Chaguzi zote zijazo, zikiwemo chaguzi ndogo, zitakosa kabisa wapiga kura

Chaguzi zote zijazo, zikiwemo chaguzi ndogo, zitakosa kabisa wapiga kura

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Kwa yaliyotokea katika Uchaguzi huu, wananchi wengi sana wataacha kwenda kupiga kura kuanzia wana-CCM wenyewe,wasio na vyama na zaidi wafuasi wa upinzani.

Hali hii itaanza kujitokeza katika chaguzi za viporo, ambapo watu wengi hawatajitokeza kabisa.Kinachoweza kutokea katika chaguzi za viporo ni diwani katika kata yenye maelefu ya wakazi, kuchaguliwa na watu 500 na wakizidi sana 1000.

Haki ya kikataba ya kuchagua na kuchaguana, sasa imebaki jina tu au kwa maneno mengine, haki hiyo imebaki katika maandishi tu, kiasi kwamba hata ile maana ya kufanya uchaguzi,sasa haipo tena, na matokeo yake yatakuwa ni watu kupuuza chaguzi zote zijazo.

Time will tell.
 
Mkuu kwa taarifa yako vitaanzishwa vyama vipya vya upinzani wa kweli na sio hizi saccos za akina Mbowe, Lipumba na Maalim Seif, Mtu kama Zitto akiacha aina yake ya siasa ya kuganga njaa ni mpinzani mzuri.

Watu wamechoka viongozi wale wale akina "Besigye"!
 
Mkuu kwa taarifa yako vitaanzishwa vyama vipya vya upinzani wa kweli na sio hizi saccos za akina Mbowe, Lipumba na Maalim Seif, Mtu kama Zitto akiacha aina yake ya siasa ya kuganga njaa ni mpinzani mzuri...
Unadhani watu hawajakichoka chama CCM kilicho kaamadarakani miaka 60? Na bado kinahubiri mambo yaleyale miaka yote na bado kimeshindwa kutekeleza yale wanayo yasema, Hufikirii watu wamechoka zaidi?
 
Hoja maiti kama chama chako!
Mkuu ungejua watu tulianza kuwa wapinzani tangu enzi za CUF ya Mzee Mapalala RIP....ni wahuni hawa wametukatisha tamaa tukaona bora tubaki CCM ya JPM,
2414618_24gvpqh.jpg
 
Anaandika Dr. Christopher Cyrilo

Ulichofundishwa kwenye somo la uraia sio kweli. Kenge wewe!

Ulikuwa mwanafunzi bora darasani kuliko wengine, walimu wakakuita 'jiniasi'. Na wewe ukakenua meno na kuchekelea...utafikiri 'jiniasi' kweli!
Ulisoma kwa bidii zote, usiku na mchana - si kwa lengo la kuvuna maarifa bali kufaulu mitihani, ukafaulu bila maarifa. Sio kosa lako, ni mfumo wa elimu yetu unaomfanya mwanafunzi kuogopa mitihani zaidi kuliko kupenda kujifunza, anasema Mwl. Mabala.

Na sasa umekuwa mtu mzima, unashangaashangaa tu. Unachokishuhudia ni tofauti na kile ulichojaza kwenye mtihani wa Uraia uliyofaulu vema kuliko marafiki zako wengi.

Ulifundishwa eti Taifa linaundwa na mihimili mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama, Uongo. Taifa linaundwa na Serikali, Serikali na Serikali. Spika wa bunge na jaji mkuu wote wanasujudu kwa kiongozi wa serikali, na wanaelekezwa cha kufanya na wao wanafuata bila hiyana. Wakikataa watakiona Cha mtemakuni. Kile ulichofundishwa eti mihimili mitatu inayojitegemea ni uongo mtupu.

Ukaambiwa eti viongozi wanachaguliwa na wapiga kura, Uongo.

