CHADEMA yaweka pingamizi dhidi ya akina Mdee kuendelea kuwa wabunge wakati kesi ya msingi ikiendelea

CHADEMA yaweka pingamizi dhidi ya akina Mdee kuendelea kuwa wabunge wakati kesi ya msingi ikiendelea

Naona CHEDEMA wameamua kukubali kupotezewa muda na CCM, wenzao wanafurahia ujinga, sasa kama Chadema wakiamua kukomalia ujinga, nao watakuja kuonekana wajinga, it's a matter of time.
Ninaamini CHADEMA wanao uwezo wa kutafuna Big G, huku wakiweza kutembea pia!

Kuwaachia CCM juu ya hili itakuwa ni makosa makubwa sana. Watajenga mazoea na kuyafanya kanuni!
 
Ni upande mmoja tu unaojionyesha ubabe, ambao ni Serikali. Kwasababu ndiyo inatoa fedha pande husika. Ukiona mbuzi yuko juu ya mti ujue kapandishwa!
Covid 19 eeeh 😂😂😂😂😂😂😂
1656429288835.png
 
Katiba ya Chadema si inakataza kupeleka masuala ya chama mahakamani?
 
Kwa hiyo zikitokea forgeries nyingine toka NEC watu watulie tu na iwe poa.
Kwani utafanya nini? mahakama zao, bunge la hovyo lao, hao wahalifu marafiki zao, hizo record mnazosema mtaziweka mpaka siku CCM iondoke madarakani, kwa sanduku la kura?!

Kama mwanzo Chadema walisusia huu ujinga mpaka wao CCM wakataka maridhiano, kwanini wasiwakumbushe walipotoka ili CCM ipate muda wa kutafakari ujinga wao? na kwanini isiwe sasa?

Kuendelea kukaa nao mezani ni kuwadumaza kiakili, wanajiona wako sahihi, wakati the truth is, wanazidi kuharibu, na wale wanaokaa nao wanazidi kulikuza tatizo, pia wanastahili lawama.
 
Una moyo wa walioshindwa
 
Una moyo wa walioshindwa
Chadema walipogoma kutambua matokeo ya uchaguzi mpaka pale CCM walipotaka maridhiano haukuwa udhaifu, walishinda; na wakigomea mazungumzo ya kisanii tena hautakuwa udhaifu, watashinda pia.

Lakini kuendelea kukomalia njia moja hata kama haina dalili za mafanikio ni kujidumaza akili, na uoga tu.
 
Haya ni maigizo na batili ,inavyoonekana Kuna taasisi zimetekwa na taasisi zingine,ukiwauliza rationale ya kufanya hivi hawana majibu,watakwambia ni maagizo kutoka juu.
 
Naona CHEDEMA wameamua kukubali kupotezewa muda na CCM, wenzao wanafurahia ujinga, sasa kama Chadema wakiamua kukomalia ujinga, nao watakuja kuonekana wajinga, it's a matter of time.

Ambacho Chadema hawataki ni wale wabunge 19 kutumia Jina lao wakati siyo wanachama wa chadema. Yani waendelee na Ubunge wao kwa chama kingine na sio chadema.
 
Nadhani ni vyema na haki ikiwa watawekewa pingamizi kwakuwa hawakuwahi kuteuliwa kukiwakilisha chama.

CHADEMA wakiwaacha hawa covid 19 waendelee maana yake watakuwa wameshiriki kutenda uovu.

CDM wanaweza kuja na sababu luluki kwanini wasiendelee kukiwakilisha Bungeni.

Mosi,Chama hakijawahi kuwateua kuwakisha Bungeni,hii yaweza kuwa sababu muhimu sana.Wakiambiwa leo hii watoe nyaraka za kuteuliwa ni wazi hawata kuwa nazo.

Pil,Mdee alikuwa Mwenyekiti wa BAWACHA kwa nafasi hii alikuwa ni mjumbe wa Kamati kuu,Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa CHAMA.Hakuna kikao chochote kilichokaa kujadili majina na hatimae kuyapitisha na kuandikiwa majina na Katibu Mkuu kwaajili ya uteuzi.

Mwisho nahisi Mdee na genge lake wanaweza kujikuta katika hali ngumu iwapo Mahakama itaamua kufuata misingi ya sheria na haki.
Iwapo itaamua kufuata misingi ya sheria na haki !! You can say that again !!! Sheria ni msumeno unakata mbele na nyuma ! Tusisahau msemo huu wa kiswahili !!!
 
Haya ni maigizo na batili ,inavyoonekana Kuna taasisi zimetekwa na taasisi zingine,ukiwauliza rationale ya kufanya hivi hawana majibu,watakwambia ni maagizo kutoka juu.
Hata mhe mmoja aliyejiuzulu bila kupenda analijua hilo !!
 
Chadema walipogoma kutambua matokeo ya uchaguzi mpaka pale CCM walipotaka maridhiano haukuwa udhaifu, walishinda; na wakigomea mazungumzo ya kisanii tena hautakuwa udhaifu, watashinda pia.

Lakini kuendelea kukomalia njia moja hata kama haina dalili za mafanikio ni kujidumaza akili, na uoga tu.
Samehe saba Mara sabini ! Kisha mapambano yaendelee !!
 
