CHADEMA yaweka pingamizi dhidi ya akina Mdee kuendelea kuwa wabunge wakati kesi ya msingi ikiendelea

CHADEMA yaweka pingamizi dhidi ya akina Mdee kuendelea kuwa wabunge wakati kesi ya msingi ikiendelea

Chadema wanaicheza ngoma vizuri.
Katika mchezo wa mpira wa miguu timu pinzani ambayo ina mbinu nyingi uwanjani wakiwaona wapinzani wao ni tishio huwa wanabadili staili ya mchezo ili mcheze wanavyotaka wao, mkishaingia kwenye mtego wao basi hapo ujue wameshamaliza mchezo !! Ila kwenye sheria sijui huwa inakuwaje !!
 
Nadhani ni vyema na haki ikiwa watawekewa pingamizi kwakuwa hawakuwahi kuteuliwa kukiwakilisha chama.

CHADEMA wakiwaacha hawa covid 19 waendelee maana yake watakuwa wameshiriki kutenda uovu.

CDM wanaweza kuja na sababu luluki kwanini wasiendelee kukiwakilisha Bungeni.

Mosi,Chama hakijawahi kuwateua kuwakisha Bungeni,hii yaweza kuwa sababu muhimu sana.Wakiambiwa leo hii watoe nyaraka za kuteuliwa ni wazi hawata kuwa nazo.

Pil,Mdee alikuwa Mwenyekiti wa BAWACHA kwa nafasi hii alikuwa ni mjumbe wa Kamati kuu,Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa CHAMA.Hakuna kikao chochote kilichokaa kujadili majina na hatimae kuyapitisha na kuandikiwa majina na Katibu Mkuu kwaajili ya uteuzi.

Mwisho nahisi Mdee na genge lake wanaweza kujikuta katika hali ngumu iwapo Mahakama itaamua kufuata misingi ya sheria na haki.
 
Wangewaacha ila wao wautaarifu Umma kuwa wameshamalizana nao hivyo wasije wakafanya lolote kwa jina la chama wala kujitambulisha kwa kutumia jina la chama, na kwa kuwa siku hazigandi Bunge likija kuvunjwa na uchaguzi kutangazwa watajua pa kuelekea.
 
Mahakama haiwezi kuamua kufukuzwa ubunge au wasifukuzwe.tulia ndo mwenye maamuzi hayo.
Ila kabla ya kufukuzwa ubunge tujiulize waliingiaje bungeni na kwa utaratibu upi?
Waliingiaje? Hilo ndilo Chadema inataka liwekwe wazi nani alimtoa Nusrat gerezani usiku kesho yake akaapishwa.
 
Wangewaacha ila wao wautaarifu Umma kuwa wameshamalizana nao hivyo wasije wakafanya lolote kwa jina la chama wala kujitambulisha kwa kutumia jina la chama, na kwa kuwa siku hazigandi Bunge likija kuvunjwa na uchaguzi kutangazwa watajua pa kuelekea.
Mahakama ndiyo itakayowafanya wasitumie jina la chama na kujitambulisha kama wanaCDM.
 
Kesho mahakama inatarajiwa kusikiliza pingamizi lililowekwa na CHADEMA dhidi ya Halima Mdee na wenzake 18 kufuatia maombi ya amri ya muda ya mahakama kuzuia Tume ya Uchaguzi na Spika kuwavua ubunge.

Wabunge hao wanaomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wao.
Hakuna mahakama Tanzania.
Kuna majaji watendaji wa Ccm.
Huwezi kutegemea Jaji mwenye kujua sheria atoe maamuzi ya ajabu kwa watu wanao liibia Taifa.
 
Wastage of time, huu muda ungetumika kukazia muelekeo wa katiba mpya badala ya kupambana na mambo ambayo hayana tija.

Kinachotafutwa hapo ni kilaupande umkomoe mwenzake ikiwezekana, yani kuonyeshana ubabe, ubabe ambao hauna maslahi yoyote kwa taifa.
Ni upande mmoja tu unaojionyesha ubabe, ambao ni Serikali. Kwasababu ndiyo inatoa fedha pande husika. Ukiona mbuzi yuko juu ya mti ujue kapandishwa!
 
Wastage of time, huu muda ungetumika kukazia muelekeo wa katiba mpya badala ya kupambana na mambo ambayo hayana tija.

Kinachotafutwa hapo ni kilaupande umkomoe mwenzake ikiwezekana, yani kuonyeshana ubabe, ubabe ambao hauna maslahi yoyote kwa taifa.
Anayepaswa aone hili jambo halina maslani kwa taifa ni yule anayekusanya kodi kwa wananchi wanyonge alafu anazifuja kwa kuwalipa watu wasio na sifa.Tuwaache chadema wafanye upande wao the rest watafanya wanaoihujumu nchi.iko siku tunaweza tukapata viongozi wanaojielewa wakasaidia kuweka misingi bora ya namna yakuendesha nchi.Kwa sasa ngoja tupige mark time kwasababu hatujielewi.
 
Wastage of time, huu muda ungetumika kukazia muelekeo wa katiba mpya badala ya kupambana na mambo ambayo hayana tija.

Kinachotafutwa hapo ni kilaupande umkomoe mwenzake ikiwezekana, yani kuonyeshana ubabe, ubabe ambao hauna maslahi yoyote kwa taifa.
Wacha bhwanah!
Wewe muda huo umeutumia wapi na una maslahi gan juu ya swala hilo?
 
Back
Top Bottom