Viongozi wanachaguliwa na wanaojumuisha mahesabu ya kura. Unapoacha shughuli zako kwenda kupanga foleni ya kupiga kura, sio kwamba ndio unachagua kiongozi - no - no - no, pale unawaongezea kazi wanaohesabu kura tu. Kura zikiwa nyingi ujue watachelewa kumtangaza mtu wanaomtaka wao. Hilo ulikuwa hujui? Wewe kweli ni pimbi.

Ukaambiwa Polisi ni walinzi wa raia na mali zao, na wewe ulivyo kilaza ukaamini kabisa! Kilaza mkubwa wewe!

Polisi ni walinzi wa viongozi wa nchi na matajiri dhidi ya masikini wasumbufu wanaojifanya kudai haki wakati hawana haki. Polisi ni ukuta unaotenganisha wananchi na 'WENYENCHI'. Na Kama hujui basi kuanzia leo ujue - masikini aliyekwapua kuku wa jirani anastahili adhabu kubwa hata kifo wakati tajiri aliyeibia serikali milioni 7 kwa kila dakika anasamehewa. Unakodoa macho?
Unasubiri mkuu mmoja wa mkoa atekwe - apotee uone jeshi la polisi litakavyohangaika? Sasa potea wewe! Watasema umejiteka au umekwenda kutembelea ndugu.

Halafu kuna lile suala la binadamu wote ni sawa! Na wewe uliamini kabisa?

Sikiliza, hata waasisi wa Taifa la Marekani, akina George Washington waliandika hivyo kwenye katiba yao, wakati huohuo wakiwa na mashamba makubwa yenye watumwa kibao wakiwafanyisha kazi za kitumwa. Bado unaamini binadamu wote ni sawa? Muone! wapo binadamu wengine ni sawa zaidi ya wengine - usipoelewa hapo sio tatizo langu.

Ndio maana kuna watu wanakunywa na kupikia tope huko Lindi kwa kukosa kisima cha Milioni 5, huku wengine wanapiga vigeregere mbele ya Dreamliner la Bilioni 500, na baadhi yao hawatalipanda hadi wazeeke wafe. Si binadamu wote ni sawa. Umeelewa we tumbili?

Elimu ni ufunguo wa maisha eti? He hee! Daah. Ungejua! Kuna profesa aliwahi kujizolewa umaarufu na kuonekana moja wa watu muhimu katika kuamua mustakabali wa nchi, leo ni mpumbavu mbele ya mtu aliyeghushi vyeti vya PhD! Unatoa macho? Jichunge na vumbi.

Elimu haiondoi ujinga, bali inampa mtu uwezo wa kuujua zaidi ujinga wake ili ajichunge, na hiyo haimaanishi kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Ujinga ndio ufunguo wa maisha na kadiri unavyokuwa mjinga ndivyo unavyofanikiwa zaidi- kama alivyosema mwandishi nguli wa zamani Mark Twain; "Ili ufanikiwe maishani unahitaji vitu viwili, Ujinga na kujiamini". Wajinga wengi wanaojiamini wametoka kwenye maisha kuliko wanaojifanya werevu... Ujinga ndio ufunguo wa maisha. Wewe endelea kujifanya mwerevu kwa sababu eti ulifaulu darasani! Faulu na maisha sasa! Ha haaa.

Tuache sisi wajinga tukomae na mapambio ya kusifu - kusifu - kusifu na kuabudu...na tukishateuliwa -nakwambia mtakoma. Mlijifanya sana kufaulu darasani sisi tukawa tunawachora tu... Eti wataalamu, utaalamu bongo!!! mapimbi wakubwa!
#JingaMimi
 
Unadhani watu hawajakichoka chama ccm kilicho kaamadarakani miaka 60? Na bado kinahubiri mambo yaleyale miaka yote na bado kimeshindwa kutekeleza yale wanayo yasema, Hufikirii watu wamechoka zaidi?.
Uchaguzi Serikali za Mitaa tukaambiwa tususie tukatii amri na kusubiri tamko, kimya! Yenyewe kwenye ubunge yakaingia kichwa kichwa bila kurekebisha kasoro zilizokuwepo..."yameibiwa kura" yanatuambia tuingie barabarani huku wengine wakikimbilia ubalozini... Tukisema hawa ni wapinzani kwa ajili ya matumbo yao utabisha....na sinema ndio kwanza inaanza ngoja uone wanavyopigania viti maalumu ndio utajua!
 
