Sisi sio timu useme tuna msemaji wetu, hili ni jukwaa huru kila mtu anaweza kuchangia apendacho, sisi tulioamua kwamba hatutapiga kura ni mpaka hapo itakapopatikana tume huru, ama mazingira ya kuridhisha kupiga kura msimamo wetu uko pale pale. Kuoana mawazo na mitazamo kwenye baadhi ya mambo haimaanishi tunakubaliana kwenye kila jambo au tunalazimika kukubaliana kwa kila jambo. Yeye kama anaamini kwenye box la kura aendelee kuamini hiyo ni haki yake, lakini sisi wengine hilo ni zoezi haramu kama haramu nyingine na hatuyumbi kwenye hilo. Hata aseme kiongozi yoyote wa cdm, ccm, dini nk, bado msimamo mwetu ni dhabiti kwa kutoshiriki ushenzi unaoitwa uchaguzi kwenye awamu hii ya tano hilo halitawezekana.