Mpaka sasa vyakula vinavyoongoza kwa kuchukiwa:
1. Kabichi: Kabichi tatizo lake kubwa ni mapishi. Haitakiwi ipikwe yenyewe, lazima itiwe vikorombwezo hasa nazi au ichanganywe na nyama nk ndio italika. Pia kabichi ni nzuri kama una mboga nyingine mf maharage
2. Choroko: Choroko japo sio nzuri saana, ila kidogo zikipikwa na nazi nyingi zinavumilika na unaweza kula na wali tu, sio ugali pls! Pia ukiwa na mboga ya majani pembeni itasaidia zaidi
3. Mlenda: Mimi binafsi kama mlenda ndio chakula pekee kilichobaki duniani, basi mi ntakufa njaa tu sitakua na namna nyingine
4. Njugu mawe + mbaazi: hizi kwakweli tukubaliane tuu hata mimi mwenyewe hazipandi ni kula usife mradi siku kuzisogeza
5. Kongoro: Kongoro lile hua halina mapishi mengine zaidi ya hayo, kwahiyo kama huliwezi unaacha tu, haina kubembelezana
6. Utumbo: Utumbo una sheria mbili kuu za kuupika ili ulike: 1) Kabla ya kuupika hakikisha UNAUOSHA SANA ikiwezekana tumia sabuni, jiki, stili waya nk we osha tuu! 2) Chemsha sanaa kuanzia masaa manne na kuendelea hakikisha umelainika kabisa ndembendembee! Ukizingatia hayo, utahitaji kitunguu swaumu na kitunguu maji tu unapata bonge la kituu.. au unaunga na kabichi/mchicha na nazi unakula ugali mkubwa hivi.....!
Itaendelea