Kwa yaliyotokea katika Uchaguzi huu, wananchi wengi sana wataacha kwenda kupiga kura kuanzia wana-CCM wenyewe,wasio na vyama na zaidi wafuasi wa upinzani...
Tatizo tutalolikabili kama Taifa kwa hivi saaa ni Bwana yule, kuamua kuwachagulia wananchi wa nchi hii ni viongozi gani wa kuwawakilisha.

Na yule atakayepinga udhalimu huo anafunguliwa mashtaka ya ugaidi!
 
Kwa yaliyotokea katika Uchaguzi huu, wananchi wengi sana wataacha kwenda kupiga kura kuanzia wana-CCM wenyewe,wasio na vyama na zaidi wafuasi wa upinzani...
Endeleeni kususa uchaguzi Kama mlivyofanya serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili muendelee kula kichapo halafu mpeleke mashtaka kwa Amsterdam.
 
Kwa yaliyotokea katika Uchaguzi huu, wananchi wengi sana wataacha kwenda kupiga kura kuanzia wana-CCM wenyewe,wasio na vyama na zaidi wafuasi wa upinzani...
Watanzania wazalendo tutapiga kura. Wewe unatupangia kama nani?
 
Kwa yaliyotokea katika Uchaguzi huu, wananchi wengi sana wataacha kwenda kupiga kura kuanzia wana-CCM wenyewe,wasio na vyama na zaidi wafuasi wa upinzani...
Uchaguzi huu Tundu Lissu alitumia muda mwingi kuwakatisha watu tamaa wasiiamini tume. Ndio maana wafuasi wengi wa Chadema hawajapiga kura na Chadema imeshindwa vibaya.

Chaguzi zijazo itategeme na jinsi kauli za wagombea zitakavyokuwa. Kama wapinzani wataendelea kukatisha watu tamaa kupiga kura, watu wachache watapiga kura, lakini CCM itaendelea kushinda kwa kishindo kwa kuhamasisha wafuasi wake wakapige kura.
 
Kwa Akili za Meko atafurahi sana. Maoni yangu ni kuwa hakuna kususia uchaguzi. Wananchi waendelee kupiga kura na kushiriki kampeni ili ukweli wa wizi wa Meko and co udhihiri.

Nyani asiachiwe shamba mpaka kitaeweke siku watanzania akili ikichoka wizi wa kura
 
Kwa yaliyotokea katika Uchaguzi huu, wananchi wengi sana wataacha kwenda kupiga kura kuanzia wana-CCM wenyewe,wasio na vyama na zaidi wafuasi wa upinzani.
Sisi CCM hatujawahi wala hatutawahi kususia uchaguzi,nyie suseni sisi tunakula
 
Hajahaha
Kwa yaliyotokea katika Uchaguzi huu, wananchi wengi sana wataacha kwenda kupiga kura kuanzia wana-CCM wenyewe,wasio na vyama na zaidi wafuasi wa upinzani...
Hahahaha yaani kila siku mnalalamika, kabla ya kuja Lisu mlisema hamtapiga kura, alipokuja mkasema lazima mpige kura mumtoe jiwe, mmeshindwa mmeanza tena kuwa hamtapiga kura ssa wapi mnashika nyie?
 
Uchaguzi Serikali za Mitaa tukaambiwa tususie tukatii amri na kusubiri tamko, kimya! Yenyewe kwenye ubunge yakaingia kichwa kichwa bila kurekebisha kasoro zilizokuwepo...
Hii hatari itahamia ndani ya chama cha ccm kuko ndiyo moto utawaka vile tena meko atakuwa anawarekodi sim zao na kumwaga hadharani hahhaa!
 
Back
Top Bottom