Chagua CHADEMA upate Demokrasia na maendeleo Mtaani kwako

Hizi siasa bhana zimefanya tumekosa kujengewa soko la kisasa tumekosa kujengewa mradi wa maji viongozi mliopo madaraka munayo ya fanya hayata saidia kitu chochote zaidi ya kuweka aibu kwa vizazi vijavyo ni vyema ukafanya lile kama wajibu wako ndio maana ukaomba nafasi

Ccc NAKWEDE
 
Nyie ambao mko kwenye ufalme hatuna tatizo na nyie maana mnapigania mlo, na wala hatungoji ushawishi wenu, kuleni na kusaza lakini hatuna muda wa kushiriki chaguzi za kishenzi.
Laiti ungalijua, it's only God knows
Mimi niko sekta binafsi, na hii ndio situation wetu

P
 
Helikopta za kabla zilikuwa za dk.Slaa na wafadhili wake wazungu ambao baada ya kuondoka hazipo za dk slaa Wala za Lowasa na Mbowe hana wafadhili wenye helikopta za kumpa wawe wa ndani au nje

Ndio maana nakuambia umeanza kujua siasa enzi hizi za Magufuli, ndio maana unabeba propaganda nyepesi unazigeuza ndio hoja zako. Kwa taarifa yako Helkopta alianza kutumia Mbowe alipogombea uchaguzi wa urais mwaka 2005. Na nguvu hizo ni za kina Ndessamburo na matajiri wengine. 2010 helkopta ilipata umaarufu baada ya cdm kuwa na mgombea sahihi ambaye ni Dr. Slaa. Ila Slaa hakuwa anajua hata pesa inatokea wapi maana hakuwahi kuwa mfanyabiashara.

Ni vyema ukabaki kujadili SGR, na SG wangalau ndio zilizo kwenye upeo wako, hayo ya helkopta za cdm utaishia kuchekesha tu.
 
Laiti ungalijua, it's only God knows
Mimi niko sekta binafsi, na hii ndio situation wetu

P

Ni hivi Paschal ww uko 50+, na hata uandishi wako inabidi uandike hivi na ukizingatia uko na verified user sikulaumu sana. Haya ninayoongea ya katiba mpya na tume huru kwako ni ndoto na huna muda tena wa kungonja kwani umebakiza miaka michache kufika 60, miaka ya kulea wajukuu na kupambana na kisukari, ndio maana unasema tutasubiri sana ukiamini upinzani ni lazima uwe chini ya cdm au chama chochote cha siasa, hivyo kwako 2020 ni mwisho wa upinzani.

Hii post uliyoileta hapa kuonyesha financial status yako chini ya Magufuli, ni kutaka tu uonyeshe na ww sio sehemu ya wafaidika wa awamu hii. Ila ni wiki iliyopita tu ulikuwa kwa Anthony Mtaka na ukapata Airtime Star TV, ungekuwa kweli uko kinyume hata huo mwaliko wa Mtaka usingepata. Isitoshe huenda chini ya awamu hii hujala shavu kama awamu zilizopita, ila ni ukweli usioacha shaka ww ni mmoja ya watanzania mliokula keki ya taifa hili, kihalali na kiupendeleo. Hivyo una haki ya kulia sasa maana hauko kwenye eneo ulilozoea, sisi wenzako hatujawahi, ndio maana hatuwezi kuuma na kupuliza kama ww. Kwa nafasi yako unaweza kushabikia huu uhuni unaondelea katika box la kura hivi sasa, kwani historia yako pia ww ulifaidika na mifumo mibovu ya utawala wa nchi hii.
 
Asante Mkuu Sky Eclat kwa uhamasishaji huu, kwa bahati nzuri sana, Watanzania wa sasa, wameisha amka kutoka, usingizini, sio watu tena wa kupelekwa pele kwa kufuata tuu mkumbo, wameishajua wanataka nini kwa maendeleo yao, na wanajua watamchagua nani anayeweza kuwaletea maendeleo.

Hata hivyo pamoja na kujua, ukweli kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa na mshindi ameisha julikana, uchaguzi ni wa kukamilisha tuu taratibu, lakini bado uhamasishaji kama huu ni muhimu sana kwa sababu angalau mtaambulia ambulia tujikura tuchache, twa kuhalalisha kwa wafadhili wetu Tanzania tuna demokrasia, na kuwa ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki wa kidemokrasia, uliokuwa na ushindani wa kweli

Asante tena kwa uhamasishaji huu.

P
We uteuzi hupati ng'ooo
 
Mlihamasisha tusijiandikishe, sasa ivi mnasema tichague chadema! Sasa tutapigaje kura?
 
