Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 76,039
- 230,142
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hukupata za nazi kwa mam ntilie kwani? 😂 Hiyo makitu uipate na maandazi /mahamri, dah utatafuna hadi vidole aisee! 🤣 🤣 🤣Aisee nimekula mbaazi, hii kitu sitokula tena
Kwanini sasa, zile mbona tamu hataree!
Hapo namba sita, dah. Utumbo waupitisha kwa waya na sabuni, wewe dingi kweli! 🤣 🤣 🤣Mpaka sasa vyakula vinavyoongoza kwa kuchukiwa:
1. Kabichi: Kabichi tatizo lake kubwa ni mapishi. Haitakiwi ipikwe yenyewe, lazima itiwe vikorombwezo hasa nazi au ichanganywe na nyama nk ndio italika. Pia kabichi ni nzuri kama una mboga nyingine mf maharage
2. Choroko: Choroko japo sio nzuri saana, ila kidogo zikipikwa na nazi nyingi zinavumilika na unaweza kula na wali tu, sio ugali pls! Pia ukiwa na mboga ya majani pembeni itasaidia zaidi
3. Mlenda: Mimi binafsi kama mlenda ndio chakula pekee kilichobaki duniani, basi mi ntakufa njaa tu sitakua na namna nyingine
4. Njugu mawe + mbaazi: hizi kwakweli tukubaliane tuu hata mimi mwenyewe hazipandi ni kula usife mradi siku kuzisogeza
5. Kongoro: Kongoro lile hua halina mapishi mengine zaidi ya hayo, kwahiyo kama huliwezi unaacha tu, haina kubembelezana
6. Utumbo: Utumbo una sheria mbili kuu za kuupika ili ulike: 1) Kabla ya kuupika hakikisha UNAUOSHA SANA ikiwezekana tumia sabuni, jiki, stili waya nk we osha tuu! 2) Chemsha sanaa kuanzia masaa manne na kuendelea hakikisha umelainika kabisa ndembendembee! Ukizingatia hayo, utahitaji kitunguu swaumu na kitunguu maji tu unapata bonge la kituu.. au unaunga na kabichi/mchicha na nazi unakula ugali mkubwa hivi.....!
Itaendelea
Changanya na zako mkuu 😀😀Hapo namba sita, dah. Utumbo waupitisha kwa waya na sabuni, wewe dingi kweli! 🤣 🤣 🤣
Ah nishashiba tayari... 😂 😂 😂Changanya na zako mkuu 😀😀
Hahahaha , ata mm hawa wadudu wapite kushoto aiseeKumbikumbi nilionja mmoja tu nikahisi nakula mende.
Ukila mchicha sana mchawi hakuoni! ila wewe unamuona na ukila mbegu zake mtu awaye yeyote hakutetiMCHICHA siupendi tangu nikiwa tumboni kwa mama, mama yangu leo akiona nasema siupendi uwa anacheka sana, anasema niliuchukia tangu nipo kwake, alikuwaga ad anazidiwa akinusa harufu ya mchicha
Sent from my Pixel 2 XL using JamiiForums mobile app