Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Mishkaki ya nundu!!
Jmn mbona mnakula mafuta namna ile
I felt like nakunywa Korie moja kwa moja
Nilishindwa kwa kweli na siwezi rudia
Mi tamu balaa[emoji39][emoji39]
 
Ndiyo maana nimeshangaa, yaani wengine home kulikua kunapikwa nguna mchana na usiku na asubuhi mnanywea chai kiporo aaih nilikua namind kunywa chai na kiporo cha ugali ila mama anasema ukitaka kula usipotaka acha njaa ikukomeshe😀
 
Mtu yuko serious kbsa anakutuma buchani ukamnunulie utumbo wa ng'ombe

halafu anakwambia eti "huu nikiunga na nazi,utajilamba nakwambia" yaniiii

huo utumbo hata ukatie humo noti za elf kumi kumi upike siliii ng'o,hata harufu staki iskia...
Ni mtamu sana...[emoji39][emoji39][emoji39]
 
Aisee umenipa somo zuri...nilikuwa najua fillet ni stek ya kawaida tu ambayo haina mfupa
 
Ndiyo maana nimeshangaa, yaani wengine home kulikua kunapikwa nguna mchana na usiku na asubuhi mnanywea chai kiporo aaih nilikua namind kunywa chai na kiporo cha ugali ila mama anasema ukitaka kula usipotaka acha njaa ikukomeshe[emoji3]
Ila hapa kwenye Kula kipolo cha ugali na chai asubuhi umeniokota [emoji3][emoji3]

Unasound was kishua sn

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Supu ya maboga ptyuuuu nilitaka kurudisha change ugenini na soda ya novida.
 
Bro bila shaka utakua mu adventist

Wali wa samli ulinishinda...
 
dah,poleni wote ambao mnapata shida kwenye baadhi ya vyakula.
 
Mie nilikula konokono..mwanzoni utamu wake ulikua kama firigisi.Shida ilikuja pale mwenyeji wangu aliponiuliza unajua ulichokula?Doh zile hisia nikikikumbuka natamani kutapika hadi utumbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…