mara mbili, wana,alizia mara ya tatu chadema a aongoza kwa kura 150 zaidi tu. Lisiingizwe sanduku feki angalieni wana mageuzi


kwa nini warudie mara tatu? hawaamini kama wamepigwa chini?

jimbo letu jingine hilo tushahesabu
 
Safi safi sana chadema, umaliziaji mzuri ebu tupeni mbunge wa 46
 

Asante sana "Nikupateje"...Hivyo ndio ilivyotakiwa kufanya katika kuhesabu kura za awali,maana Tume nao huja na hesabu zao za Uongo.Nakumbuka RO Geita alimtangaza Slaa mshindi kwa kura 22,000+ lakini Bwana Makame na NEC yake wakatangaza kuwa Dr.Slaa ameshinda kwa kura 3,700+ sasa unajiuliza wamepeleka wapi jumla ya kura 17,000 unashindwa kugundua.
Ni kura ulizoziorodhesha hapo ni wazi Mzee Said Amour Arfi anarudi Bungeni kuwawakilisha Wanachi wa Mpanda Mjini.
 

Safi sana, hii inafaa kutumiwa na kila mtu mwaka 2015
 
Taarifa nilizozipokea sasa hivi kutoka kwa Mhe Zitto aliyepo huko Mpanda Mjini ni kwamba CHADEMA wameshinda kwa tofauti ya kura 607 kwa majumuisho ya kura kutoka katika vituo. Kinachosubiriwa ni msimamizi kutangaza matokeo na kwa uzoefu kutoka uchaguzi uliopita hapo ndipo songombingo ilipo!
 

Safi sana, tusubiri tuone watakavyotangazo ilhali matokeo tunayo vibindoni
 
Asante sana.

Pasco. tuko interested kuona ni nini itakuwa outcome ya analysis yako uliyoitoa. Bado tunaikumbuka. Tukumbushane hapa chini:

 
kama bado vituo 9 tu mbona idadi ya watu ni dogo sana je ni kweli vituo viko 28 tu?
 


Kitila, tunashauri Ulinzi wa Kura kama ilivyofanyika Mwanza, Mbeya, Arusha, Kawe, Ubungo na Iringa.

Ikiwezekana Makamanda wakuu wa CHADEMA waende huko.

Ikumbukwe kuwa CHADEMA ikishinda na viti maalumu vitaongezeka kama niliwasikia Vema NEC.
 

mgombea wa chadema said amur arfi ameshinda na amemzidi mgombea wa ccm kwa kura 67 tu,na ameshatangazwa na tume na mpanda yote imelipuka kwa shangwe,niko mitaani hapa mjini mpanda ni shangwe na nderemo.
 
mgombea wa chadema said amur arfi ameshinda na amemzidi mgombea wa ccm kwa kura 67 tu,na ameshatangazwa na tume na mpanda yote imelipuka kwa shangwe,niko mitaani hapa mjini mpanda ni shangwe na nderemo.

Mwera hizo ni habari njema sana.

Na mimi napata kikombe cha kahawa hapa huku shemeji yenu akinichezea "Yori Yori"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…