Chagua wachezaji watatu ambao ni viungo wakabaji (CDM) bora wa muda wote?

Chagua wachezaji watatu ambao ni viungo wakabaji (CDM) bora wa muda wote?

Hiyo hiyo ya kina kaka, 2004 ile, san siro anampiga chuma 4-1, anaenda spain anampiga chuma 4 kavu, deportivo anakuja kutoka nusu fainali kwa porto ya mourinho... Ugenini 0-0, nyumbani anakufa 1-0
But nilikua disappointed sana, nilitamani deportivo aende mbele.
Monaco walikua vizuri sana nao wakanidisappoint kwenye final. Nilikua namkubali Sana Jerome Rothem, sijui kwa nn hakupataga timu kubwa

Hiyo Porto nilikua namkubali sana fundi Carlos Alberto, alikua na style ya kuweka plasta puani. Nae hakupataga bahati ya kwenda timu kubwa
 
Ilizoeleka viungo wakabaji ni wavunja kuni
Mfano: makelele, Gattuso Roy keane, mamadou diarra, edmilson, essien n.k

Lakini yeye alikuja kuwa wa tofauti, very soft na hakabi kwa nguvu ni kucheza kwenye nafasi tu.
Tiki taka la Pep lilimfaa sana kumfichia madhaifu yake I.e lack of physical combativeness.

Angecheza kwenye timu ambayo haimiliki mpira sana angekua exposed zaidi.
 
Busquets jamaa kaleta mapinduzi makubwa sana kwenye hiyo namba so kwangu ndiye namba moja,then Claudio Makelele,halafu Captain Dunga hawa ni aina ya wachezaji wasio onekana, ila wakikosekana ndipo unajua umuhimu wake kwenye timu.
Kweli kabisa
 
But nilikua disappointed sana, nilitamani deportivo aende mbele.
Monaco walikua vizuri sana nao wakanidisappoint kwenye final. Nilikua namkubali Sana Jerome Rothem, sijui kwa nn hakupataga timu kubwa

Hiyo Porto nilikua namkubali sana fundi Carlos Alberto, alikua na style ya kuweka plasta puani. Nae hakupataga bahati ya kwenda timu kubwa
Maisha kiujumla yanahitaji bahati zaidi kuliko chochote kile. Nami tamaa yangu ilikuwa ni kuona monaco anabeba lile kombe, fainali kina morientes hawakufua dafu mbele ya kina calvarho
 
Maisha kiujumla yanahitaji bahati zaidi kuliko chochote kile. Nami tamaa yangu ilikuwa ni kuona monaco anabeba lile kombe, fainali kina morientes hawakufua dafu mbele ya kina calvarho
Aisee morientes alikuwa ni balaa
 
Nitakueleza kwa uelewa wangu, japo naweza nisiwe sahihi sana

Pirlo alikua central midfielder, kwenye hii position kuwa yule anakua more of attacking na yule anakua more of defensive.
Pirlo hakuwa natural defensive, ndio maana unaona kwa miaka zaidi ya 10 aliyokaa Ac Milan defensive alikua ni Gattuso.

Lakini zipo mechi Pirlo aliswitch kama defensive,na hii ilikuja baadae na pengine ni sababu ya influence ya Busquets, maan ilionekana defensive sio lazima atumie nguvu na kukaba sana. Pia Pep ndio alikuja kuiweka sawa hii kitu tofauti na dhana iliyokuwepo. Uliona hata Bayern kule alimbadilisha hadi beki wa pembeni Joshua Kimmich na kumuweka namba 6
Man city pia zipo mechi nyingi tu anammchezesha Rico Lewis kama namba 6
Nakuelewa. Naelewa pia utata wa namna Pirlo na Gattuso walivyotumika. Coz historia inaeleza na kuweka wazi kuwa GG alikuwa mkabaji hatari sana.

Ila, katika mechi tuliona matumizi ya Pirlo yalivyokuwa. Wakati mwingi angecheza juu ya mabeki wa kati na General Rhino angekuwa anachafua zaidi juu yake.
Nimefurahi kuona wakongwe kadhaa wakiweka mambo sawa kwa rekodi na kumbukumbu murua hasa za mechi za CL.

Hivyo tunaweza kusema Busquets atapewa heshima kwa kustahimili role hiyo kwa muda mrefu ila wapo watu ambao walishafanya hayo kabla yake na kwa ustadi mkubwa kama Andrea.. Wakongwe mzabzab makaveli10 tuondoleeni utata.
 
Pirlo kacheza akiwa milan.. Wanacheza diamond formation.
Ndio maana nilitamani watu wampe heshima Pirlo japo Sergio nae anastahili heshima yake. Ni kama wanaouona mpira sasa wanaamini Busquets ndie mtu wa kwanza kufanya anachofanya kwa ubora.
 