Safari hii helokpta na ndege za Lowasa haziko hewan kutangaza wagombea chadema safari mtakoma Lowasa ndiye aliwapaisha.Mnaishia internet cafe kutengeneza matangazo
Kuleta hadithi za Lowassa ni sawa na kujidhalilisha bure
 
Ni hivi Paschal ww uko 50+, na hata uandishi wako inabidi uandike hivi na ukizingatia uko na verified user sikulaumu sana. Haya ninayoongea ya katiba mpya na tume huru kwako ni ndoto na huna muda tena wa kungonja kwani umebakiza miaka michache kufika 60, miaka ya kulea wajukuu na kupambana na kisukari, ndio maana unasema tutasubiri sana ukiamini upinzani ni lazima uwe chini ya cdm au chama chochote cha siasa, hivyo kwako 2020 ni mwisho wa upinzani.

Hii post uliyoileta hapa kuonyesha financial status yako chini ya Magufuli, ni kutaka tu uonyeshe na ww sio sehemu ya wafaidika wa awamu hii. Ila ni wiki iliyopita tu ulikuwa kwa Anthony Mtaka na ukapata Airtime Star TV, ungekuwa kweli uko kinyume hata huo mwaliko wa Mtaka usingepata. Isitoshe huenda chini ya awamu hii hujala shavu kama awamu zilizopita, ila ni ukweli usioacha shaka ww ni mmoja ya watanzania mliokula keki ya taifa hili, kihalali na kiupendeleo. Hivyo una haki ya kulia sasa maana hauko kwenye eneo ulilozoea, sisi wenzako hatujawahi, ndio maana hatuwezi kuuma na kupuliza kama ww. Kwa nafasi yako unaweza kushabikia huu uhuni unaondelea katika box la kura hivi sasa, kwani historia yako pia ww ulifaidika na mifumo mibovu ya utawala wa nchi hii.
Duh!. Mkuu Tindo, maneno makali sana haya ila ni ukweli mtupu japo ni mchungu, one thing which is not true ni ile ya "kiupendeleo", sio kiupendeleo bali ni juhudi tuu.

The law of the jungle ina kanuni zake and you are free to choose in between to join them and keeping on living or stick to your guns and perish, I've chosen to live.

Please soma tarehe ya bandiko hili uangalie niliamua lini na kwa nini?.

Nakubaliana na maelezo yako ili mjadala uendelee na siku zisonge, ila kiukweli Paskali ww sio sehemu ya mabadiliko ya kweli, hasa kwa kigezo za historia yako na umri wako wa sasa. Ww baki ukishabakia chaguzi za hujuma kwa usalama wa maisha yako na sehemu ya mlo wako. Acha wale ambao tumeamua kusimamia mabadiliko ya kweli, hata tusipoyapata sasa watayapata watoto wetu, lakini huko kwenye mfumo wa chama kimoja hatutorudi, ni kama waisraeli kurejea utumwani Misri.
 
Asante Mkuu Sky Eclat kwa uhamasishaji huu, kwa bahati nzuri sana, Watanzania wa sasa, wameisha amka kutoka, usingizini, sio watu tena wa kupelekwa pele kwa kufuata tuu mkumbo, wameishajua wanataka nini kwa maendeleo yao, na wanajua watamchagua nani anayeweza kuwaletea maendeleo.

Hata hivyo pamoja na kujua, ukweli kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa na mshindi ameisha julikana, uchaguzi ni wa kukamilisha tuu taratibu, lakini bado uhamasishaji kama huu ni muhimu sana kwa sababu angalau mtaambulia ambulia tujikura tuchache, twa kuhalalisha kwa wafadhili wetu Tanzania tuna demokrasia, na kuwa ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki wa kidemokrasia, uliokuwa na ushindani wa kweli

Asante tena kwa uhamasishaji huu.

P
Chadema hawakujianda kwa huu uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji.
 
Tamisemi ndio walijiandaa na ndio tunapoona hujuma za wazi toka kwa waliopewa jukumu la kusimamia uchaguzi. Ukitaka kujua ujinga wa mtu mweusi, angalia chaguzi zetu, hapo ndio utajua kabisa wazungu kutuita manyani wako sahihi sana. Halafu kichekesho, watu wanaoingia madarakani kwa kunajisi box la kura ndio hujifanya kuhadaa wananchi kuwa wao ni wazalendo, na wanapambana na rushwa na dhuluma!
 
Nakubaliana na maelezo yako ili mjadala uendelee na siku zisonge, ila kiukweli Paskali ww sio sehemu ya mabadiliko ya kweli, hasa kwa kigezo za historia yako na umri wako wa sasa. Ww baki ukishabakia chaguzi za hujuma kwa usalama wa maisha yako na sehemu ya mlo wako. Acha wale ambao tumeamua kusimamia mabadiliko ya kweli, hata tusipoyapata sasa watayapata watoto wetu, lakini huko kwenye mfumo wa chama kimoja hatutorudi, ni kama waisraeli kurejea utumwani Misri.
Watu tumetofautiana uoni, in terms of point of views, magnitude na distance of vision, wengine uwezo wao ni kuona hadi mwisho wa pua zao, na wengine miaka 10 mbele, wengine hadi miaka 100 mbele.

