Bishweko
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 4,985
- 3,493
CHADEMA madai ya kuwepo mabadiliko katika mfumo mzima wa dola ya Tanzania yanaanza kuonekana kwa ushndi mmoja na kufuatiwa na mengine mengi hadi kieleweke
LEO MAHAKAMANI 22 OCTOBER 2026 CHADEMA YAIBUKA NA USHINDI
View: https://m.youtube.com/watch?v=96G94pRcRRI
CHADEMA imeshinda shauri la kisheria leo tarehe 22 Oktoba 2026 dhidi ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohammed.
Katika uamuzi uliotolewa na Jaji Awamu Mbagwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania (Masjala Ndogo ya Dar es Salaam), mahakama imetupilia mbali maombi ya kutaka chama hicho kizuiwe kufanya shughuli zake za kisiasa.
Yaliyojiri Mahakamani Leo:
Uamuzi wa Jaji: Jaji Mbagwa ameeleza kuwa mahakama kuu ya Tanzania haioni sababu za msingi za kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA kwa ajili ya kesi hiyo ya madai.
Kuhusu Kesi Hiyo
: Shauri hili (Kesi ya Madai Na. 13832 ya mwaka 2026) lilifunguliwa na Said Issa Mohammed akishirikiana na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu, John Mnyika. Walikuwa wakiomba amri ya kukizuia chama kufanya shughuli za kisiasa na kutumia mali zake hadi kesi ya msingi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar itakapomalizika.
Historia ya Kesi: Huu ni mwendelezo wa mapambano ya kisheria ambapo awali, mnamo tarehe 28 Mei 2026, Mahakama Kuu ilitupilia mbali kesi nyingine kama hiyo iliyofunguliwa na Said Issa kutokana na kasoro za kisheria kabla ya yeye kuirejesha tena mahakamani. (Kumbuka: Said Issa Mohammed alishafukuzwa uanachama wa CHADEMA mnamo tarehe 6 Juni 2026 kutokana na hatua yake ya kukishtaki chama mahakamani
View: https://m.youtube.com/watch?v=mLmHrHBI3pM
Mahakama imezima simu ili isipokee maelekezo kutoka juu nini?