Chadema, kina Mdee kortini tena leo​

Wednesday June 29 2022​

mdeepiic

Summary

  • Waliokuwa wanachama 19 wa Chadema, akiwamo Halima Mdee wanaingia katika mchuano na chama hicho wakati wa usikilizwaji wa pingamizi dhidi ya maombi ya amri ya kudumisha hali ilivyo (kulinda ubunge wao).
Dar es Salaam. Waliokuwa wanachama 19 wa Chadema, akiwamo Halima Mdee wanaingia katika mchuano na chama hicho wakati wa usikilizwaji wa pingamizi dhidi ya maombi ya amri ya kudumisha hali ilivyo (kulinda ubunge wao).

Mdee na wenzake 18 wamefungua maombi Mahakama Kuu, Masjala Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa chama cha Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi namba 16 ya mwaka 2022 kwa ajili ya kupata amri ya mahakama kudumisha hali ilivyo kwa sasa.

Amri hiyo inalenga kuizuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Spika, kutekeleza uamuzi huo wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yote yalitajwa mahakamani juzi, lakini Chadema wakaibua pingamizi dhidi ya maombi hayo ya zuio.

Katika pingamizi lao, Chadema wanapinga usikilizwaji wa maombi hayo ya zuio wakidai kuwa kiapo kinachoyaunga mkono kina kasoro za kisheria, huku wakibainisha hoja tatu za kasoro hizo.

Pamoja na mambo mengine, Chadema kupitia kwa jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala inadai kiapo hicho kina kasoro kutokana na kuingizwa mambo yasiyopaswa kuwamo.

Mambo hayo ni hoja, maoni na mambo ya uvumi, masuala ambayo ni kinyume cha matakwa ya kisheria, inayoelekeza kuwa taarifa za kwenye kiapo ziwe ni za ufahamu wa mla kiapo na kusiwe na maoni, mapendekezo au taarifa za uvumi.

Hata hivyo, Mahakama hiyo ilitoa amri ya kudumisha hali ilivyo kwa sasa kuhusu hadhi ya ubunge wa kina Mdee hadi leo wakati maombi hayo ya zuio yatakaposikilizwa.

Tayari jana Chadema waliwasilisha mahakamani kiapo kinzani kujibu maombi hayo ya kina Mdee wanaowakilishwa na mawakili Aliko Mwamanenge, Ipilinga Panya na Edson Kilatu.
 
Kwani utafanya nini? mahakama zao, bunge la hovyo lao, hao wahalifu marafiki zao, hizo record mnazosema mtaziweka mpaka siku CCM iondoke madarakani, kwa sanduku la kura?!

Kama mwanzo Chadema walisusia huu ujinga mpaka wao CCM wakataka maridhiano, kwanini wasiwakumbushe walipotoka ili CCM ipate muda wa kutafakari ujinga wao? na kwanini isiwe sasa?

Kuendelea kukaa nao mezani ni kuwadumaza kiakili, wanajiona wako sahihi, wakati the truth is, wanazidi kuharibu, na wale wanaokaa nao wanazidi kulikuza tatizo, pia wanastahili lawama.
Una moyo wa walioshindwa
Chadema walipogoma kutambua matokeo ya uchaguzi mpaka pale CCM walipotaka maridhiano haukuwa udhaifu, walishinda; na wakigomea mazungumzo ya kisanii tena hautakuwa udhaifu, watashinda pia.

Lakini kuendelea kukomalia njia moja hata kama haina dalili za mafanikio ni kujidumaza akili, na uoga tu.
Suala la forgeries ni la mwelekeo wa kijinai na si la kisiasa.
Wanaotaka kuliweka likawa la kisiasa ni kwa sababu wanafaidika nalo.
 
Ambacho Chadema hawataki ni wale wabunge 19 kutumia Jina lao wakati siyo wanachama wa chadema. Yani waendelee na Ubunge wao kwa chama kingine na sio chadema.
Good. Hii ndiyo sababu muhimu ninayoona kwa CHADEMA kuhangaikia hili suala. Jina la chama kutumika bila ridhaa ya chama.

Kumbukumbu zinawekwa na inatokea msimamo wa CHADEMA kunasibishwa na kauli za hao wabunge ilhali chama hakihusiki nao. Si sahihi kisiasa wala kisheria. Hivyo wao wajikite kwenye suala la uanachama na matumizi ya jina la chama tu.

Zaidi ya kuzuia jina lake kutumika isivyostahili, CHADEMA hawana haja ya kuhangaika ukiukaji wa katiba wala kodi inayofujwa kuwalipa hao wabunge feki. Kama wananchi wenyewe hawasumbuki kuihoji serikali kwa ukiukaji wa katiba na kuchezea hazina ya taifa, so be it.

Si vyema CHADEMA kumwaga kilio kuliko wenye msiba wao. Nchi yenyewe watu hata hawaoni shida kuona wanasiasa wanaochaguana na kuteuana kishikaji wanapimiwa malipo makubwa makubwa bila mantiki yoyote huku watumishi muhimu wakilipwa peanuts na ajira zikibanwa kadiri viongozi wanavyojisikia!
 
Naona CHEDEMA wameamua kukubali kupotezewa muda na CCM, wenzao wanafurahia ujinga, sasa kama Chadema wakiamua kukomalia ujinga, nao watakuja kuonekana wajinga, it's a matter of time.
sasa ngoja tuone kwenye hii saga kati ya chadema na wewe nani ni ZWAZWA POYOYO
 
Back
Top Bottom