Uchaguzi 2020 CHADEMA yatangaza kusudio la kuweka Mgombea Urais wa Zanzibar

Uchaguzi 2020 CHADEMA yatangaza kusudio la kuweka Mgombea Urais wa Zanzibar

CDM wangewachia huko ACT tu
Maana ACT kidogo Ana nguvu huko
CDM akiweka mgombea watawapunguzia kura ACT

ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Iko hivi , kila chama kitateua mtu na kumleta mezani ili ajadiliwe na vyama vyote , kingine ambacho umekisahau ni kwamba maharamia wa ccm walipanga njama za kumzuia Maalim Kugombea ili kuepuka aibu ya kipigo , wamepanga njama chafu nyingi sana kwa vile hawana ushawishi
 
Wasisahau kuwa sas hivi tume ipo chini ya TISS- uvccm ambao wote ni chato die hard. Mwaka huu atakayetoboa ujue ni kidume. Magu atakuwa anagaw majimbo kama karanga. Na wakishajazana bungeni watakuambia chaguo la Mungu libadilishiwe katiba.
Hi ndo plan ya Magu ..kuwapa majimbo machache nccr na cuf halafu badae wapeleke azimio la kuondoa ukomo wa urais ili Magu atawale atakavyotaka...
 
... halafu badae wapeleke azimio la kuondoa ukomo wa urais ili Magu atawale atakavyotaka...
which is healthy for the nations' democracy. kwanini wananchi wawekewe vikwazo kuchagua kiongozi wanayemtaka?!
 
Hiyo ni hatua ya pili. Kwanza kila chama kinatangaza uwezo wake kisha wanaungana.
Hii ni tofauti na TLP eti inamtangaza mgombea was CCM kuwa mgombea wao wakati CCM wenyewe hawajamtangaza. Watu wazima wapumbaf ndio hao.
Yeah nimekusudia hio hatua ya 2, kivyovyote vile kuungana kunahitajika ingawaje kuna watu ambao watarumiwa kuvuruga muunganiko
 
Chadema wajinga CUF iliamua kuungana na chadema sababu CUF walikuwa na nguvu Sana Zanzibar lakini Tanzania bara hawakuwa ma nguvu wakasacrifice Duni Haji ajiunge chadema ili chadema iwe na nguvu Zanzibar na CUf iwe na nguvu bara

Matokeo Baada ya chadema kupata wabunge wengi kikaota ndevu na kuanza dharau kwa waliowafikisha Hapo walipo akiwemo Lowasa na Seif na Duni Haji hawakujua kuwa muungano wa Lowasa na Seif sharriff Hamd ulikuwa muungano wa the CCM frustrated people .Seif alitimuliwa CCM Na Lowasa akapigwa chimi CCM kugombea uraisi mmoja akawa Chadema Lowasa the fristrated akaungana na the frustrated mwingine wa CUF maslim.Seif kuunga alliance ya kuipiga chini CCM ambayo wanahisi iliwafrustarate ndoto zao hewa wakitumia UKAWA Kama fimbo!!!

Kilichotokea walikuwa fustrated more kupindukia kwenye uchaguzi mkuu na ndani ya vyama walivyokuwa vya CUF na Chadema!!
Seif na Duni Haji na wafuasi wao wakatimka alliance ya chadema na kukimbilia ACT wazalendo kwa Zitto Kabwe ambaye alitimuliwa na chadema !!!

Sahau ACT wazalendo kuungana na chadema sababu wote mliwaumiza Chadema kuanzia Zitto Kabwe ,Duni Haji nk pambaneni na hali zenu . Chadema Wana short sighted leaders !!! Safari hii mtatupwa nje.Nobody wants to join you matapeli nyie wa kisiasa
Mjambaji tu ww huna Lolote
 
Hakika. Umeona mbali sana.wameamua kuwatisha ACT.
Zitto atakuwa bwege akikubali muungano huo wakitapeli
Wakitapeli vipi mkuu, huo ndio ukweli, mm kwa mawazo yangu anaepinga muungano huu kivyovyote ni CCM coz anajua kuwa nguvu yote itakua inamuelekea yeye
 

Taarifa hii imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho upande wa Zanzibar Mh. Salum Mwalimu Mjini Zanzibar alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari.

