CHADEMA Yasogeza Mbele Kikao cha Baraza Kuu, Viongozi Kushiriki Kesi ya Mwenyekiti wao Lissu

CHADEMA Yasogeza Mbele Kikao cha Baraza Kuu, Viongozi Kushiriki Kesi ya Mwenyekiti wao Lissu

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeazimia kusogeza mbele kikao cha Baraza Kuu la chama hicho hadi tarehe nyingine, ili kutoa nafasi kwa viongozi wakuu wa Chama kushiriki kikamilifu katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama hicho Amani Golugwa, amesema uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 29, 2026, katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wajumbe wamejadili maandalizi ya Baraza Kuu na mwenendo wa kesi hiyo.

Kabla ya kuahirishwa kwa kikao hicho leo, kilitarajiwa kufanyika Septemba 15, 2026, ambapo tarehe ya kufanyika tena haijatajwa. Golugwa kupitia taarifa yake amesema itapangwa. Kuhusu kesi ya uhaini, Kamati Kuu imewaelekeza viongozi wakuu wa chama kuelekeza nguvu katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato wa kesi hiyo

Soma Pia: Kikao maalum cha Kamati Kuu ya CHADEMA kufanyika Agosti 29, 2026

 
Hii ndio Demokrasia ya mweusi kwake kwanza kuogopa mkate wake usimponyoke‼️ kisha ndio Demokrasia yako ❗️

Vyama vingi nisawa na mtoto njiti kwa Africa ✍️
 
Cdm mfanye mfumo kama wa Iran, mnakuwa na replacement tayari, halafu muwe mnashambulia kila kona sio kila siku Heche pekee yake anajibu kila mtu hadi hakina manara.

Kipindi hiki kutoa elimu kwa watanganyika kila kona sio kusubiria ccm wamesema nini ndio mnajitokeza, mpeane majukumu kusipoe hata kama mnampambania mwenyekiti wenu.
 
Hii ndio Demokrasia ya mweusi kwake kwanza kuogopa mkate wake usimponyoke‼️ kisha ndio Demokrasia yako ❗️

Vyama vingi nisawa na mtoto njiti kwa Africa ✍️
Kwani mritalajia kufanya Nini kwenye lile Baraza kuu la CHADEMA naona Kama Kuna Jambo CCM mlikua mmelipanga Ila limepalaganyika ghafula hebu funguka kidogo comredi kipepe.
 
Cdm mfanye mfumo kama wa Iran, mnakuwa na replacement tayari, halafu muwe mnashambulia kila kona sio kila siku Heche pekee yake anajibu kila mtu hadi hakina manara.

Kipindi hiki kutoa elimu kwa watanganyika kila kona sio kusubiria ccm wamesema nini ndio mnajitokeza, mpeane majukumu kusipoe hata kama mnampambania mwenyekiti wenu.
Good idea
 
Back
Top Bottom