Kwa mtazamo wangu, upinzani huu uliopo mwisho wake ni 2020, tutakaa mapumziko ya miaka 5 hadi Magufuli atakapoondoka 2025, ndipo ujenzi wa upinzani stanza tena mdogo mdogo, hivyo uchaguzi mwingine wa vyama vingi ni 2030.

P
 
Kuwapigia kura Chadema ni sawa sawa na kutumbukiza mkate chooni... Baada ya Mwaka unasikia amejiuzulu uanachama na kuhamia CCM kuunga mkono juhudi... Ni bora kuwapigia CCM kabisa
 
Chadema hawakujianda kwa huu uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji.
Bora Tukuachie Wewe, Chadema wenyewe hawapendi kuambiwa ukweli huu. Ukipandisha uzi wowote kuzungumzia mapungufu ya Chadema, wanakuwa wakali na kukushukia kama mwewe.

Nisome hapa,

P
 
Watu tumetofautiana uoni, in terms of point of views, magnitude na distance of vision, wengine uwezo wao ni kuona hadi mwisho wa pua zao, na wengine miaka 10 mbele, wengine hadi miaka 100 mbele.

Kwa mtazamo wangu, upinzani huu uliopo mwisho wake ni 2020, tutakaa mapumziko ya miaka 5 hadi Magufuli atakapoondoka 2025, ndipo ujenzi wa upinzani stanza tena mdogo mdogo, hivyo uchaguzi mwingine wa vyama vingi ni 2035.

P

Mkuu huenda macho yako yanaona kwenye ushindani wa vyama tu, kana kwamba viongozi wote duniani hupatikana kwa box la kura tu. After all hatujali ushindani wa vyama pekee kwani siasa inaweza kufanyika bila hata uwepo wa hivyo vyama. Usichojua ukiua mfumo rasmi wa ushindani utaanzisha mfumo usio rasmi wa ushindani. Umma unaweza kufanya upinzani bila hata kutegemea platform za vyama vya siasa, vyama vya siasa ni platform rasmi. Subiri tu utajionea aina mpya ya siasa za upinzani bila vyama vya upinzani.
 
Kuwapigia kura Chadema ni sawa sawa na kutumbukiza mkate chooni... Baada ya Mwaka unasikia amejiuzulu uanachama na kuhamia CCM kuunga mkono juhudi... Ni bora kuwapigia CCM kabisa

Uza ubongo huo maana unaishi nao kwa hasara, nani kakudanganya anayetaka kuwapigia kura wapinzani wasipokuwepo basi atawapigia ccm? Kwa taarifa yako hizo hujuma dhidi ya upinzani sio faida hata kwa hiyo ccm, kwani kama ni wapiga kura watazidi kuwa wachache, hata wale waliokuwa waipigie kura ccm hawatakuwa na wa kiwasisimua kushiriki huo uchaguzi.
 
Mkuu huenda macho yako yanaona kwenye ushindani wa vyama tu, kana kwamba viongozi wote duniani hupatikana kwa box la kura tu. After all hatujali ushindani wa vyama pekee kwani siasa inaweza kufanyika bila hata uwepo wa hivyo vyama. Usichojua ukiua mfumo rasmi wa ushindani utaanzisha mfumo usio rasmi wa ushindani. Umma unaweza kufanya upinzani bila hata kutegemea platform za vyama vya siasa, vyama vya siasa ni platform rasmi. Subiri tu utajionea aina mpya ya siasa za upinzani bila vyama vya upinzani.
Haya kama ni kwa Watanzania hawa hawa wenye utii wa ukondoo, na wengine waoga kama kunguru, ... ok, ngoja tusubiri, ila wale waona mbali, tumeisha ona na kufanya maamuzi
P
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Bora Tukuachie Wewe, Chadema wenyewe hawapendi kuambiwa ukweli huu. Ukipandisha uzi wowote kuzungumzia mapungufu ya Chadema, wanakuwa wakali na kukushukia kama mwewe.

Nisome hapa,

P

Uko sahihi sana kwamba cdm hawapendi kuambiwa ukweli, je unaweza kutuonyesha ni uzi upo ulipandisha kuwaambia ccm mapungufu yao wakifurahia hayo mapungufu uliyowaambia? Kama ni cdm tu wanachukia kuambiwa mapungufu yao, bungeni uliopitwa na kamati ya maadili walienda kukupongeza kwa ukweli uliowaambia?
 
Haya kama ni kwa Watanzania hawa hawa wenye utii wa ukondoo, na wengine wagon kama kunguru, ... ok, ngoja tusubiri, ila wale waona mbali, tumeisha ona na kufanya maamuzi
P

Mkuu siongelei watanzania wengine bali naongelea hawa hawa wenye utii wa kondoo.
 
Back
Top Bottom