=====

TAMKO LA KUTANGAZA NIA KUWANIA NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatangaza kusudio la kusimamisha mgombea katika nafasi ya Rais wa Zanzibar katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu na hivyo inafungua milango kwa wanachama wake wenye sifa kutangaza nia.

Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kutangaza rasmi kuweka mgombea katika nafasi hiyo ya juu ya nchi kwa upande wa Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalim ametoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika leo Jumamosi June 06, 2020 katika Ofisi Kuu ya Chadema , Kisiwandui Zanzibar.

“Tunawatangazia rasmi wanachama wetu wenye sifa na ambao wana nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar waandike kwa Katibu Mkuu wa chama na kuwasilisha barua hizo ofisi ya Makao Makuu Zanzibar wakati wowote kuanzia leo hadi Juni 15, 2020 Saa Kumi na Nusu Alasiri”

“Chama kimejipima na kutafakari kwa kina na kimeona kwamba sasa ni wakati mufaka kuwapa nafasi wanachama wake wenye ndoto na uwezo wa kugombea nafasi hiyo kutimiza ndoto zao”

Kwa sasa ni kutanga nia zao kwa chama na kwamba baada ya hapo utafuata mchakato wa uchukuaji wa Fomu za ndani ya chama ambapo maelekezo yake pamoja na utaratibu mzima utakaofuata utatolewa baadae. Kwa watakaowasilisha taarifa zao wataruhusiwa kutangaza kusudio lao hilo kwa Umma kupitia vyombo vya habari.

Chama kinawahimiza wanachama wote wenye Sifa, Vigezo na Maadili kama ilivyoanishwa kwenye Kanuni za chama Sura ya Kumi (10) katika Katiba ya Chama ya Mwaka 2006 Toleo la 2016 na matakwa ya Katiba ya Zanzibar kujitokeza.
”Niwatake wanachama wetu wote kufuguliwa kwa mlango huu usiwe chanzo cha kuvuruga umoja na mshikamano ambao umekuwa thabiti ndani ya chama chetu Zanzibar.”

Pamoja na tangazo hili, chama chetu kipo tayari kuendeleza ushirikiano na vyama na kulinda nia na shabaha ya ushirikiano huo bila kuathiri malengo ya vyama vyetu kwa masilahi ya kila M-Zanzibari katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Aidha, tunaendelea kuwasisitiza wanachama wetu walioonesha nia ya kugombea nafasi za Udiwani, Uwakilishi na Ubunge kwa Unguja na Pemba kuendelea na taratibu za chama na kwamba milango bado ipo wazi kwa ambao bado hawajafanya hivyo.

Chama kinawatakia kheri wanachama wake, pamoja na wafuasi na wapenzi na kwa pamoja tunawataka kuendelea kujipanga kukiletea chama ushindi katika uchuguzi Mkuu wa Oktoba .

Imetolewa na:
Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar
Kwa taarifa hii hapa, CHADEMA wasafishe nyumba yao mapema kabla hata ya kuteua wagombea kwa sababu wakati wa kampeni nguvu kubwa itapaswa kutumika kumsafisha Mbowe, M/Kiti wa chama, ambaye ndiye hubeba sura ya chama.

 
Wakitapeli vipi mkuu, huo ndio ukweli, mm kwa mawazo yangu anaepinga muungano huu kivyovyote ni CCM coz anajua kuwa nguvu yote itakua inamuelekea yeye
Cdm si wakweli. Wanapenda kuwatumia wengine tuu. Pitia humu nyuzi zipo nyingi wakiwakejeli vyama wenza wa ukawa kwamba wao ndio wamewabeba.
Muungano wa kweli labda ACT na Nccr mageuzi
 
Back
Top Bottom