Chagua jinsia ya mtoto umtakaye

Chagua jinsia ya mtoto umtakaye

kabwigwa

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
933
Reaction score
1,540
Habari wanajamvi,

Kumekua na malalamiko katika familia nyingi sana kuhusiana na jinsi₍ jinsia₎ ya watoto.Waweza kukuta mzazi anazaa watoto wa kike tu au kinyume chake hii inapunguza furaha na kuleta mifarakano katika jamii.

Kwakutumia Calenda ya kichina iitwayo Chinese Lunar Calendar waweza kupata jinsia ya mtoto umtakaye. Kalenda hii inaanza kusoma kuanzia miaka kumi na nane ₍ 18₎mpaka miaka arobaini na tano₍45₎

Unachotakiwa kufanya ni kuangalia umri wa mama ambao upo upande wa juu wa chat na miez ambayo ipo upande wa kushoto kwa chat, na mwezi ambao utaonyesha ni mtoto wa aina gani anapatikana katika mwezi husika, mfano mama /mwanamke ana miaka ishirini na tisa₍29₎ na anataka mtoto wa kiume, akiangalia kwenye kalenda ataona kuwa kwa umri wake miezi ya kupata mtoto wa kiume ni mwez 2,5,6,7,8 na wa 9.cha kuzingatia ni mama/mwanamke kutokudanganya tu umri wake. Kinachoangaliwa ni siku katika mwezi mimba ilipoingia/itakapo ingia na umri wa mama.

NB: Kalenda hii imekua ikitumika huko china kwa miaka na mikaka, binafsi nimeshaifanyia majaribio na imethitisha jinsia ya mtoto kwa asilimia 99 kwa ambao hawakudanganya umri.
Nimeambatanisha hiyo kalenda.
 

Attachments

  • chinese-lunar-calendar - Copy.png
    chinese-lunar-calendar - Copy.png
    64.6 KB · Views: 1,013
  • chinese-lunar-calendar - Copy.png
    chinese-lunar-calendar - Copy.png
    64.6 KB · Views: 899
hizi kalenda ni usanii wa wapiga kareti (komando kipensi) jinsia anapanga Mungu si wachina? kama wao mabingwa waunde kalenda ya kuongeza urefu (kimo).
 
Kueleweka sasa, hiyo 18-34 ni miaka au tarehe ktk huo? Kama ni miaka hiyo miezi ina siku ngapi mkuu?
 
hizi kalenda ni usanii wa wapiga kareti (komando kipensi) jinsia anapanga Mungu si wachina? kama wao mabingwa waunde kalenda ya kuongeza urefu (kimo).
Mungu alishaweka kanuni na maarifa sio miujiza tu, kufuata kanuni hizo ndo uchamungu wenyewe na si vinginevyo.
 
Wengi wa rika letu hawajui umri wao kwa sababu wazee wao hawakusoma hivyo walikadiria tu.

Sasa utajuaje ukweli?
 
Habari wanajamvi,Kumekua na malalamiko katika familia nyingi sana kuhusiana na jinsi₍ jinsia₎ ya watoto.Waweza kukuta mzazi anazaa watoto wa kike tu au kinyume chake hii inapunguza furaha na kuleta mifarakano katika jamii.
Kwakutumia Calenda ya kichina iitwayo Chinese Lunar Calendar waweza kupata jinsia ya mtoto umtakaye.Kalenda hii inaanza kusoma kuanzia miaka kumi na nane ₍ 18₎mpaka miaka arobaini na tano₍45₎
Unachotakiwa kufanya ni kuangalia umri wa mama ambao upo upande wa juu wa chat na miez ambayo ipo upande wa kushoto kwa chat, na mwezi ambao utaonyesha ni mtoto wa aina gani anapatikana katika mwezi husika,mfano mama /mwanamke ana miaka ishirini na tisa₍29₎ na anataka mtoto wa kiume,akiangalia kwenye kalenda ataona kuwa kwa umri wake miezi ya kupata mtoto wa kiume ni mwez 2,5,6,7,8 na wa 9.cha kuzingatia ni mama/mwanamke kutokudanganya tu umri wake.Kinachoangaliwa ni siku katika mwezi mimba ilipoingia/itakapo ingia na umri wa mama.
NB Kalenda hii imekua ikitumika huko china kwa miaka na mikaka,binafsi nimeshaifanyia majaribio na imethitisha jinsia ya mtoto kwa asilimia 99 kwa ambao hawakudanganya umri.
Nimeambatanisha hiyo kalenda.
Mbona kalenda zako zimeishia mwisho miaka 35 tu?
 
Duh....kwa hivyo wanawake wenye umri unaofanana (say wadada mapacha wenye 25 years) wakipata mimba leo hii (19 December 2016) wote watapata watoto wa kiume? Ngumu sana kumesa hii.
 
Wengi wa rika letu hawajui umri wao kwa sababu wazee wao hawakusoma hivyo walikadiria tu.

Sasa utajuaje ukweli?
Kama huujui umri wako ni shida kalenda itakupa matokeo tofauti huwez kuupata ukweli
 
Back
Top Bottom