Ndio maana nilitamani watu wampe heshima Pirlo japo Sergio nae anastahili heshima yake. Ni kama wanaouona mpira sasa wanaamini Busquets ndie mtu wa kwanza kufanya anachofanya kwa ubora.
Hajavunjiwa heshima na ndio maana ya hiyo Rank, wote hamuwezi kuwa namba moja ndio maana kuna moja mpaka kumi.
 
Hajavunjiwa heshima na ndio maana ya hiyo Rank, wote hamuwezi kuwa namba moja ndio maana kuna 1 mpaka kumi.
Labda nimeiweka kwenye namna isiyoeleweka kirahisi kidogo. Ila sijasema kwamba amevunjiwa hshima. Ila ni kama watu wengi wa mpira hawajui au kumpa heshima Pirlo katika role aliyocheza.
 
Kwenye hiyo list kakosekana huyu mwamba chini Emerson.
 
Nakuelewa. Naelewa pia utata wa namna Pirlo na Gattuso walivyotumika. Coz historia inaeleza na kuweka wazi kuwa GG alikuwa mkabaji hatari sana.

Ila, katika mechi tuliona matumizi ya Pirlo yalivyokuwa. Wakati mwingi angecheza juu ya mabeki wa kati na General Rhino angekuwa anachafua zaidi juu yake.
Nimefurahi kuona wakongwe kadhaa wakiweka mambo sawa kwa rekodi na kumbukumbu murua hasa za mechi za CL.

Hivyo tunaweza kusema Busquets atapewa heshima kwa kustahimili role hiyo kwa muda mrefu ila wapo watu ambao walishafanya hayo kabla yake na kwa ustadi mkubwa kama Andrea.. Wakongwe mzabzab makaveli10 tuondoleeni utata.
Ninavyoelewa mie kwa italia kuna positions mbili kuu...regista na trequatista. Regista anacheza chini na trequatista ni namba kumi.
Pirlo mwanzoni alikuwa acheze kama namba kumi i.e. trequatista but hana mobility kubwa but had excellent passing skills. Hivyo basi wakaona wamshushe aje kucheza kama namba sita, regista kwa sababu atakuwa na muda na nafasi ukijumlisha umahiri wake wakupiga pasi basi ataweza kupiga pass hatari akiwa katika position hii.

Kutokana na kwamba hana uwezo wa kukaba sana but still ubora wake wa pass unahitajika ndio maana don carlo akaweka pembeni yake watu wa shughuli, gattusso na ambrossini.

Vile vile alivyotoka ac na kwenda juventus, conte aliendekea kumtumia hivyo hivyo albeit yeye conte alikuwa anatumie 3-5-2 formation.
Pembeni ya pirlo alikuwa paul pogba na macchissio ambao ndio walikuwa ndio wapokonyaji mipira kwa asilimia kubwa.

Kwa mtazamo wangu tofauti kuu kati ya pirlo na busquet ni range of passing, pirlo alikuwa na uwezo wakumsaka mchezaji kwa pass ya mita 50 while busquete hakuwa na uwezo huo.
 
Labda nimeiweka kwenye namna isiyoeleweka kirahisi kidogo. Ila sijasema kwamba amevunjiwa hshima. Ila ni kama watu wengi wa mpira hawajui au kumpa heshima Pirlo katika role aliyocheza.
Mfano mimi ukiniwekea Pirlo ni huyu mwamba Emerson na mchagua huyu.Mtoa mada amemsahau ila hili jembe lina kazi sio ya kitoto.
images (91).jpeg

Pirlo mzuri kweli,ila kwenye kupokonya mipira,bado wa kawaida,ila Pirlo mzuri sana kwenye kupiga pasi yupo vizuri, faulo,Kona yupo vizuri,ila ile kukichafua pale kati sio kivile.Ndio Maana pale kati AC Milan alikiwa ana saidiwa sana na Gatuso pamoja na Seedorf na Juve alikuwa anasaidiwa na Aturo Vidal.

Bado kuna mashine nyingine
,hiyo Gilberto Silva ile Arsenal ya Invisible mwamba alikuwa haonekani sana wala kuimbwa ila shughuli yake pale kati sio ya kitoto.
images (92).jpeg

Kwa kifupi kwenye hii list kwa mtizamo wangu amekosekana Mascherano, Gilberto Silva na Emerson.
 
Aisee morientes alikuwa ni balaa
Morientes alikua striker wa kawaida tu, sikuwahi kumuelewa. Huo msimu aliuotea tu ndio maana aliporudi Madrid alipotea
Kama ilivyokua kwa striker wao Dado Prso. Baada ya hiyo season akapotea
 
Back
Top Bottom